Niulize swali lolote kunihusu leo

Ndugu yangu, hakuna kipindi kibaya kwa binaadamu yoyote wakike au wakiume kama kipindi cha baleghe, kwa maana mtoto wa kike katika kipindi hicho ndipo atakapojiona kuwa yeye ni mwanamke kamili na mtoto wa kiume ndipo atakapojiona kuwa ni mwanaume kamili. Kwa maana katika ukuaji ile ni hatua mbaya na ni swala la kumshukuru Mungu kwa kutuvua salama na mabalaa ya kipindi hicho. Maana ndio kipindi ambacho kitamharibu mtu au kitamfanya kuwa mwema.
 
Sawa kakangu wa faida!
Ila mpaka ukajiita beberu we ulikuwa shidaaa
 
Mwana JF yupi wakike na kiume wanaukuvutia zaidi?
Kwa nini?
Swali lako ni dogo lakini majibu yake ni mengi. Hapa napenda niwe muwazi zaidi kulingana na mitizamo tofauti niliyonayo. Wanajf wengi wananivutia kutokana na stori pamoja na mawazo, michango yao kulingana na mada mbali mbali zinazojadiliwa, bahati nzuri kila mmoja anaupeo mzuri wa kuchambua mambo kulingana na mtizamo wake, hivyo naweza kusema wanajf wote wananivutia kulingana na michango, mitazamo yao kulingana na mada husika zinazojadiliwa.
 
Nimekubali kishingo upande. Me naamini kuna mtu tu ukikuta hata comment yake unajihisi kuenjoy.... Lkn tuache.
 
Sawa kakangu wa faida!
Ila mpaka ukajiita beberu we ulikuwa shidaaa
Baleghe ni kitu mbaya sana na bahati nzuri hakuna yeyote anaeingia kwenye utu uzima bila kupitia baleghe.
 
Ushawahi kudanganya ili kukamilisha misheni flani?
Unaweza kutusimulia kidogo?
Kudanganya ni kweli nishawahi. Kuna kipindi niliwahi kuwadanganya wanawake ambao nilikuwa nao kwa wakati mmoja na kila mmoja kipindi nipo nae nilimwambia kuwa yeye ni wa pekee kwangu na nikiondoka kwake nikienda kwa mwingine nae namwambia hivyo hivyo. Ila kwasasa nimeshakuwa mtu mzima. Nishaacha mambo hayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…