Niwezeshe kutimiza ndoto yangu

Niwezeshe kutimiza ndoto yangu

Mkuu muleta maada kwanza kabis nikupongeze sana make hizi ndo moja ya investment ambazo zinaweza watoa WATANZANIA, kama kuna uwekezaji wenye tija moja wapo ni huu wa kwako, na kinacho takiwa ni kuwa na VISION nzuri, Na ni bora na wengine tukawa tunajifunza kutoka kwa jamaa hapa, mleta maada hata akipresent hii proposal yake mahali fulani watu wanaweza kumuelewa,

- Ni bora watanzania tuachane kabisa na Biashara za uchuuzi ambazo hazina tija kabisa na tujikite kwenye project za aina hii na zinginezo ambazo zinatija kwa Taifa,

- Na vitu kama hivi ndo vinatakiwa kupewa kipa umbele badala ya jamii kuwekeza kwenye Anasa, kama Harusi zisizo kuwa na Tija kwa Taifa, na kiwango anacho omba mlete thread ni kidogo sana ambacho hata Ndugu, jamaa na marafiki wangeweza kuchangia lakini Ndugu, Jamaa na marafiki hawawezi changia kwa sababu hakuna ulaji kwao, hapo mleta thread angetangaza kuoa zingeisha patikana

-ok mkuu nitafanya process nitakutumia, ingawa kwa sasa niko mbali kidogo, ila nitakutumia mchango
,

Natanguliza shukrani kwa mchango wako; kwa mtazmo huu naamini tutafika tunapotaka kufika.
 
Nashukuru Mkuu Malila; Kwa kweli ninawakumbuka sana kwa changamoto tunazoendelea kupeana, napata update za KILIMOTZ; Pongezi za pekee kwako kwa kazi njema unayoendelea nayo,nawatakia kila la kheri kwa hatua mliyofikia, nitaungana nanyi baada ya kupata utulivu kidogo hapa makao mapya. Baada ya kuotesha mbegu ninazotarajia, nitakupa matokeo yake na baada ya hapo nitaweza nitakushauri njia sahihi. Nategemea mchango wako, Niwezeshe......!!!

Mi nakuahidi buku kumi, nishitue jioni nikurushie voda. Kwa habari za KILIMOTZ,mambo ni mazuri hata sijui nikuelezeje. msimu uliopita ulioishia april tumeotesha miti ya mbao isiyopungua milioni moja na ushee. msimu ujao lengo tupande miti milioni mbili hivi na ushee. Yaani baadae tuje tuwe akina SAO HILL ktk biashara ya mbao.

Naomba nikutie moyo, Watz hela wanayo, kama utafanikiwa kuonyesha matumizi sahihi ya michango yao,naamini utafunika sana. Haya nayaona kupitia KILIMOTZ.
 
Mi nakuahidi buku kumi, nishitue jioni nikurushie voda. Kwa habari za KILIMOTZ,mambo ni mazuri hata sijui nikuelezeje. msimu uliopita ulioishia april tumeotesha miti ya mbao isiyopungua milioni moja na ushee. msimu ujao lengo tupande miti milioni mbili hivi na ushee. Yaani baadae tuje tuwe akina SAO HILL ktk biashara ya mbao.

Naomba nikutie moyo, Watz hela wanayo, kama utafanikiwa kuonyesha matumizi sahihi ya michango yao,naamini utafunika sana. Haya nayaona kupitia KILIMOTZ.

Mkuu MALILA, Natanguliza shukrani kwa mchango wako; kuhusu KILIMOTZ kwa kweli nimekuwa nikipata updates na ninaona mafanikio ya kazi njema uliyoanzisha, ubarikiwe sana kaka. Nimedhamiriwa kuweka taarifa zote hapa ikiwa ni pamoja na michango nitakayopokea na matumizi yake, pamoja na hatua za utekelezaji.
 
Mkuu Mgombezi, na mimi nitakuomba mbegu fupi chache, za kupanda hapo nyumbani kwangu.
Nimejaribu sana kupanda mipapai kwangu Dar lakini inarefuka tuu haizai, sijui tatizo nini. Mbegu huwa natumia za mapapai ninayokula hapo kwangu.
any tips
 
Mkuu Mgombezi, na mimi nitakuomba mbegu fupi chache, za kupanda hapo nyumbani kwangu.
Nimejaribu sana kupanda mipapai kwangu Dar lakini inarefuka tuu haizai, sijui tatizo nini. Mbegu huwa natumia za mapapai ninayokula hapo kwangu.
any tips

Mkuu MUHINDA; mimi nimeshauriwa kununua mbegu (hybrid seed) katika duka la mbegu, kwani zina uhakika wa kutoa mazao. Nikirudi tena katika duka ninalotaka kununua mbegu basi nitakuletea jina la hizo mbegu, kwani nilienda kwa kupata taarifa za awali, wakati nafanya upembuzi yakinifu.
 
Sina comment zaidi kwa hili zaidi ya kukuchangia ili utimize ndoto zako.

Nitatoa kamchango kangu sikubali kuwa sehemu ya wale wanaokatisha tamaa wenzao ila nitakuwa upande wa wale wanao watia moyo wale wanaothubutu kama wewe.
 
Mkuu nimekurushia 5000. Komaa na kazi nitakuja kujifunza kwako nimeshanunua shamba tayari. Nimeanza kupanda miti kidogo ila nahitaji uwezo/uzoefu kutoka kwa wanaJF.

May God bless your work.
 
Sina comment zaidi kwa hili zaidi ya kukuchangia ili utimize ndoto zako.

Nitatoa kamchango kangu sikubali kuwa sehemu ya wale wanaokatisha tamaa wenzao ila nitakuwa upande wa wale wanao watia moyo wale wanaothubutu kama wewe.

Natanguliza shukrani, Mkuu PETER; vile vile nashukuru kwa mtazamo wako huo wa kuwatia moyo wale wanaothubutu.
 
Hongera kaka, l am very much touched. Nimekurushia kidogo nilichokuwanacho Mpesa. 10,000 tu!

Asante for sharing!
 
Mkuu nimekurushia 5000. Komaa na kazi nitakuja kujifunza kwako nimeshanunua shamba tayari. Nimeanza kupanda miti kidogo ila nahitaji uwezo/uzoefu kutoka kwa wanaJF.

May God bless your work.

Mkuu AMKAWEWE, Nashukuru kwa mchango wako. Karibu sana, nitaweka kila hatua; naamini utapata kujifunza.
 
Hongera kaka, l am very much touched. Nimekurushia kidogo nilichokuwanacho Mpesa. 10,000 tu!

Asante for sharing!

Nakushukuru KAUNGA, haba na haba hujaza kibaba.
 
Hiyo tigo,voda au airtel yako umeandika wapi nikurushie buku zako.

Zipo katikati ya maelezo, hizi hapa:

TIGO PESA - 0714 460528 or M - PESA - 0757 941044

Natanguliza shukrani Mkuu.
 
Papai linaweza kutoa paroducts nyingi; bado nahitaji Tsh. 4,935,000/=, kati ya Tsh. 4,970,000/= nilizoomba kwa jamii ili niweze kuanza mradi huu. NIWEZESHE..........!!!

HOMEMADE SKIN CARE FACIALS WITH PAPAYA:
View attachment 55721

Ingredients:

1 cup fresh pineapple

Half-a-cup fresh papaya

1 tablespoon honey

Puree fruit together. Add honey and mix into a smooth paste.

Pineapple and papaya contain natural enzymes and alpha-hydroxy acids that remove dead skin cells while the honey moisturizes the skin. Leave mask on 15 to 20 minutes. Rinse completely.
 
Samahani,
yaani hizo 5,000 ni kama hisa za kua member, au mchango tu wa hiyari but kwenye mavuno hatumo.
 
Mkuu, mgombezi, hakika wewe ni mfano bora kwa wajasiraimali , nkupa pongezi, kweli kabisa bajeti yangu ya kuchangia harusi mwezi huu nakupa wewe, pokea tsh 20,000/= japo kuwa ni kidogo najua kitakufaa sana.
 
Ndugu Wana-Jamii

Ni matumaini yangu mnaendelea vyema na shughuli za kila siku, pamoja na changamoto mbalimbali zinazotukabili. Kwa wale tunaofahamiana kwa kukutana ua namna yeyote ile; MALILA, LAT, KANYAGIO, THE FINEST, na wengine ambao nisingeweza kuwataja wote, habari za siku nyingi…..!!!; kwa muda mrefu sikupatikana sana katika jukwaa hili kama MGOMBEZI, hii ilitokana na harakati zangu za kuhamia hapa mjini Dodoma.

Mitandao ya kijamii imetumika katika kutuunganisha, hivyo basi kila wakati ni vyema kuangalia au kutafuta jinsi ambavyo mitandao hii inaweza kutumika katika kuleta maendeleo ya mtu binafsi na jamii kwa jumla; kama inavyotumika JAMII FORUM. Kupitia mtandao wa FACEBOOK ambao vijana wetu wengi wamejikita huko niliamua kuanzisha kundi (Group) linaloitwa WAJASIRIAMALI KWELI, kwa lengo la kushirikishana elimu ya ujasiriamali na kupeana mbinu mbalimbali za kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika kuanzisha shughuli za uzalishaji mali. Kwa wale wanaotembelea Facebook watakuwa wanaelewa kwamba kwenye FACEBOOK kuna option ya kuunda kundi na kujitengenezea Page. Nimeona ni vyema kuleta mawazo haya pia kwa “Great Thinkers”, ambapo naamini nitapata michango ya kutosha.

WAJASIRIAMAILI KWELI: Log In | Facebook

Dhana ya UJASIRIAMALI katika jamii yetu inaelekea kupoteza mwelekeo au uhalisia. Naamini utaungana nami kwamba mtazamo wa wengi juu ya MJASIRIAMALI, ni pamoja na kununua bidhaa za kichina na kupita nazo mtaani kuuza au hata kama amepanga mahali kuuza. Kwa hiyo basi dhana ya UJASIRIAMALI ni kununua na kuuza (trading), jambo ambalo ninaona kama tunapoteza mwelekeo.

Hiki ni kikundi cha wajasiriamali wakionyesha bidhaa zao; lakini bidhaa nyingi zilizopo ni kutoka china.

MAANA YA UJASIRIAMALI:

Neno ujasiriamali linatokana na maneno mawili ambayo ni UJASIRI na MALI. Hivyo maana ya ujasiriamali ni kuwa na: -

  • Ujasiri au mshawasha wa kutafuta na kupata mali;
  • Uwezo wa kutambua fursa za biashara haraka na uthubutu wa kuzitekeleza fursa hizo pindi zinapojitokeza; na
  • Uwezo wa kuthubutu kushinda vikwazo vinavyoweza kuzuia utekelezaji wa fursa za biashara.

Kwa hiyo mjasiriamali:


  • ni mtu ambaye ana sifa na uwezo wa kutambua mapema fursa za kutengeneza faida na mwenye kuunganisha nguzo kuu za uzalishaji mali (nguvu kazi, mtaji na rasilimali);
  • ni mwanzilishi wa wazo na mwenye maono ya mbali ya jinsi ya kufanya biashara, uwezo wa kupanga, kuratibu na kutekeleza wazo lake na kufikia mafanikio;
  • pia ni mwenye kujiamini, kujituma kwa muda mrefu, kukubali makosa na kujisahihisha, mbunifu na mwenye kuwa tayari kutumia vizuri uwezo na maarifa ya watu wengine

Tunaweza kusema hizi ndizo NGUZO kuu tatu (3) za MJASIRIAMALI:


  1. Ujasiri au mshawasha wa kutafuta na kupata mali;
  2. Uwezo wa kutambua fursa za biashara haraka na uthubutu wa kuzitekeleza fursa hizo pindi zinapojitokeza; na
  3. Uwezo wa kuthubutu kushinda vikwazo vinavyoweza kuzuia utekelezaji wa fursa za biashara.

Hivyo basi mtazamo wa WAJASIRIAMALI KWELI ni kujenga uwezo wa kutekeleza nguzo hizi miongoni mwetu, hasa kwa vijana ambao tunawategemea katika shughuli za uzalishaji mali; kama tusemavyo “VIJANA NDIO TAIFA LA KESHO”. Tutajengana kwa kupeana elimu ya ujasirimali na mbinu mbalimbali katika kushinda vikwazo mbalimbali.

Msemo tunaotumia…, - “TIMIZA NDOTO ZAKO KWA KUCHANGIWA MTAJI” Je una maana gani?

MTAJI NI NINI?

Mtaji ni uwezo unaoweza kutumika katika kuzalisha mali au kuongeza kipato. Kuna usemi unasema “MTAJI WA MASKINI NI NGUVU ZAKE”, kwamba nguzu za mtu zaweza kutumika katika uzalishaji au kuongeza kipato. Katika kuanzisha biashara uwezo huu unaweza kutokana na nguvu alizonazo mtu; kwa maana ya uwezo binafsi juu ya kile anachotaka kufanya, pamoja na rasilimali atakazohitaji.

DHANA YA KUCHANGIWA MTAJI:

Watu wengi wamekuwa na mawazo mazuri katika kuanzisha biashara lakini kikwazo kikubwa ni MTAJI. Katika kutekeleza nguzo namba tatu (3) ya Mjasiriamali; “Uwezo wa kuthubutu kushinda vikwazo vinavyoweza kuzuia utekelezaji wa fursa za biashara”. Nimeamua kutumia dhana ya kuchangiana katika kutekeleza wazo la mtu binafsi katika kuanzisha biashara.

Jamii yetu imekuwa na utamaduni wa kuchangiana katika kutimiza lengo la mtu binafsi; hii imekuwa ikitumika katika kufanikisha sherehe mbalimbali za ndugu au jamaa au rafiki zikiwemo za kuzaliwa, ubatizo, kipaimara, maulidi, harusi n.k. Kwamba mtu anakusanya watu wachache ni kuwaeleza haja ya kufanikisha jambo lake na kuwataka ndugu au jamaa au marafiki kumchangia kwa hali na mali katika kufanikisha jambo hilo.

Hivyo basi kutokana na utamaduni huu ambao tumekuwa tukitumia katika kufanikisha sherehe na shughuli nyingine za kijamii, tunaweza kutumia sasa utamaduni huu katika kutekeleza malengo ya mtu binafsi ambaye anataka kuanzisha shughulli za uzalisha mali au biashara kwa kumchangia mtaji.

Mitandao ya kijamii imetumika katika kutuunganisha, hivyo basi muungano huu tunaweza kuutumia vyema katika kuangalia mahitaji ya wengine katika kutimiza ndoto zao.

Mchango tunaoweza kumpatia mtu ni pamoja na mawazo yetu katika kuboresha wazo husika na rasilimali zinazohitajika.

MRADI WA MAJARIBIO (PILOT PROJECT):

Nikiwa kama mwezeshaji wa kujitegemea, nimeamua kutekeleza wazo langu kwa vitendo kwa kuliwakilisha kwenye jamii kwa lengo la kuomba michango yao, kupitia “NIWEZESHE CAMPAIGN”.

KILIMO CHA MAPAPAI – STAN’S PAPAYA

Kumekuwa na uhitaji mkubwa wa mapapai katika mji wa Dodoma na hata sehemu nyinginezo za nchi kutokana na utafiti mdogo niliyofanya, Bei ya papai katika maeneo mengi ya nchi inakadiriwa kuwa Tsh. 1000 – 3000, hapa Dodoma ni kati ya Tsh 2000 – 3000. Nikiwa kama mjasiriamali nimeona vyema kutumia uhitaji huu kama fursa ya biashara kwa kuanza kilimo cha mapapai ili kwa sehemu niweze kuchangia uzalishaji wa bidhaa hii, ambapo itasaidia pia kupunguza bei katika soko. Dhamira yangu ni papai kumfikia mlaji kwa bei kati ya Tsh. 500 – 1000. Vile vile nimehamasika kuanzisha kampeni ya matumizi ya mapapai, ikiwa ni pamoja kulitumia kama tunda na bidhaa nyinginezo zitokanazo na papai. Unaweza kutembelea page yangu kupitia mtandao wa FACEBOOK ambapo utapata dondoo za matumizi ya papai na mengineyo. Stan's PaPaYa | Facebook


Ili niweze kuanzisha mradi huu nahitaji kiasi cha fedha Tsh. 5,920,000, ambapo mchango wangu binafsi zitakuwa gharama za uendeshaji zitakazo gharimu kiasi cha Tsh. 950,000/=. Hivyo basi mchango wa fedha ninao hitaji kutoka kwa jamii ni kwa ajili ya gharama za uanzishaji (start-up fund), ambazo ni Tsh. 4,970,000/=. Natafuta watu 1000 kutoka katika jamii watakaoweza kunichangia Ts.4970/= kila mmoja.

Nawatafuta watu hawa kupitia mitandao ya kijamii (JAMII FORUM na FACEBOOK) pamoja na jamaa inayonizunguka.
Unaweza kuwakilisha Mchango wako kupitia:

TIGO PESA - 0714 460528 or M - PESA - 0757 941044

(Mwisho ya kupokea michango tarehe 30/06/2012)

Taarifa za kupokelewa kwa michango na utekelezaji wa mradi hatua kwa hatua zitawakilishwa kupitia:

JAMII FORUM - Business & Economic Forum, Katika post hii
FACEBOOK - Stan,s PaPaYa Stan's PaPaYa | Facebook
WAJASIRIAMALI KWELI Log In | Facebook

NB: Ikiwa upo ndani ya Mji wa Dodoma, unaweza kutoa order ya Mapapai na kufanya malipo ya awali. Kiwango cha chini ni mapapai kumi (10) na kila papai utalipia Tsh.500/=

Naomba kuwasilisha..............!!!, Natanguliza Shukrani.......!!!

MAHITAJI YA MRADI:


A: UWEKEZAJI

I: RASILIMALI

MAHITAJI
MAELEZO
KIASI
BEI
JUMLA
Ununuzi wa Shamba
Heka
1
1,000,0000/=
1,000,000/=
Ujenzi wa Nyumba ya Wafanyakazi
Nyumba
1
700,000/=
700,000/=
Bomba – ¾ inch (pvc)
Mita
1500
1000/=
1,500,000/=
Tank la Maji
1000 Lita
1
160,000/=
160,000/=
Pump ya kusukuma maji
1
300,000/=
300,000/=
Bomba la kuvuta maji
Mita
5
10,000/=
50,000/=
Bomba la kupeleka kwenye Tank
Mita
20
3,000/=
60,000/=
Ujenzi wa Mnara wa Tank
1
300,000/=
300,000/=
4,070,000/=

[TD="colspan: 5"]VIFAA VYA UMWAGILIAJI – Umwagiliaji kwa njia ya matone (Drip irrigation systems)
[/TD]

[TD="colspan: 4"] JUMLA
[/TD]

NB: KILIMO CHA UMWAGILIAJI:
Kilimo cha umwagiliagi kwa njia ya matone (Drip Irrigation System), ambapo mabomba (mipira) itapita kataka kila shina la mche na kudondosha matone ya maji yanapohitajika.



II: UPANDAJI

MAHITAJI
MAELEZO
KIASI
BEI
JUMLA
Maandalizi ya Shamba
Heka
1
100,000/=
100,000/=
Mbole – Samadi ya Ng’ombe
Tani
10
10,000/=
100,000/=
Manunuzi ya Mbegu
1000
500/=
500,000/=
Upandaji wa Mbegu
1000
200/=
200,000/=
900,000/=

[TD="colspan: 4"] JUMLA
[/TD]

III: UENDESHAJI

NB: Kutokana na mbegu itakayotumika Mche wa papai utachukua Miezi sita (6) mpaka kuanza uzalishaji.

MAHITAJI
MAELEZO
KIASI
BEI
JUMLA
Mfanyakazi (miezi 7)
Miezi
7
100,000/=
700,000/=
Gharama Nyinginezo
250,000/=
250,000/=
950,000/=

[TD="colspan: 4"] JUMLA
[/TD]

JUMLA YA MTAJI = Tsh. 5,920,000/=

B: JINSI YA KUPATA MTAJI:

Mtaji nategemea kupata kwa kuchangiwa na wana-jamii kama ifuatavyo:

MCHANGO BINAFSI – Gharama za Uendeshaji
950,000/=
MCHANGO WA WANA-JAMII – Rasilimali + Upandaji
4,970,000/=
JUMLA
5,920,000/=

Hivyo Basi Wana-Jamii = 1000
Kila mmoja anaweza kunichangia = Tsh. 4,970/=

***********************************UPDATES***********************************

A: HATUA ZA UTEKELEZAJI:

31/May/2012 - Upatikanaji wa eneo/shamba huko Michese, bado halijalipiwa.



B: MICHANGO KUTOKA KWA JAMII:

[TABLE="width: 587"]
[TR]
[TD]S/NO
[/TD]
[TD]ID
[/TD]
[TD]AMOUNT
[/TD]
[TD]DATE
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]1
[/TD]
[TD]Bakari Kawiza
[/TD]
[TD]5,000
[/TD]
[TD]29-May-12
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]2
[/TD]
[TD]Fadhili Chitanda
[/TD]
[TD]5,000
[/TD]
[TD]29-May-12
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]3
[/TD]
[TD]Amkawewe
[/TD]
[TD]5,000
[/TD]
[TD]4-Jun-12
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]4
[/TD]
[TD]Kaunga
[/TD]
[TD]10,000
[/TD]
[TD]4-Jun-12
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]5
[/TD]
[TD]Rose Lusinde
[/TD]
[TD]10,000
[/TD]
[TD]5-Jun-12
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD]Total contributions as today:
[/TD]
[TD]35,000
[/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD]Total Amount Requested:
[/TD]
[TD]4,970,000
[/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD]Balance:

[/TD]
[TD]-4,935,000
[/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Awesome... Awesome kaka mgombezi....ntafuatilia maendeleo ya mradi wako kwa ukaribu niboreshe na kwangu mkuu.. count me in katika fundraising yako...
 
Mkuu, mgombezi, hakika wewe ni mfano bora kwa wajasiraimali , nkupa pongezi, kweli kabisa bajeti yangu ya kuchangia harusi mwezi huu nakupa wewe, pokea tsh 20,000/= japo kuwa ni kidogo najua kitakufaa sana.

Mkuu MIUONDOMBINU, nakushukuru kwa mchango wako; umepokelewa.
 
Samahani,
yaani hizo 5,000 ni kama hisa za kua member, au mchango tu wa hiyari but kwenye mavuno hatumo.

Mkuu SHARK, nashukuru kwa swali lako; hapa naomba mchango wa hiyari zaidi; bali kuna option ya kutoa order ya mapapai na kulipia awali, lakini hii ni kwa wale wanaoishi dodoma mjini. Kiwango cha chini kwa order ni mapapai 10 na kila papai kwa bei ya Tsh. 500/=; nita - deliver hayo mapapai FEB 2013 wakati wa mavuno.
 
Back
Top Bottom