Don Moen
JF-Expert Member
- Nov 12, 2020
- 1,636
- 3,142
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, wananchi wa Meru Arusha wamepigwa na butwaa kwa vitendo vya udokozi na wizi wa vitu mbambali pamoja na vyakula vya aina mbalimbali vilivyoiva au vibichi.
Kumekuwa na malalamiko mengi ya watu kuibiwa hasa jikoni na kuibiwa vyakula kama ugali, ndizi, karoti na chochote kitakachopatikana.
Hali hii imekuwa gumzo hadi kupelekea mchungaji wa Pentekoste Kata ya Ambuereni aitwaye Merinyo
aliyekuwa anaongoza mazishi siku ya leo kuwataka waombolezaji wasimame na kuombea hali hiyo kwani inatishia usalama wa raia.
Hali sio nzuri, tunaibiwa hadi ugali? Hali ambayo haijawahi kutokea katika historia ya Meru...Alisika Mchungaji Merinyo.
Hali hiyo inajitokeza wakati vyakula na mafuta vimepanda bei kupindukia ambapo bei ya mchele imefikia sh.3,500/kg, unga 2,000/kg, mafuta ya kupikia ni 7,500/lita.
Mungu alete mvua hali inatisha.