Njaa inaweza kutufundisha kuliko Walimu

Njaa inaweza kutufundisha kuliko Walimu

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
324
Reaction score
649
NJAA INAWEZA KUTUFUNDISHA KULIKO WALIMU.

Na Elius Ndabila
0768239284

Kumekuwa na mjadala mkubwa juu ya pembejeo za kilimo kupanda bei mara dufu. Bahati mbaya toka mijadala hii imeanza hakujawa na suluhisho.

Wapo wanaojaribu kutengeneza sababu kuwa kupanda Kwa pembejeo za kilimo kunatokana na Ugonjwa wa Covid 19 na pia Vita ya Urusi na Ukreni. Inawezekana hizi sababu zinaukweli, lakini ninashindwa kuziamini Moja Kwa moja Kwa kuwa bei ya Mahindi au nafaka zingine bei yake haiwiani na bei ya mbolea.

Wakati bei ya Mbolea inakadiriwa kuwa mpaka sasa ni Shilingi 140,000/= kwa mfuko bei ya Mahindi kule kwetu Ileje debe ni shilingi 7,000/= Kwa wastani. Ili mtu aweze kununua mfuko mmoja wa Mbolea inamlazimu auze debe 20 za mahindi. Tafsiri yake mwaka ujao kunaweza kukawa na njaa kali kwa kuwa hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kuuza debe 20 Kwa mfuko mmoja wa mbolea.

Serikali inapaswa kuja na sulujisho ijapo wamechelewa. COVID 19 au Vita ya Urusi na Ukren si sababu zinazoweza kuwa na mashiko kwenye uhai wa binadamu. Kama taifa ni lazima kuwa na vipao mbele. Huwezi kuwekeza kwenye barabara, Shule n.k kama watu wana njaa . Nani atasoma hayo madarasa kama watu wananjaa? Elimu inapatikana Kwa watu walioshiba.

Uhai wa Taifa unategemea zaidi Chakula na Afya. Kukiwa na Chakula mtu atashiba na atapata afya. Mtu akishiba, akawa na afya bora ndipo anapoweza kusoma. Hivyo silaha za kwanza mhimu ni Chakula na afya.

Ushauri wangu kwa serikali walipaswa na Wanapaswa kuchukua walau 50% ya bei ya mbolea ili kumuokoa mkulima. Hii inatakiwa kuja kama dharura. Badala ya kuelekeza fedha nyingi kwenye Wizara zingine, ninashauri fedha nyingi zielekezwe wizara ya Kilimo. Wizara ya kilimo inunue mbolea kwa asilimia 50 ili badala ya mkulima kununua mbolea 140,000/= aweze kununua kwa walau 60,000/=.

Mataifa yote yaliyoendelea Duniani yalifanya mapinduzi kwenye sekta ya kilimo. Taifa haliwezi kuendelea kama kilimo hakijengewi mazingira rafiki Kwa mkulima. Wakulima wengi ambao ndio wanaolilisha taifa hawana uwezo wa kununua mbolea Kwa bei hizo.

Ninaamini fedha zipo ndio maana miradi mingi inaendelea. Lakini miradi mingine inaweza kustishwa ili kwenda kuokoa kilimo. Chakula ndio uhai wa binadamu.
 
Back
Top Bottom