Mchambuzi wa Masuala ya Siasa na Uongozi, Paternus Niyegira, akizungumza katika mahojiano na Crown Media mnamo Julai 14, 2026, amesema kuwa hakukuwa na haja Msemaji Mkuu wa Serikali kutoa tamko kuhusiana na Makala iliyotolewa hivi karibuni ya BBC kwa kufanya hivyo inabidi ijiridhishe kwanza kuwa na Ushahidi wa kutosha wa ndani.
Ameeleza kuwa kujibu hoja hizo kunaamsha migogoro ambayo tayari ilikuwa inaanza kutulia, na kwamba matamko ya namna hiyo yanatengeneza hofu ya kufungiwa kwa vyombo hivyo vya habari na kuishia kuchochea migogoro mikubwa zaidi.
Ameongeza kuwa mara nyingi taarifa hizo hutolewa kwa makusudi ili kupima uwezo, mipango, na vyanzo vya serikali. Amedai kama angekuwa kwenye nafasi ya msemaji wa serikali, angemshauri Rais na vyombo husika kutovipa nguvu vyombo vya nje kwa kuvijibu, bali kujenga uhusiano imara na vyombo vya habari vya ndani ili kuimarisha taswira ya nchi kimataifa.
Soma pia Serikali: Makala ya BBC haina ushahidi. Tutachukua hatua kulinda uhuru, heshima na usalama wa nchi