pole sana
nyama njegere:
- mahitaji:-
- nyama
- njegere
- nyanya
- vitunguu
- pilipili hoho
- karoti
- chumvi
- pilipili manga kidogo (sio lazima)
- kitunguu swaumu na tangawizi
- mafuta.
hatua za upishi:
- kataka nyama yako osha kisha changanya kitunguu swaumu na tangawizi na pilipili manga chumvi then weka jikoni (usiweke maji had nyama yako ianza kuchemka)
- osha njegere zako na uzichemshe kidogo tu ( kama dakika 5 hivi maana zinawai kuiva na zitaiva wakati wa kuunga nyama yako)
- katakata nyanya zako vipande vidogo vidogo, kata karoti na hoho zako vipande vidogo vidogo.
- nyama yako ikiiva itoe. bandika sufuri unayoitumia kuungia weka mafuta kiasi yakipata moto kaanga vitunguu vyako vikianza kuwa vya brown weka kitunguu swaumu na tangawizi (kidogo tu ) then weka nyanya zako. vipike kwa moto mdogo had ziive.
- nyanya zikiiva weka nyama yako, karoti na njegere vichanganye vizuri then ongeza kidogo supu ya nyama then acha ichemke kama dakika 3 alaf uweke hoho zako (hoho zina wekwa mwishon ili zisiive sana zikapoteza radha) utaacha vichemke kwa mda kidogo(dakika 2-3 zinatosha)
- unaweza ongeza supu kama utaona haikutoshi.
had hapo mbona yako ipo tayari kwa kuliwa.
WALI:
Mahitaji:
- mchele
- iliki
- chumvi
- kitunguu
- karoti
- mafuta
Jinsi ya kipika:
- osha mchele wako.
- bandika sufuria jikoni weka mafuta na kaanga vitunguu na karoti zako .
- vitunguu vikibadirika rangi kidogo tu weka mchele wako na anza kuukaanga kwa kama nusu dakika weka chumvi then tia maji kiasi cha kuivisha dondoshea na iliki kiasi (punje 3-4 inategemea na wingi wa wali wako) then funika acha wali wako uive.
- ukiiva unaweza zitoa iliki.
NB: sijaweka vipimo maana sijajua idadi ya walaji pia nivumilie mm sio mwandishi mzuri