Niwasikilize ndugu au niamue mwenyewe

Niwasikilize ndugu au niamue mwenyewe

ngwesa

Member
Joined
Jan 27, 2012
Posts
24
Reaction score
1
Ni miez 5 tangu nitengane na mke wangu nahitaj kumrudia lkn ndugu zangu hawataki hasa mama. nifanyeje? nishaurini.
 
Weka sababu za kutengana nae ndio ushauriwe. Huwezi kutatua tatizo kama hujui source!
 
Alichokiunganisha Mungu binadamu asikitenganishe, wewe na mkeo ndio mliweka agano, wao wanakukatalia wakati wametulia na wenza wao tuli? nachokuambia maadam ulimuoa, wakakubali, baasi waambie mlikuwa na matatizo madogo na yameisha.la muhimu ni wewe ndio unaenda kuishi nae na sio wao
 
Mkuu ukisikiliza ya watu utaumia sana ikiwa watakuingilia kwenye ndoa yako. Mpe mama heshima yake lakini mwambie kuwa ndoa yake ni personal life.

Kama alivyosema BB hapo juu kuwa kama walimkubali mwanzo whats the problem now.
 
Ni miez 5 tangu nitengane na mke wangu nahitaj kumrudia lkn ndugu zangu hawataki hasa mama. nifanyeje? nishaurini.

Hope we mwenyewe unajua umuhimu wa mama, ndugu na mke. Mama/ndugu wanataka uachane na mkeo, je wewe unataka nini? Kile utakacho ndo ukifuate lakini be ready to take the risks.
 
Kwani mkeo anatabia gani? sababu sio rahisi mama mkwe akasema hamtaki mkwewe bila sababu yamsingi? au wewe mwenyewe ndio unamjua zaidi mkeo kuliko mzazi wako kama unahisi anastaili kupewa nafasi nyengine,ongea na Bimkubwa akuelewe ....
 
Kwani mkeo anatabia gani? sababu sio rahisi mama mkwe akasema hamtaki mkwewe bila sababu yamsingi? au wewe mwenyewe ndio unamjua zaidi mkeo kuliko mzazi wako kama unahisi anastaili kupewa nafasi nyengine,ongea na Bimkubwa akuelewe ....
aliyewaunganisha MUNGU binadamu asiwatenganishe
 
walikutafutia woa huyo mke mpaka ushikiwe maamuz...ngoja nikuambie kaka,kuna umri ambao mzazi ana uhuru wa kukufanyia maamuz,pia inafika umr mzazi hatakiwi kukufanyia maamuz ila anashirikishwa/kueleweshwa tu kwenye mambo yako.so kaz kwako,km bado upo kwenye wakat wa kufanyiwa maamuz au kuamua mwenyewe na kumshirikisha mzaz.
 
Tuambie kama kuna tatizo lingine la kutengana. Kama hakuna mrudishe mkeo tofauti zenu mtazimaliza wenyewe.
 
aliyewaunganisha MUNGU binadamu asiwatenganishe

Walishajitenganisha wenyewe kabla na wasingefanya hivyo bila sababu> Iwapo mama alishirikishwa hapo kabla juu ya uamuzi wa wawili hao vipi asishirikishwe sasa uamuzi unapobadilika?
Mke walitengana na maisha yakaenda jee mama anaweza tengana nae? Nafikiri ni kuendelea kumshauri mama juu sababu ya uamuzi wake hadi aafiki.
 
huyo mke ulimuoa wewe au walioa ndugu zako?

hayo ndo matatizo ya ndoa za kiafrica, mwanamke akiolewa ukoo mzima unafikiri umemuoa, kila mtu atapanga sheria na kanuni zake juu ya mwanamke.....

la hasha, ndoa ni watu wawili, wewe na mkeo hakuna cha mama, baba, wala ndugu, mama na baba wana ndoa yao wakaijenge , kaka ana ndoa yake akaijenge na kama hajaoa aoe ashughulike na ndoa yake, wewe una ndoa yake simama kama mwanaume ufanye maamuzi.... ukipelekeshwa na ndugu utawezaje kusimamia nyumba yako?

angalizo:
unless mke awe amekufanya jambo baya, mfano kukusagia chupa kwenye ugali, au umemfumania nk.........

ila kama ni migongano midogo midogo hebu mrudishe
 
Nimeona Kama Umesema Mke wako; Ulifungishwa ndoa wewe, mke na ndugu?


Chukua mke yako weka Home and endeleza Maisha Ngwesa.


Ni miez 5 tangu nitengane na mke wangu nahitaj kumrudia lkn ndugu zangu hawataki hasa mama. nifanyeje? nishaurini.
 
Mkuu wewe ndiye chanzo cha kuvunjika ndoa yenu.
Dhambi hii itakugharimu sana kama hautajirudi na kuwa imara. Sifa mojawapo ya mwanandoa ni kumlinda na kumtetea mwenzake.
 
Mpaka watu wasiohusika wanakuingilia kwenye masuala yako binafsi kama haya unakua una tatizo wewe mwenyewe!
 
Ndugu jamani! Hao ndugu hawana miji yao? Mrudie mkeo muendeleze maisha.
 
Back
Top Bottom