KOROSHO BOMBA
Senior Member
- May 11, 2024
- 186
- 313
"The best way to win is to weaken your opponent(s)". Hii ndio mbinu wanayotumia mataifa makubwa kama Urusi kupambana na maadui zao wakubwa kama Marekani kwa kuwapora majajusi wao Bora.
Mbinu hii pia ilikua inatumiwa na viongozi wa Simba SC kipindi kile Cha Hans Pope na Manara kwa kupora wachezaji Bora wa Yanga na Azam kama Niyonzima, Morisson, Boko, Manura, Kapombe, Nyoni na wengineo. Basi tangu Hans Pope afariki na Manara kupeleka mbinu hii upande wa pili Yanga wanapora tu wanavyotaka kwa kuchukua wachezaji Bora wa Simba na kuwadhoofisha wakati huo Simba wamelala pasipo kupora akina Pacome na Max. Hii mbinu imeisaidia Yanga kuwa dominant kwa Simba.
Nilikua sielewi kwanini mashabiki wa Simba wanaulalamikia uongozi, sasa naanza kuelewa taratibu. Hivi unaachaje kuchukua Aucho tulieshuhudia ubora wake kwa miaka minne unaenda kuchukua garasa Kante asiejiamini hata ku dribble hawezi? Kusajili mchezaji usiemjua ni sawa na kubeti.
Viongozi wa Simba hacheni kulala, kuchukua wachezaji wa Yanga haimaanishi kwamba mmefeli kwenye scouting Bali ni njia sahihi ya kumdhoofisha wakati ukiendelea kujiimarisha. Nendeni Yanga pora wachezaji Bora wanaokaribia kumaliza mikataba waraghai kwa mikataba minono, chukua backbone ya timu kama lipacome lile, Max, Mudathir, Baka, Job, Diarra. Jifunzeni kwa Eng. Hersi hachukui magarasa yenu mnayotupa kama akina Okejepha na Mavambo, yeye anachukua clean products Ile mihimili ya timu kama Zimbwe, Chama, Mkude, etc.
Msipofanya hivyo mtaendelea kuwa vibonde kila siku hata Ile Raha ya derby haitakuwepo tena. Tumemiss zile sarakasi za miaka Ile za kunyang'anyana akina Morisson na Mbuyu Twite yan ilikua piga nikupige lakini sasa hivi imekua upande Mmoja Engineer amewazidi kila kitu.