Njaa haina adabu, uliwahi kukamatwa na njaa kisawa sawa na uliituliza vipi ?

Siku bwana nikiwa na miaka kama minne hivi. Nimdamka zangu usubuhi usubuhi nataka kwenda kukojoa. Nimeamka na njaa sii nikaona chupa ya sprite bwana ipo kwenye corrido nikajua mwanafamilia kaacha. Chap kwa hara nikapiga fundo. Duh! Kumbe mshinze mmoja alikuwa kakojolea mule ndani bwana.
 
Matukio ni mengi;
Nishawahi kuvua samaki wa mtoni na nikawala wakiwa wabichi vilevile.

Kuna siku nyingine njaa ilinipiga sana, nikawa napitapita sehemu usiku kama saa 6, nikasikia harufu ya mkate wa ngano unaiva, ikabidi niingie kwenye kale kajiko na nikaona mlango umeegeshwa tu, basi nikazama ndani.

Nilivyoingia ndani nikakuta kweli bwana mkate ndio unaiva ule mkaa wa juu ndio unazimazima, sasa kwa furaha niliyokuwa nayo ikabidi niimbe kidogo wimbo wa kikongo MUZINAAA. Sasa kumbe kuna jamaa anaitwa ...... na yeye alikuwa amezamia kwenye hicho kijiko na yeye alikuwa anasaka mkate sema alijificha alivyoona naingia alijua ni mwenye nyumba.

Kwa hiyo nilivyoimba Muzinaaa, nikashangaa mtu anaujibu wimbo huku anacheka. Basi pale tukaanza kupiga stori utafikiri tupo kwetu.
Jamaa alikuwa na sado ya togwa ya moto alisema kuna mahali amekwapua usiku uleule.

Sema mimi nilivyoshiba nikamwacha palepale manake nasikia alikuwa na kawaida ya kujisaidia haja kubwa kwenye majiko ya watu akishashiba menyu.
Kwa kisa chako kisicho na miguu, imenibidi kubofya avatar yako kwa taarifa zaidi [emoji848]
 
Siku moja nimepiga mapombe yangu kuanzia sa4 asubuhi hadi sa4 usiku sikula chochote sio kwamba nilikua sina hela sema akili za pombe zinaniambia, acha ujinga usile wewe umeshiba.
Basi bwana nikarudi kiotani kulala ile imefika sa8 natetemeka njaa jasho linatoka Dunia nzima nikajitahidi kuamka nikakata kachumbari ya nyanya mbili na vitungu vitano ndio vilivyoniokoa plus maji ya kunywa lita mbili.
Njaa ya usiku sitaisahau inauma alafu hakuna msosi usiku unakuwa mrefu sana[emoji3]
 
Watu wamepitia mengi sana, ushawahi kufikiria mtu ana njaa hadi anajifunga jiwe kwenye tumbo au analala kifudifudi ili abinye tumbo usiku upite au yale makoko ya ugali yanalowekwa maji ili kesho asubuh iwe ndo breakfast...
 
[emoji26][emoji26][emoji24][emoji24]. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Niliwahi Kaa siku 4 nakula mara moja kwa siku bila kushiba, sababu ya kukosa hela, jioni nakunywa maji mengi ili njaa isiume usiku, usiku wa manane nilipata kichefuchefu cha njaa nikawa natapika maji.
 
Matukio ni mengi;
Nishawahi kuvua samaki wa mtoni na nikawala wakiwa wabichi vilevile.

Kuna siku nyingine njaa ilinipiga sana, nikawa napitapita sehemu usiku kama saa 6, nikasikia harufu ya mkate wa ngano unaiva, ikabidi niingie kwenye kale kajiko na nikaona mlango umeegeshwa tu, basi nikazama ndani.

Nilivyoingia ndani nikakuta kweli bwana mkate ndio unaiva ule mkaa wa juu ndio unazimazima, sasa kwa furaha niliyokuwa nayo ikabidi niimbe kidogo wimbo wa kikongo MUZINAAA. Sasa kumbe kuna jamaa anaitwa ...... na yeye alikuwa amezamia kwenye hicho kijiko na yeye alikuwa anasaka mkate sema alijificha alivyoona naingia alijua ni mwenye nyumba.

Kwa hiyo nilivyoimba Muzinaaa, nikashangaa mtu anaujibu wimbo huku anacheka. Basi pale tukaanza kupiga stori utafikiri tupo kwetu.
Jamaa alikuwa na sado ya togwa ya moto alisema kuna mahali amekwapua usiku uleule.

Sema mimi nilivyoshiba nikamwacha palepale manake nasikia alikuwa na kawaida ya kujisaidia haja kubwa kwenye majiko ya watu akishashiba menyu.
Daah qmmk [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Unaishiwa nguvu, unatetemeka na unaweza kuanguka kabisa.

Ukinywa maji njaa inaongezeka
 
Back
Top Bottom