SoC01 Njia bora ya kuondoa tatizo la ukosefu wa ajira nchini

Stories of Change - 2021 Competition

Desi P

Senior Member
Joined
Jul 31, 2017
Posts
151
Reaction score
80
Tatizo la ukosefu wa ajira ni janga ambalo lipo duniani kote, lakini ukubwa wa tatizo hili hutofautiana baina ya nchi moja na nyingine, mathalani nchi ambazo zimeendelea tatizo la ukosefu wa ajira ni dogo sana ukilinganisha na nchi zinazoendelea kama nchi yetu Tanzania. Kinachosababisha kuwepo kwa utofauti wa ukubwa wa tatizo ni mifumo ya elimu iliyopo katika nchi husika.Hii ina maana kwamba mifumo ya elimu kwa nchi zilizoendelea ni mizuri zaidi kuliko mifumo ya elimu iliyopo kwenye nchi zinazoendelea kama Tanzania

Mfumo wetu wa elimu uliopo huwa unamuandaa kijana kuwa mwajiriwa wa eneo fulani katika jamii badala ya kumuandaa kijana kujiajiri mwenyewe katika jamii yetu ya kitanzania, kwa kuwa serikali na sekta binafsi hazina nafasi nyingi ya kuajiri wahitimu, kundi kubwa la wahitimu hujikuta wapo tu mtaani na hawana kazi yoyote ya kufanya kulingana na taaluma zao walizosisomea.

Ili kutibu tatizo hili kwa uhakika kabisa ni vema tukaanza kwa kutibu kwanza chanzo cha tatizo ambacho ni mfumo wa elimu.Kama taifa tunapaswa kuwa na mfumo wa elimu ambao utajikita zaidi katika vipaji vya watoto (student talent) badala ya mfumo huu wa sasa unaojikita kwenye umahiri wa mtoto (student competent). Mfumo huu ninapendekeza uwe na muundo kama ifuatavyo:-

ELIMU YA MSINGI
Elimu ya msingi iwe ya kuanzia awali mpaka darasa la nane (8). Hii ina maana kwamba mtoto ataanza darasa la awali akiwa na umri wa miaka 4 atasoma kwa miaka miwili (2), akifikisha miaka sita (6) ataanza darasa la kwanza na atakuwa anahitimu elimu ya msingi akiwa na umri wa miaka 13. Mchakato mzima wa elimu ya msingi utakuwa kama ifuatavyo:
Kuanzia awali mpaka darasa la tano (5) walimu watakuwa na jukumu la kumfundisha mtoto elimu ya kujitambua pamoja na masomo mengine machache mfano kama uraia, tehama, lugha, sayansi na hesabu na huku wakiwa na jukumu la kusoma na kutambua kipaji cha mtoto husika.

Kuanzia darasa la sita (6) mpaka darasa la nane (8) mtoto atawekwa kwenye mkondo ambao unaendana na kipaji chake na hapo ataanza kufundishwa masomo ya awali yanayohusiana na kipaji chake, mathalani mwenye kipaji cha muziki ataanza kufundishwa masomo ya awali yanayohusiana na muziki, mwenye kipaji cha kuchora ataanza kufundishwa masomo ya awali ya uchoraji, wenye vipaji vya ufundi mbalimbali nao pia wataanza kufundishwa sawasawa na vipaji vyao masomo ya awali. Kwa ufupi ni kwamba kila mtoto atasoma masomo kulingana na kipaji chake husika.

Ili kulifanikisha hilo serikali italazimika kuajiri wataalamu wa elimu ya saikolojia kuanzia ngazi ya elimu ya msingi ambao wao watakuwa na kujukumu la kuwafundisha watoto elimu ya kujitambua na kujiamini maishani mwao. Serikali pia italazimika kuweka miundombinu ya msingi kwenye shule za msingi sawasawa na vipaji vinavyopatikana hapa nchini. Watoto watapimwa sawasawa na vipaji vyao badala ya upimaji wa jumla unaofanyika sasa.

ELIMU YA SEKONDARI
Elimu ya sekondari itakuwa na ngazi moja tu nayo itakuwa kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha tano (5), Shule za sekondari zitakuwa zinapokea watoto sawasawa na vipaji vyao kwa namna hiyo kutakuwepo na shule za sekondari zinazohusika na vipaji vya ufundi, michezo, kilimo, biashara, lugha, siasa, uongozi, afya na mambo mengine.Tofauti na sasa amabapo watoto huwa wanachanganywa kwa pamoja bila hata kuwatambua vipaji vyao na matokeo yake watoto wengi wanaacha shule kutokana na kwamba wanasoma vitu ambavyo siyo vipaji vyao hivyo wanaona shule nikama sehemu ya mateso. Mfano mtoto ambaye kipaji chake ni muziki yeye hana furaha na "logarithms" kwenye hesabu maana hana faida nazo. Tunakaa darasani kumfundisha 'the earth as a sphere" mtoto ambaye kipaji chake ni upambaji.

Mtoto huyu atakuwa na muda mwingi wa kukaa nje ya darasa kwa ajili ya mazoezi ya kipaji chake awapo shuleni na kutumia muda mchache akiwa darasani kwa ajili ya kusoma nadharia za masomo mengine kama vile uraia, tehama , lugha na masomo yenye uhusiano na kipaji chake. Kutokana na watoto kusoma vitu wavipendavyo mioyoni mwao natumaini hawatakuwepo watoto wanaoacha shule kama hali ilivyo sasa kwenye shule zetu.

Upimaji wa mtoto utakuwa ni endelevu na atapimwa sawasawa na jinsi ambavyo anafanya kwenye mazoezi yake ya kipaji na darasani pia, kwa hiyo hakutakuwepo na mtihani wa mwisho kama ilivyo sasa. Jukumu la kumpima mtoto litabebwa na baraza la mitihani pamoja na jopo litakalokuwa linafuatilia maenndeleo ya mtoto tangu aingie kidato cha kwanza.

Pindi mtoto anapohitimu serikali italazimika kumpa nusu ya vitendea kazi sawasawa na kipaji chake, mathalani kwa wale ambao ni mafundi serikali itawapa vifaa vya ufundi wao ili kiwe kama kianzio pindi watakapo ingia mtaani na wahitimu wengine pia. Kwahiyo sasa badala ya watoto kuwavika mataji kwenye mahafari yao ya kuhitimu watakuwa wanapewa vitendea kazi vya vipaji vyao. Mtoto pia atapewa vyeti viwili kimoja cha kuhitimu elimu ya sekondari kingine cha kuhitimu elimu ya kipaji chake kwa ngazi ya astashahada.

Kwa wale ambao watafanya vizuri sana kwenye miaka yao ya masomo watapata nafasi ya kuendelea na ngazi nyingine ya elimu kama stashahada na shahada. Natumaini hakuna muhitimu ambaye atarundi nyumbani na kukaa tu kwani kila mmoja atakuwa na kitu cha kufanya kwenye jamii sawasawa na kipaji chake na kwa kuwa ni kipaji chake atakifanya hicho kitu kwa ufanisi mkubwa na jamii itanufaika nacho.

ELIMU YA VYUO
Mfumo wa vyuo vya kati itakuwa ni kutoa stashahada tu maana astashahada itakuwa imetolewa kwenye ngazi ya sekondari, vyuo vikuu vitajikita kutoa shahada na ngazi nyingine ya ujuzi. Vyuo vitapokea vijana waliotoka kwenye elimu ya sekondari sawasawa na vipaji vyao, wenye vipaji vya mambo ya kompyuta watasoma mambo ya kompyuta wenye vipaji vya kuelekeza wengine watafundishwa ili wakaelekeze wengine, wenye vipaji vya mambo ya afya wataandaliwa ili wakatibu kwenye jamii. Vijana chuoni watakaa kwa muda wa miaka mitatu (2) kwa vyuo vya kati na miaka mitatu (3) kwa vyuo vikuu.

MASOMO KWENYE MFUMO USIO RASMI
Serikali itajenga vituo vya vipaji kwa ajili ya watoto ambao watakuwa wameukosa mfumo rasmi na pia vyuo vyetu vya VETA vitahusika zaidi kwenye kulibeba jukumu hili la watoto walio nje ya mfumo rasmi wa elimu.

HITIMISHO
Hii itasaidia sana kuondoa tatizo la ajira hapa nchini kwetu na pia matatizo mengine ya elimu hapa nchini yatakuwa yamepungua sana . Mfumo wote wa elimu kuanzia ngazi ya awali mpaka sekondari utagharamiwa na serikali kwa asilimia themanini (80%) na asilimia ishirini (20%) ataghharamia mzazi au mlezi wa mtoto husika.

'Kumbuka kipaji ndicho hutambuliwa na dunia na dunia siku zote huvutwa na kipaji"

Upvote 3
Ndo maana kuna masomo Meengi humo humo!! Mwanafunzi ataona ni kipi kinamfaa au ni kipi hakimfai!! ktk akili ya uelewa!! napinga kuweka wana saikolojia hayo ni matumizi mabaya ya rasilimali!!

Watoto/wazazi ......wanauwezo wa kugundua vipaji vyao wenyewe!! siyo kila kitu ufundishwe! jijue/jitambue/jiongeze/jidadisi/jisimamie ili ufike safari yako kitaaluma!!!...mkiendekeza hili jambo itafika mahali mtasema...

waalimu sasa mtusagie nyama ya kula meno yanauma kwa kutafuna hovyo! halafu tunasahau sahau tuliyo jifunza!!...kitendo cha wewe kwenda shule ni kutaka ujitambue! mapenzi yako na! uwepesi wako ktk utendaji wa somo husika!

siyo kila kitu uige mzungu/ sijui ugunduliwe umekuwa madini weye???.....Unasema ajira???.... Hivi mtu umefundishwa shule ya kilimo Ihungo/Ufundi/Mara sec. school jamani unatasubiri ajira ya nini?? ..hizi shule unaweza ukaanza mwenyewe Aglomechanics mwenyewe nyumbani!!

Bee keeping/ Book keeping unajajili kabisaaa!! nyumbani!!....jamani hayaa Dr hata consultation si unaweka tu!...sasa hilo nalo ufundishwe!! Mwalimu fungua tuition centre mwenyewe!! hata nyumbani hapo weka makuti ivi....ili maradi uwe vizuri kichwani!! watakuja tu!

Mwanasheria jamani zungukia mahakamani saidia watu uone kam huta pata hela watu wameanza haya wakiwa bado shule why not uraiani??....well fundi magari hata ma bus yanayopita kijijini hapo fix them!

Hao waalimu wenu mnawaonea sana akufundishe masomo!! Michezo na bado agundue na vipaji vyenu? nafasi ya mzazi iko wapi hapo? Bar na CD au? unakwepa majukumu??? eneee! kwanza kwa hela ipi hiyo ya sirikali au ...... kenge kabisa nyie.

au ndo kuiga ulaya......wenzenu kule wanashiba....wanahela/thaminiwa hasa....huko kwenu..mwlm anatoa asilimia 20 tuu..zilizo bakia ni za muhusika.....ukitaka hayo unayo sema mzazi uchangie Million 20...kwa miezi sita km ile ya MO kamuulize!

Lkn ukitegemea shule za katani hee!! ee!! utadoda na huko nako katani hamna dogo akili zenu hizo saabu mwalimu akinona kidogo tu mtaanza kulalama ooh!! mwalimu kala binti yangu! hivi hivi kesi tayari! kifupi mnaogopwa!

uzuri ni kuwa kila kitu bongo kipo! ni wewe tu...siyo unataka mwanao asome uzuri wewe unaenda kesha Bar!!...huna hela mpeleke katani huko kwa maskini wenzako msitusumbue au mleta mada unatoka kijijini nini?

shule nzuri zipo km Baba yako hakukupeleka huko!! ni umaskini wake linatuhusu nini sisi!!!...usijaribu kutuyumbisha Mama Samia akakusikiliza buree!!! make huko juu kuna Mawaziri vilaza km wewe!! wanaweza kumshauri Mama huu utoporo!! Tuta yumba.
 
Tatizo la ukosefu wa ajira ni janga ambalo lipo duniani kote, lakini ukubwa wa tatizo hili hutofautiana baina ya nchi moja na nyingine, mathalani nchi ambazo zimeendelea tatizo la ukosefu wa ajira ni dogo sana ukilinganisha na nchi zinazoendelea kama nchi yetu Tanzania. Kinachosababisha kuwepo kwa utofauti wa ukubwa wa tatizo ni mifumo ya elimu iliyopo katika nchi husika.Hii ina maana kwamba mifumo ya elimu kwa nchi zilizoendelea ni mizuri zaidi kuliko mifumo ya elimu iliyopo kwenye nchi zinazoendelea kama Tanzania

Mfumo wetu wa elimu uliopo huwa unamuandaa kijana kuwa mwajiriwa wa eneo fulani katika jamii badala ya kumuandaa kijana kujiajiri mwenyewe katika jamii yetu ya kitanzania, kwa kuwa serikali na sekta binafsi hazina nafasi nyingi ya kuajiri wahitimu, kundi kubwa la wahitimu hujikuta wapo tu mtaani na hawana kazi yoyote ya kufanya kulingana na taaluma zao walizosisomea.

Ili kutibu tatizo hili kwa uhakika kabisa ni vema tukaanza kwa kutibu kwanza chanzo cha tatizo ambacho ni mfumo wa elimu.Kama taifa tunapaswa kuwa na mfumo wa elimu ambao utajikita zaidi katika vipaji vya watoto (student talent) badala ya mfumo huu wa sasa unaojikita kwenye umahiri wa mtoto (student competent). Mfumo huu ninapendekeza uwe na muundo kama ifuatavyo:-

ELIMU YA MSINGI
Elimu ya msingi iwe ya kuanzia awali mpaka darasa la nane (8). Hii ina maana kwamba mtoto ataanza darasa la awali akiwa na umri wa miaka 4 atasoma kwa miaka miwili (2), akifikisha miaka sita (6) ataanza darasa la kwanza na atakuwa anahitimu elimu ya msingi akiwa na umri wa miaka 13. Mchakato mzima wa elimu ya msingi utakuwa kama ifuatavyo:
Kuanzia awali mpaka darasa la tano (5) walimu watakuwa na jukumu la kumfundisha mtoto elimu ya kujitambua pamoja na masomo mengine machache mfano kama uraia, tehama, lugha, sayansi na hesabu na huku wakiwa na jukumu la kusoma na kutambua kipaji cha mtoto husika.

Kuanzia darasa la sita (6) mpaka darasa la nane (8) mtoto atawekwa kwenye mkondo ambao unaendana na kipaji chake na hapo ataanza kufundishwa masomo ya awali yanayohusiana na kipaji chake, mathalani mwenye kipaji cha muziki ataanza kufundishwa masomo ya awali yanayohusiana na muziki, mwenye kipaji cha kuchora ataanza kufundishwa masomo ya awali ya uchoraji, wenye vipaji vya ufundi mbalimbali nao pia wataanza kufundishwa sawasawa na vipaji vyao masomo ya awali. Kwa ufupi ni kwamba kila mtoto atasoma masomo kulingana na kipaji chake husika.

Ili kulifanikisha hilo serikali italazimika kuajiri wataalamu wa elimu ya saikolojia kuanzia ngazi ya elimu ya msingi ambao wao watakuwa na kujukumu la kuwafundisha watoto elimu ya kujitambua na kujiamini maishani mwao. Serikali pia italazimika kuweka miundombinu ya msingi kwenye shule za msingi sawasawa na vipaji vinavyopatikana hapa nchini. Watoto watapimwa sawasawa na vipaji vyao badala ya upimaji wa jumla unaofanyika sasa.

ELIMU YA SEKONDARI
Elimu ya sekondari itakuwa na ngazi moja tu nayo itakuwa kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha tano (5), Shule za sekondari zitakuwa zinapokea watoto sawasawa na vipaji vyao kwa namna hiyo kutakuwepo na shule za sekondari zinazohusika na vipaji vya ufundi, michezo, kilimo, biashara, lugha, siasa, uongozi, afya na mambo mengine.Tofauti na sasa amabapo watoto huwa wanachanganywa kwa pamoja bila hata kuwatambua vipaji vyao na matokeo yake watoto wengi wanaacha shule kutokana na kwamba wanasoma vitu ambavyo siyo vipaji vyao hivyo wanaona shule nikama sehemu ya mateso. Mfano mtoto ambaye kipaji chake ni muziki yeye hana furaha na "logarithms" kwenye hesabu maana hana faida nazo. Tunakaa darasani kumfundisha 'the earth as a sphere" mtoto ambaye kipaji chake ni upambaji.

Mtoto huyu atakuwa na muda mwingi wa kukaa nje ya darasa kwa ajili ya mazoezi ya kipaji chake awapo shuleni na kutumia muda mchache akiwa darasani kwa ajili ya kusoma nadharia za masomo mengine kama vile uraia, tehama , lugha na masomo yenye uhusiano na kipaji chake. Kutokana na watoto kusoma vitu wavipendavyo mioyoni mwao natumaini hawatakuwepo watoto wanaoacha shule kama hali ilivyo sasa kwenye shule zetu.

Upimaji wa mtoto utakuwa ni endelevu na atapimwa sawasawa na jinsi ambavyo anafanya kwenye mazoezi yake ya kipaji na darasani pia, kwa hiyo hakutakuwepo na mtihani wa mwisho kama ilivyo sasa. Jukumu la kumpima mtoto litabebwa na baraza la mitihani pamoja na jopo litakalokuwa linafuatilia maenndeleo ya mtoto tangu aingie kidato cha kwanza.

Pindi mtoto anapohitimu serikali italazimika kumpa nusu ya vitendea kazi sawasawa na kipaji chake, mathalani kwa wale ambao ni mafundi serikali itawapa vifaa vya ufundi wao ili kiwe kama kianzio pindi watakapo ingia mtaani na wahitimu wengine pia. Kwahiyo sasa badala ya watoto kuwavika mataji kwenye mahafari yao ya kuhitimu watakuwa wanapewa vitendea kazi vya vipaji vyao. Mtoto pia atapewa vyeti viwili kimoja cha kuhitimu elimu ya sekondari kingine cha kuhitimu elimu ya kipaji chake kwa ngazi ya astashahada.

Kwa wale ambao watafanya vizuri sana kwenye miaka yao ya masomo watapata nafasi ya kuendelea na ngazi nyingine ya elimu kama stashahada na shahada. Natumaini hakuna muhitimu ambaye atarundi nyumbani na kukaa tu kwani kila mmoja atakuwa na kitu cha kufanya kwenye jamii sawasawa na kipaji chake na kwa kuwa ni kipaji chake atakifanya hicho kitu kwa ufanisi mkubwa na jamii itanufaika nacho.

ELIMU YA VYUO
Mfumo wa vyuo vya kati itakuwa ni kutoa stashahada tu maana astashahada itakuwa imetolewa kwenye ngazi ya sekondari, vyuo vikuu vitajikita kutoa shahada na ngazi nyingine ya ujuzi. Vyuo vitapokea vijana waliotoka kwenye elimu ya sekondari sawasawa na vipaji vyao, wenye vipaji vya mambo ya kompyuta watasoma mambo ya kompyuta wenye vipaji vya kuelekeza wengine watafundishwa ili wakaelekeze wengine, wenye vipaji vya mambo ya afya wataandaliwa ili wakatibu kwenye jamii. Vijana chuoni watakaa kwa muda wa miaka mitatu (2) kwa vyuo vya kati na miaka mitatu (3) kwa vyuo vikuu.

MASOMO KWENYE MFUMO USIO RASMI
Serikali itajenga vituo vya vipaji kwa ajili ya watoto ambao watakuwa wameukosa mfumo rasmi na pia vyuo vyetu vya VETA vitahusika zaidi kwenye kulibeba jukumu hili la watoto walio nje ya mfumo rasmi wa elimu.

HITIMISHO
Hii itasaidia sana kuondoa tatizo la ajira hapa nchini kwetu na pia matatizo mengine ya elimu hapa nchini yatakuwa yamepungua sana . Mfumo wote wa elimu kuanzia ngazi ya awali mpaka sekondari utagharamiwa na serikali kwa asilimia themanini (80%) na asilimia ishirini (20%) ataghharamia mzazi au mlezi wa mtoto husika.

'Kumbuka kipaji ndicho hutambuliwa na dunia na dunia siku zote huvutwa na kipaji"

Well said
 
Back
Top Bottom