Zanzibar 2020 Njama? Mgombea wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya ACT-Wazalendo, Maalim Seif awekewa Pingamizi

Zanzibar 2020 Njama? Mgombea wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya ACT-Wazalendo, Maalim Seif awekewa Pingamizi

Mtoto akiliia wembe mpe!

Wameamua kuleta vurugu Zanzibar na kuua Wazanzibar, Sasa hata tone moja la damu ya Wazanzibar ikimwagika itakuwa mikononi mwao
MUNGU AKATUJALIE UCHAGUZI WA HAKI NA AMANI. awajalie watawala kujua uhai na pumzi kuwa ni mali ya Mungu,na Makeke yote Mungu ndo mwamuzi
 
Hata siamini pingamizi linahusu tarehe ya kiapo. Yaani kwa kuzingatia Maalim Seif anavyowindwa. Na umakini wote waliouweka kwenye kujaza form chini ya mwanasheria wao wamewezaje kutoa mwanya wa pingamizi la kienyeji kama hili! Nahisi huu sio ukweli halisi.
Kiapo chake ametia saini 07/07/2020 ambapo tume ilikuwa bado haijatoa fomu!
 
z
Hii ndio taarifa iliyotolewa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar kwa waandishi wa habari , huku ofisa wa Tume hiyo akionekana kuwa na uso wa bashasha jambo lililoashiria kufurahia pingamizi hilo , ameendelea kusisitiza uhalali wa pingamizi jambo lililoshangaza wengi .

Tuendelee kutega sikio kwa yatakayojiri .
[/QUOTE
Sisi tutapiga Magoti na pia tutasali tutamwambia MUNGU atujalie amani na furahaa. awezi kutupa nyoka
 
Mapingamizi yapo kwa mujibu wa sheria sasa mnalialia nini? Magufuli alipowekewa mapingamizi chadema mlikuja hapa mkishangilia haswa, mlisahau kuwa wembe ni ule ule tulieni mnyolewe
 
Au inawezekana ni tatizo la mwandiko. Kwenye mwezi inawezekana hiyo 'tisa' imecharangwa ikawa na inaumbo linalofanana_fanana na 'saba'. Tisa ya mcharango hivi. Ndio maana msimamizi wa uchaguzi akawa anacheka kwa mzaha!
 
Ukifanya trend reading utagundua kuwa hiyo form ya kiapo amebadilishiwa mara baada ya kuiwasilisha.

ZEC watakuwa wameghushi ili kutafuta kisingizio cha kujaribu kumuengua Maalum kwenye kinyang'anyilo.

Haiwezekani form ya mgombea Urais inayoangaliwa na kujazwa na jopo la wasaidizi ikosewe bila kuona typo obvious kama hiyo.

Ni CCM hao, lakini hawatafika mbali kwa maana ACT watakuwa na nakala ya original iliyowasilishwa ZEC ambayo wataitumia kupinga pingamizi hilo.
 
Hii ndio taarifa iliyotolewa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar kwa waandishi wa habari , huku ofisa wa Tume hiyo akionekana kuwa na uso wa bashasha jambo lililoashiria kufurahia pingamizi hilo , ameendelea kusisitiza uhalali wa pingamizi jambo lililoshangaza wengi .

Tuendelee kutega sikio kwa yatakayojiri .
Pingamizi haliangalii sura ,dini ,chama ,kabila ,rangi au umri,hakuna ajabu hapo ,cha msingi haki itendeke kwa wote
 
Ina maana naye alikosea kujaza fomu au kunani jamani?
Wanasema form badala ya kujazwa na kuonyesha tarehe 9 September 2020, mzee kaweka tarehe 7 July 2020

Kapewa muda na nafasi ya kuwasilisha utetezi wake
 
Sheria inataka kiapo kifanyike siku ya kurejesha na ndio usaini na tarehe .yeye amesaini 07/09/2020 na amewakilisha jana tarehe 09/09/2020.makosa haya makatibu wengi wanayajua sijui hakuwa na msàidizi wa kuielewa fomu.
 
Back
Top Bottom