Foxhound
JF-Expert Member
- Dec 15, 2013
- 28,710
- 76,243
- Thread starter
-
- #81
Vijana wengi siku hizi huwa wanaingia ndoani bila kujua/kupata mafundisho ya ndoa kiasi kwamba kwenye ndoa zao ni ugomvi, maneno na kupigana kila siku.Mkeo akikukasirisha huwa unachukua hatua gani kupunguza hasira zako.
Pia ukimkasirisha huwa unafanya nini kumrudisha normal?
(Jibu lako mabechela tunaweza kujifunza)
Kwanza kabisa unatakiwa umjue mkeo ni mtu wa namna gani na ukishamjua hapo haikupi shida jinsi ya kutatua mitafaruku ya ndoani kwako na lau kama ukioa kufata mkumbo ndio utajikuta kila siku unashinda majukwaani kuomba ushauri juu ya ndoa.
Tukizungumzia ndoa ni kitu sensitive sana kwani jinsi sisi wanaume tulivyo na utofauti basi na ndivyo wanawake nao walivyo na utofauti.Ila cha msingi ni kumwelewa mwenza wako nae akuelewe mkiwa hivyo hamtosumbuana wala kupigana. Wanawake huwa wanapenda sana kubembelezwa na kutunzwa zaidi ya lulu au mboni ya jicho. Usioe ili tu kwa vile utaondoa kizuizi cha kupata ukitakacho bali oa ukiwa na uhakika sasa unakwenda kumchukua mtoto wa kike kwao toka kwenye mikono ya wazazi wake na wewe ndio utakuwa kila kitu kwake.