Niwalipe au niuze deni la Bodi ya Mikopo?

Niwalipe au niuze deni la Bodi ya Mikopo?

Ipo hivi, mimi ni Mtumishi wa Serikali idara elimu, daraja langu ni E, nakatwa kiasi cha laki Moja na elfu arobain na nane mia tano (148,500/) kwa kila mwezi kama malipo ya deni la Bodi ya Mkopo.

Kwa sasa nikisoma deni langu kupitia salary slip ni millioni tatu na nusu. Katika mazungumzo yangu na mwajiriwa wa serikali leo kaniambia anashukuru kamaliza deni la bodi na kanishauri na mimi nifanye mpango wa either kuuza deni ama kuwalipa bank in a lump sum.

Ukitazama hii pesa iliyobaki tafsri ni bodi watanikata hadi 2025, nimebaki njia panda. Ipi njia nzuri na salama ya kumaliza haya makato kwa ushauri wako?
Inategemea,me ilipobaki kama 150000/= niliwaibukia mwanza nikaongea nao nikawalipa tena kupita sim tu Kwa Ile control number iliyopo kwenye account yangu ya LOANBORD then siku hiyohyo walinitumia barua ya kumaliza deni nkapeleka utumishi wakafuta deni kwenye mfumo
 
Mimi sijui hata nadaiwa bei gani maana sijawahi kulipa mpaka leo ila nahisi plus riba itakuwa nadaiwa pesa ndefu sana maana nmemaliza kitambo kweli...
Wanakata sawa tu,baada ya miaka 8 ya utumishi hatimae juz wameanza kunikata ,sikuwa na mpango wa kulipa kabisa
 
Hilo deni huwa halilipwi kwa pupa/mkupuo acha wakate taratibu unaweza shangaa sera zinabadilika linafutwa lote kama walivyofanya kwenye retention fee. Kiufupi ni deni la kisiasa na kuviziana
Wewe jamaa lazima utakuwa uligombea ubunge wajumbe wakakupa kura 1,unaonekana kuwa mwanasiasa mtata... Au ni mfuasi wa yule jamaa aliyetuahidi kutupeleka Birmingham kuishi😂
 
Hilo deni huwa halilipwi kwa pupa/mkupuo acha wakate taratibu unaweza shangaa sera zinabadilika linafutwa lote kama walivyofanya kwenye retention fee. Kiufupi ni deni la kisiasa na kuviziana
Hapo kwenye kuviziana unawezashangaa ameviziwa yeye na deni likaongezeka!
Kama ana uwezo wa kulipa mwache alipe
 
Back
Top Bottom