Njaa mbaya sana; Ni jambo gani la hatari uliwahi fanya ulipokumbwa na njaa?

Njaa mbaya sana; Ni jambo gani la hatari uliwahi fanya ulipokumbwa na njaa?

Udom block H enzi hizo. Njaa ya siku mbili inaelekea ya tatu....washkaji room washanisaidia hadi najiona mzigo usiobebeka. Niko kitandani sauti imeanza kukata, nikisimama nahisi kutetemeka kabisa....Mara paap washkaji hawa hapa wanauliza kama nimepata msosi nikajibu tayari kumbe holaa....
Walivoingia room nami nikavunga kama naenda toilet,kumbe moyoni ni kuficha aibu ya kuonewa huruma....pia ni kuwaamisha kwamba nimekula sasa naenda chooni kama wao.
Dah kumbe kule chooni lengo lilikuwa ni kumlilia Mungu kuwa endapo ningekufa asinichome maana tayari cha moto nimekiona huku duniani... Basi wakuu ile nimeingia tu chooni,Niko usawa wa kile choo cha kukaa si nikauona muujiza. Sikuamini kwamba siku ile Mungu alinilisha kutoka kwenye tundu LA choo, wakuu nilikuta 5000/= pesa halali ya Tanzania inaelea kwenye vile vimaji vya choo. Sikujali...niliichukua kwa mkono wangu wa kulia bila kujali usalama wa afya yangu.
Kilichofuata ni direct canteen kula ukoko....maisha yakaendelea.
Aisee hii noma sanaa maana hiyo sio location ya kukuta hela imedondoka kabisaa
 
Tulikwama kijiji flani njaa kali tukampiga mtu kabali tukampokonya muhindi wa kuchoma alikua amebakiza mistari miwili.
Hii chai kabisa, kwa akili zangu timamu siwezi kukubali hii..
3bf74a91f19a552c4b5f7ec22bb5560f.jpg
 
Bora yako ulikuwa na tumaini pesa ipo, hata kukopa ungeweza. ila kasheshe pesa huna na huna ratiba ya kuipata karibuni halafu njaa inakubabua.
Kweli mkuu lakini bado ile njaa ikiyonishika acha tuu. Mchele mbichi umelowekwa halafu nikaweka na sukari maji yake pia nikanywa.

Situation za njaa zimenipata nyingi ila sio kwa kusema nilikuwa sina option kabisa hapana namshukuru Mungu kwa hilo. Sema mimi naogopa sana kukopa ni mara mia nikae njaa ila sio kukopa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilishikwa na njaaa mda wa kujampa nikaweka mkono matakoni Kisha nikanusa ili angalau niufurahishe moyo
 
Udom block H enzi hizo. Njaa ya siku mbili inaelekea ya tatu....washkaji room washanisaidia hadi najiona mzigo usiobebeka. Niko kitandani sauti imeanza kukata, nikisimama nahisi kutetemeka kabisa....Mara paap washkaji hawa hapa wanauliza kama nimepata msosi nikajibu tayari kumbe holaa....
Walivoingia room nami nikavunga kama naenda toilet,kumbe moyoni ni kuficha aibu ya kuonewa huruma....pia ni kuwaamisha kwamba nimekula sasa naenda chooni kama wao.
Dah kumbe kule chooni lengo lilikuwa ni kumlilia Mungu kuwa endapo ningekufa asinichome maana tayari cha moto nimekiona huku duniani... Basi wakuu ile nimeingia tu chooni,Niko usawa wa kile choo cha kukaa si nikauona muujiza. Sikuamini kwamba siku ile Mungu alinilisha kutoka kwenye tundu LA choo, wakuu nilikuta 5000/= pesa halali ya Tanzania inaelea kwenye vile vimaji vya choo. Sikujali...niliichukua kwa mkono wangu wa kulia bila kujali usalama wa afya yangu.
Kilichofuata ni direct canteen kula ukoko....maisha yakaendelea.
Mipango ya Mungu sio sawa na ya mwanadamu, kwenye furaha, kwenye huzuni, Mungu anatupenda

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Eti mtu anaenda ATM siku 3 wakati bank zimejaa tele Dsm
Hizo bank utaenda kwa mguu?? Kutoka Sinza Vatican atlist nearest bank ni pale Millenium tower na ndio kuna ATM na makumbusho ukiachana na hizo za kijiweni na Africasana, je unaweza tembea umbali huo vatican hadi makumbusho??? Let say bank nyingine karibu ipo Shekilango na ndio kuna ATM from kijiweni, utatembea kwa mguu??
Tatizo lenu JF ni kujifanya mnajua judging kila kitu na kuona kila anayeleta mkasa ni mwongo. Au mkuu unafikiri Dar ni kama pale kijijini kwenu unafika popote unapotaka kwa kutembea??

Kwamba ni kabla ya 2008?
 
Njaa inaweza kumfanya mtu afanye jambo la ajabu sana!

Tena usiombe upatwe na njaa ikiwa unga umeisha, mafuta yameisha, gesi imeisha, luku imekata n.k Hakika kuna uchizi huwa unaingia ghafla hata usijue cha kufanya.

Njaa huifanya akili ifanye kazi kwa speed kubwa halafu isipate majibu sahihi!

Njaa huutweza utu!

Njaa inaweza kuifanya akili ikachoka ghafla na kukata tamaa!

Nakumbuka Siku moja nilikuwa sina kitu kabisa, mishe ilikuwa imegoma, njaa ilikuwa inauma balaa, nikapanda daladala nikiwa na mawazo makali hadi nikasinzia kwenye daladala kiasi cha kupitilizwa kituo! Na sikuwa na nauli ya ziada! Nikaamua kuuza saa nikapata 5000 ya nauli na kula!..

Njaa huleta hasira na maamuzi magumu! Njaa huifanya akili Ione kila kitu kitamu hata ukipewa ming'oko utasema keki!

Naomba tuelezane hapa, nikituko gani au jambo gani la hatari uliwahifanya ulipopatwa na njaa wakati huna kitu mfukoni?
Nilizimia nikalazwa
 
Siwezi sahau SUA 2008 nikiwa mwaka 2 nilipojifanya mjanja kutokuandika wala kupeleka jina langu kama ninaendelea mwaka 2 ili walipeleke loan board. Hahaaaa, nilishindia Maji na Indi kwa siku 3 na jamaa wakanichoka wakawa wananinyanyasa kuniwezesha msosi na nauli toka Hosteli to Mazimbu. Vibanda vya mama ntilie madawa, madeni ya msosi kila kona. nilijifanya mgumu na sikutaka sema nyumbani hadi hali ilipokuwa ngumu nilipoanza shindia muhindi na maji, siendi vipindi kwani sina nauli. Ikabidi niwe muwazi kwa sister na mzee wangu. Uzuri sister alikuwa anaishi Kihonda nami nilikuwa naishi hostel za Kihonda Maghorofani. Uncle akawa ananiletea poti lenye msosi kila jioni na mzee kuanza nitumia pesa za matumizi semister nzima. Semister ile nilikuwa na sup 4 na moja ya "Fundamental of Soil Science" ya SHAYONGOI nikaenda piga "third attempt". R.I.P Mzee Swai, ulijitahidi kunijenga na kunisomesha mwanao.
 
Mimi mpka sasahivi ndo hali napitia unapigwa na njaa halafu huku mwenye nyumba anataka kodi.Wiki iliyoisha nilikaa kama siku nne hivi sijala kitu bhana halafu nikiangaza kitu cha thamani nilicho nacho gheto ni jiko na masufuria nkaona hivi havina msaada kama hata msosi kupata ni shida ilikuwa mida ya saa tatu nikachukua kajiko kadogo ka mkaa nikamwaga majivu nikalitia kwenye begi nkaweka kisu masufuria nikayaweka kwenye mfuko nikashuka zangu kwa mam ntilie yule bi mkubwa aliona na shida akaamua kunilalia kabisa nikauza vitu vyangu kwa elfu 10 akanipa na sahani ya wali nkalala nkarudi kulala shida haziishi wazee hapa nawaza nauza nini nilipe kodi kitu cha thamani nilicho nacho ni pc kama ingekuwa yangu ningekuwa nishapiga bei sema nathamini vitu vya kupewa.
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Sijawahi kumbwa na njaa ya kutisha. Hapa ghetto wenzangu huwa wanafuja mali hela zinaisha wanashindia mihogo wakitaka niwakopeshe nawajibu ovyo kama "kwani wakati unazitumia na mademu zako hukujua njaa ni ya kila siku". Unakuta mtu katumia 60k juzi alafu leo hana maisha.

Zamu yangu ikafika simu yangu ikapotea, ninajua namba ya mama tu nikapiga kwa simu nyingine hapatikani siku nzima. Asubuhi sijala mpaka usiku kilichofata nilienda hostel usiku kwa ex wangu aniokoe akanipa 20k nikarudi ghetto na fujo kwa wana walionibania. Hiyo njaa ya siku hiyo naipa tuzo
Ex wako mtu sana. Inaonekana hamkuachana kwa kinyongo. Ninashawishika kukushauri umuweke kwenye mipango yako ya muda mrefu.
 
Back
Top Bottom