Kulikuwa na wakati nilikuwa nasoma katika gazeti la The New York Times, mmoja wa wasemaji wa serikali, Ulli Mwambulukutu, aliandika kitu kukosoa taarifa zilizoandikwa katika gazeti hilo kuhusiana na mambo ya haki za binadamu Tanzania.
Bila kusema chochote kuhusu usahihi wa kilichoandikwa na gazeti la The New York Times au upande wa serikali ya Tanzania, lakini angalau niliona ukisoma kanusho lile la Ulli Mwambulukutu, unaona kanusho la kisomi, kanusho lililoenda shule, yani hata kama lilikuwa na figisu, zilikuwa figisu za kimataifa zilizoenda shule.
Ukisoma kanusho la Msigwa, aibu unaona wewe.
Kuna kipindi Julius Nyerere alikuwa anabishana na Ronald Reagan na Margaret Thatcher, unaona huyu si rais wa Tanzania tu, huyu ni msemaji wa Africa na nchi zinazoendelea zote.
Ukimsikiliza Samia, aibu unaona wewe.
Tumeanguka parefu sana!