Njaa haina adabu, uliwahi kukamatwa na njaa kisawa sawa na uliituliza vipi ?

Write your reply...si ungekoroga tu uchi kama atamkavyo bibi yangu ahhhh sorry uji tu mkuu
 
Niliwahi Kaa siku 4 nakula mara moja kwa siku bila kushiba, sababu ya kukosa hela, jioni nakunywa maji mengi ili njaa isiume usiku, usiku wa manane nilipata kichefuchefu cha njaa nikawa natapika maji.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Daaaahhh.
Njaa imenikosakosa kunitoa uhai wangu si mara moja wala mbili.
Ni zaidi ya mara 2 roho yangu iliwekwa rehani na bwana njaa.
Ila Jana ndo ilikuwa kali nilitaka kuanguka kwa njaa huku mfukoni nina misimbazi, kisa tu boss kaweka kikao cha ghafla na Mimi nilikuwa sijapata chai. Kikao kiliendelea mpaka alasiri kumbe wenzangu walishitua tumbo mapema Mimi nilikuwa busy tangu asubuhi.
 
Matukio ni mengi;
Nishawahi kuvua samaki wa mtoni na nikawala wakiwa wabichi vilevile.

Kuna siku nyingine njaa ilinipiga sana, nikawa napitapita sehemu usiku kama saa 6, nikasikia harufu ya mkate wa ngano unaiva, ikabidi niingie kwenye kale kajiko na nikaona mlango umeegeshwa tu, basi nikazama ndani.

Nilivyoingia ndani nikakuta kweli bwana mkate ndio unaiva ule mkaa wa juu ndio unazimazima, sasa kwa furaha niliyokuwa nayo ikabidi niimbe kidogo wimbo wa kikongo MUZINAAA. Sasa kumbe kuna jamaa anaitwa ...... na yeye alikuwa amezamia kwenye hicho kijiko na yeye alikuwa anasaka mkate sema alijificha alivyoona naingia alijua ni mwenye nyumba.

Kwa hiyo nilivyoimba Muzinaaa, nikashangaa mtu anaujibu wimbo huku anacheka. Basi pale tukaanza kupiga stori utafikiri tupo kwetu.
Jamaa alikuwa na sado ya togwa ya moto alisema kuna mahali amekwapua usiku uleule.

Sema mimi nilivyoshiba nikamwacha palepale manake nasikia alikuwa na kawaida ya kujisaidia haja kubwa kwenye majiko ya watu akishashiba menyu.
Nimecheka sana
 
Me nilikula andazi moja la 100 siku ya pili hivyo hivyo siku ya tatu akaja bi mkubwa kuniokoa yaani 200 niliona Kama 10000 sitosahau!
 
Matukio ni mengi;
Nishawahi kuvua samaki wa mtoni na nikawala wakiwa wabichi vilevile.

Kuna siku nyingine njaa ilinipiga sana, nikawa napitapita sehemu usiku kama saa 6, nikasikia harufu ya mkate wa ngano unaiva, ikabidi niingie kwenye kale kajiko na nikaona mlango umeegeshwa tu, basi nikazama ndani.

Nilivyoingia ndani nikakuta kweli bwana mkate ndio unaiva ule mkaa wa juu ndio unazimazima, sasa kwa furaha niliyokuwa nayo ikabidi niimbe kidogo wimbo wa kikongo MUZINAAA. Sasa kumbe kuna jamaa anaitwa ...... na yeye alikuwa amezamia kwenye hicho kijiko na yeye alikuwa anasaka mkate sema alijificha alivyoona naingia alijua ni mwenye nyumba.

Kwa hiyo nilivyoimba Muzinaaa, nikashangaa mtu anaujibu wimbo huku anacheka. Basi pale tukaanza kupiga stori utafikiri tupo kwetu.
Jamaa alikuwa na sado ya togwa ya moto alisema kuna mahali amekwapua usiku uleule.

Sema mimi nilivyoshiba nikamwacha palepale manake nasikia alikuwa na kawaida ya kujisaidia haja kubwa kwenye majiko ya watu akishashiba menyu.

nimecheka knoma afu niko pharmacy mpaka watu waniona sipo serious [emoji23][emoji23]
 
Kuna kipindi nilipiga Pombe za kutosha asubuh naamka ninatetemeka,jasho, na njaa ya kwenda. Ilibidi nitoke saa 12 asubuh home nikaenda kununua supu Kwa Mama ntilie wa uswaz na chapati ndio ikawa pona yangu
 
Nilimaliza form four nikahama mkoa kwenda kutafuta life.Wakuu jamaa nilienda nae alikuwa mshikaji wangu ile tunafika huo mkoa akaniibia begi langu la nguo na kupotea.Mi nilikuwa mgeni basi kufupisha nilipigwa na njaa nikapita sehemu kuna mti una maembe ila bado machanga hayana hata kokwa nilikula yale maembe meno yote yakafanya ganzi na mdomo ukafanya ganzi.Yalikuwa machanga sana.Niliharisha baada ya lisaaa tu hadi nikaishiwa nguvu.Huku brother wangu katika familia anamiliki mabasi ya kwenda mikoani.Basi kama Bahati nikakutana na mwalimu wangu wa Maths alivoniona na anaijuwa familia nnayotokea wana uwezo alidondosha chozi akanitia ten nilimuona ye ndo malaika.
 
Pia kuna haja ya jamii forum kuweka option ya kutuma voice wengine sie sio waandishi wazuri.Pia voice inafupisha mambo mengi.
 
Nilimaliza form four nikahama mkoa kwenda kutafuta life.Wakuu jamaa nilienda nae alikuwa mshikaji wangu ile tunafika huo mkoa akaniibia begi langu la nguo na kupotea.Mi nilikuwa mgeni basi kufupisha nilipigwa na njaa nikapita sehemu kuna mti una maembe ila bado machanga hayana hata kokwa nilikula yale maembe meno yote yakafanya ganzi na mdomo ukafanya ganzi.Yalikuwa machanga sana.Niliharisha baada ya lisaaa tu hadi nikaishiwa nguvu.Huku brother wangu katika familia anamiliki mabasi ya kwenda mikoani.Basi kama Bahati nikakutana na mwalimu wangu wa Maths alivoniona na anaijuwa familia nnayotokea wana uwezo alidondosha chozi akanitia ten nilimuona ye ndo malaika.
Daaaah pole Sana mkuu ila natamani ungeendelea kusimulia yaliyoendelea.
 
Mwaka 2016 nilipiga 60m kwenye machimbo, Kahama.
2017 sikumbuki mwezi gani nilifulia mbaya hata mia sikuanayo. Yaani nikifanikiwa kula leo sikua najua mlo mwingine utapatika lini.

Siku moja nilikua karibu na Kanisa Katoliki jimboni Kahama mida ya mchana, nikaona watu wanaingia Kanisani na jeneza nikajua kuna ibada ya mazishi nikaunganao ibadani.

Ibada ilivyoisha nikajiunga na msafara kwa miguu hadi Nyihogo ,kufika tu msibani tukakuta sahani za wali maharage zinatembezwa ndani ya sinia.( Nikajisemea mkeka umetiki nilikua sijala kitu kwa muda wa siku mbili.)

Nikadaka sahani ya wali maharage kwa kasi ya 5G. Kuna baadhi ya waombolezaji walikosa chakula nikajisemea kimoyoni mbwa kala mbwa.
Mpaka leo hii sijajua jinsia ya yule marehemu, all i know he/she saved my life atleast for a day.
 
Back
Top Bottom