1: Ukiambiwa leo ufanye kitu ili wenzako wafurahi kama wewe utafanya nini na kwa watu wa aina gani?
2: Je kulingana na furaha uliyonayo kwa leo unaweza kumsamehe mtu ambaye mlikuwa hamna mahusiano mazuri hapo zamani na kosa gani hilo ambalo kwa leo unaweza kusamehe?
3: Mimi huwa sipendi kufurahi sana napenda furaha kiasi je furaha uliyonayo leo inaweza kukufanya ukahuzunika?
4: Siku ya leo ni siku ambayo unaadhimisha siku yako ya kuzaliwa je unahisi baada ya kuondoka duniani siku hii itakuwa na furaha kwa waliobaki au itapotezwa na siku yako ya kufa?.
5: Tarehe ya leo ina siri gani kwenye maisha yako? (mimi kwenye saini yangu huwa naiweka tarehe yangu ya kuzaliwa ila kwa kificho sana. Je wewe hii tarehe (17) ina siri gani kwenye maisha yako ukiacha kuzaliwa?
6: Leo ukipewa nafasi ya kukutana na role model wako utakutana na nani?.
7: Kuna mtu wako wa karibu ambaye mna-share tarehe ya kuzaliwa?.
8: Niambie matukio makubwa maishani mwako ambayo yametokea kwenye mwezi huu wa kuzaliwa kwako.
9: Una utaratibu gani kwenye kusheherekea siku yako hii, huwa unajumuika na watu gani?.
10: Siku ya kwanza unajitambua na kuanza kusherehekea siku hii ya kuzaliwa ulikuwa wapi na kwanini ulipata msukumo wa kufanya hivyo?
1. Nitakachofanya nikupresent kazi zote tulizopewa kwa maana nipo masomoni.
2. Ni kawaida yangu ninapofurahi huwa nasamehe wote walionikwaza kwani hata mimi huwa napenda kuomba msamaha pale ninapokosea.
3. Hapana, kwani furaha yangu mimi sinywi pombe kiasi kwamba baada ya furaha nikahuzunika juu ya hela nilizopoteza kwa kununua pombe.
4. Baada ya kuondoka duniani ni kweli kabisa siku hii itapotezwa na siku yangu ya kufa.
5. Bahati mbaya sijafuatilia hilo lakini kuna utafiti niliwahi kuufanya na kupitia kwa watafiti mbali mbali nimegundua kuwa tarehe 17 June ni siku ambayo Nabii Issa (A.S) au kama kwa wengine wanavyoamini kuwa, ni siku ambayo Yesu alizaliwa, na hii ni kwa mujibu wa watafiti waliowahi kufanya utafiti juu ya kipindi/majira aliyozaliwa Yesu miaka hiyo.
6. Nabii Muhammad (S.A.W).
7. Hapana.
8. Hakuna matukio makubwa.
9. Huwa najumuika na watu walionizunguka, nikiwa nyumbani huwa najumuika na familia yangu, mbali na nyumbani hujumuika na walionizunguka kwa muda huo.
10. Siku ya kwanza kuanza kusherehekea siku yangu ya kuzaliwa nilikuwa shule na kilichonisukuma ni kwamba kulikuwa na kibinti nilikuwa nakimendea miaka hiyo.
Natumai nimejibu maswali yako.