sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Arusha Mjini - wazawa asili Kuna Wameru na Waarusha, niliwahi kuishi hapo miaka mitano, cha ajabu kilichonishangaza ni kwamba Mji huu kwenye mambo ya fursa upo kwa majirani zao Wachaga wa Moshi, niliweza kufanya uchunguzi kwenye mambo kama hotel nyingi sana za Wachaga, Kampuni nyingi za utalii za Wachaga, biashara nyingi hapo mjini za Wachaga mpaka siasa hao kina Lema ni Wachaga.
Mbeya Mjini - wazawa asili wa hili eneo ni kabila la Wasafwa, Kwa bahati mbaya kabila hili machifu walikuwa na itikadi za kuzuia kuchanganyikana na wageni kwa kuamini ni kulinda tamaduni zao, matokeo yake wageni walipoanza kuja Wasafwa wanasogea pembeni, mema ya mji kuanzia Elimu, Biashara, Kazi, Siasa, n.k. wanufaika wakawa ni kabila la wilaya jirani ya Tukutu kwa Wanyakyusa, kwa sasa Wakinga ndio wameshikilia zaidi biashara, Ila kwa siku hizi angalau zile fikra za machifu zimeanza kufutika nao Wasafwa tunajimix nao.