The Sunk Cost Fallacy
JF-Expert Member
- Dec 1, 2021
- 19,582
- 14,167
Habari za mida..
Kuna dalili za njaa mwaka ujao kutokana na Hali ya ukame inayoendelea Nchini kwa sasa.
Sio jambo la kawaida kwa mwezi huu wa disemba mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kutokuwa na mvua.Sehemu nilipo wananchi bado hawajaotesha Mazao kwa sababu mvua hazipo.
Hali ya hewa ni jua,joto,upepo na manyunyu tuu huku nzi wakitamalaki.
Chonde chonde Serikali zuieni kuuza chakula nje ya Nchi maana hivi tunavyoongea bei za Mazao zimeanza kupanda.Hata wale wa mahindi waliokuwa wanalia saizi wanauza kwa bei ya Kati ya 45,000-55,000 kwa gunia huku mikoani.
Ili kunusuru chakula kilichopo,nashauri serikali ipige marufuku exports ya Mazao yote ya chakula.
Kama Hali hii itaendelea ,Wananchi tujiandae kisaikolojia.Ukame umeeneo si tu Tanzania bali Hali ni mbaya zaidi Ethiopia,Kenya na Somalia.
Watu wa Hali ya hewa walitabiri hali hii toka mwezi wa tatu,wakarudia mwezi Juni na mwezi November.
Mwenzako akinyolewa zako tia maji 👇