Nimepata tetesi kuwa kuna timu ya watu wa Yanga waliojipanga kufanya matukio ya kuchafua taswira ya mpira wa Tanzania hususani wakati Simba wanacheza.
Tunaendelea na uchunguzi kwani kwa taarifa kutoka chanzo kinachoaminika, mikakati hii ina lengo la kupunguza kasi ya watoto wanaoikubali Simba utotoni kwa kuwatisha na vitu vya kusadikika.
Baada ya uchunguzi kukamilika, tutaleta ushahidi wa watu walioandaa mipango hiyo michafu dhidi ya Simba.
Kuna baadhi ya waandishi makanjanja walifika mahali wakaja na takwimu kabisa za jinsi ushindi wa Simba ulivyopatikana.Si jambo la kushangaza kwa mtu asiye na elimu akisema ushindi wa Simba ulipatikana nje ya uwanja kwa 60%. Ila ni jambo la ajabu mtu kama huyu kuaminiwa na kituo kama Wasafi FM. Ukiuliza vigezo vya kupata hizo 60% huku tukiona wachezaji wetu kama Luis wakicheza hadi kutaka kuvunjwa shingo, ukweli ni kwamba hawana.
Sasa kama mlileta paka na mkapigwa 4, hebu mechi yenu leteni fisi kabisa safari hii mtakataana.Maana aliyewalea ameshaondoka.Safari hii mtaona moto wa striker wawili