Njaa inanukia, mvua zimegoma. Serikali zuieni kuuza chakula nje ya Nchi

Nenda shambani ukalime ndio uishauri serikali kuzuia mazao yasiende nje ya nchi
 
Mkulima ndio anyonywe kila siku. Kila mtu anufaike kwa kazi yake. Mbona mafuta yanapanda kila leo, hatuoni jitihada za kupunguza bei. Mwache mkulima apate uhuru wa kuuza kile alichotokea jasho.
 
Mkulima ndio anyonywe kila siku. Kila mtu anufaike kwa kazi yake. Mbona mafuta yanapanda kila leo, hatuoni jitihada za kupunguza bei. Mwache mkulima apate uhuru wa kuuza kile alichotokea jasho.
Bei zikiwa chini mnailaumu serikali na inatimiza wajibu wake kwa kununua.Sasa ni wajibu wa serikali kudhibiti bei kwa maslahi ya Nchi.
 
Hueleweki
bababikko anamaanisha ni jukumu la Faraoh kumteua Yusufu ahakikishe ghala zinajaa vyakula vya kutosha kipindi cha neema.

Yusufu ahakikishe hakuna mwananchi atakufa njaa hata miaka 7 ya ukame ikitamalaki tena ghala zinafunguliwa kwa export na sio kuzuia biashara kuendelea. Hilo ndio jukumu la msingi la serikali.
 
Tuacheni wakulima tule jasho letu,,,,madhira tunayo pitia wakulima hamuyajui, bei za pembebejeo hazikamatiki, naomba tusipangiane, kila mtu apambane na hali yake,
 
Usalama wa chakula ni muhimu sana kwa Nchi kuliko maslahi ya mtu mmja.
Usalama wa chakula isiwe chanzo cha kuwafanya wakulima kupata hasara kwasababu gharama za uendeshaji wa shamba zipo juu kuliko bei yaani pembejeo zote juu kuanzia mbolea insecticide n.k. unategemeana bei ikiwepo chini Nani atamudu gharama za kilimo. Mkulima asiwe yeye ndio wa kuumia waliopo mjini kuanzia machinga , wafanyabiashara, watumishi ndio wanufaike na bei ndogo huku mkulima akiendelea kuwa masikini.inavyoonekana wewe ni mbinafsi unajiangalia wewe mwenyewe pasipo kumuangalia anayezalisha chakula hicho. Jaribu nenda kashike jembe ndio halafu chakula chako uuzie watu Kwa bei ya chini
 
Tukiwa na njaa tunakuwa soko la wengine
 
Point kubwa sana hii... lakin kwasababu serikali hii haipo kwaajili ya wananchi, wapo kwaajili ya utukufu wao tu. Hawawezi kukusikiliza
 
Kwa sisi wakulima kwetu ni sherehe, mvua ivute vute ianze January.

Unadhani hizo bei za mbolea tutaziweza mazao yasipopanda bei? Tumeshapata hasara sana....Mvua ikaze hivyo hivyo.
 
Serikali inatakiwa iwezeshe miundombinu Wananchi wake waanze kutumia njia za umwagiliaji katika Kilimo maana ardhibyetu ina rutuba ya kuyosha tofauti na wenzetu wanaotuzunguka .

katika Soko huralia Serikali haitakiwi kuingilia mwisho wa Siku italeta matatizo ya kiuchumi ndani ya Nchi.
 
Acheni njia primitive za kupambana na matatizo.

Kumzuia mkulima kuuza mazao yake mahali popote anapoona panampa manufaa eti kwa sababu kuna dalili ya njaa, ni njia primitive za kupambana na tatizo la njaa.

Kuna wakati kumewahi kuwa na upungufu mkubwa wa cement nchini, umewahi kusikia serikali ikipiga marufuku viwanda kuuza cement nje ya Tanzania? Kwa nini iwe tofauti kwa mkulima?

Kama Serikali itakuwa imeona kuna dalili ya uwepo wa njaa, ikanunue mazao toka kwa wakulima, ikashindane na wanunuzi wengine, ikayatunze mazao hayo kwenye maghali yake, na siyo vinginevyo.

Halafu, siyo kweli kuwa siyo kawaida kutokuwepo mvua kipindi hiki huko Nyanda za Juu. Labda umezaliwa miaka ya karibuni, na hivyo hujawa na uzoevu wa kutosha wa hali ya hewa ya maeneo ya huko.

Ni mara nyingi tu, maeneo ya Nyanda za Juu kukosa mvua kipindi hiki. Na ukizungumza na wakulima wa huko, hata miaka ya nyuma, utawasikia, 'mwaka huu mvua zimechelewa lakini Christmas lazima zitanyesha, na ikiwa hivyo kutakuwa na mazao mengi mwaka huu'.

Kwa uzoefu wangu, maeneo ya Nyanda za Juu, kukiwa na upungufu wa mvua, huwa wanapata mavuno mengi na mazuri zaidi. Tatizo la Nyanda za juu, mara nyingi ni mazao yao kama mahindi kuoza kutokana na mvua kunyesha kipindi kirefu, maharage kuungua kutokana na mvua kuzidi. Nyanda za juu, kwa wastani mahindi hukomaa ndani ya miezi 3. Hivyo mavuno mazuri ni ya mazao yanayopandwa mwezi Januari au mwishoni kabisa mwa December, ambayo hukomaa mwezi March, na hukauka mwezi April mpaka May. Hata kama mvua zikiwahi, ukipanda mwezi December, mazao hayo huharibiwa na mvua maana yataanza kukauka kipindi ambacho mvua bado zinanyesha.

Kama tutafika mwezi Januari 2022 bila ya mvua, hapo kweli Nyanda za juu wataanza kuwa na hofu ya kupata mavuno mazuri. Sasa hivi tatizo kubwa la mikoa hiyo ni bei ya mbolea, mfuko mmoja umefika shilingi 120,000. Huwezi kununua mbolea kwa bei hiyo, ukaitumie kwenye kilimo cha mahindi, upate faida. Sasa hivi nimeambiwa wakulima wameanza kutafuta mbegu zao za asili ili wasitumie mbolea, maana za kisasa haziwezi kumudu bila mbolea. Kitakachotokea ni mavuno kidogo
 
Serikali inunue akiba ya chakula kwa bei ya soko sio huu ujinga.

Unakuta benki teller naye kwenye kadirisha kake ka kutolea pesa anasema thelikali ithuie uudwaji wa madhao nje......

Lima hata eka mbili ukitegemea wanao waende shule, uvae, ule, ujitibu kwa hayo mazao yako utaelewa papasi.
 
Ugali na maharage kila siku ndiyo chakula tele!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…