Paternus Niyegira Mchambuzi wa Masuala ya Siasa na Uongozi amesema kauli za baadhi ya viongozi wa serikali zinakosa utashi na staha katika uwasilishaji wa hoja zao kwa wananchi.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na Crown Media mnamo Julai 14, 2026, Niyegira ameeleza kuwa Jambo hilo linawalazimu wananchi kuwapinga viongozi badala ya kuwaunga mkono.
"Ukisikiliza mara nyingi kauli za viongozi wetu zinatushawishi tuwapinge badala ya kuwaunga mkono. Ni kitu kinachoniuma. Viongozi wetu walio wengi, ukisikiliza kauli zao, zinatushawishi tuwapinge badala ya kuungana nao."
"Kwa mfano, kiongozi anasimama anakuambia, anasema kwamba kuna mtu mmoja alikuwa analalamika kwamba hospitali haina vifaa, mfano, na alitaka kujifungua, nikamwambia, "Enda ukutane na mume wako, atafute mkasi, amzalishe." Kauli hiyo yaani inatushawishi tumpinge huyo kiongozi, sio tuungane naye mkono. Yawezekana ndio alitaka kusema kwamba kuna mapungufu tu ya kawaida ambayo tunatakiwa kuyavumilia, lakini namna anavyosema ni namna ambayo inakushawishi
Nitakupa, nitakupa mfano mwingine. Kuna mkuu mmoja sasa hivi ni mtu wa juu sana, ni kama ngazi ya tatu. Watu wakasema, "Jamani hizi tozo mbona hatuzielewi?" Akasema, "Asiyetaka aende Burundi." Ni mifano ambayo inakushawishi umpinge na sio kumuunga mkono. Sasa ziko, ziko mifano mingi sana."
Soma pia Kauli ya Mwigulu kuhusu Burundi ni hatari kwa Usalama wa Taifa. Serikali ijitenge nae!