petercharlz255
Member
- Aug 25, 2022
- 9
- 14
Kupitia jukwaa hili nataka kuwafikishia elimu hii watumiaji wa jukwaa hili la jamii kuhusu NJIA MBILI ZA KIFIKRA KATIKA JAMBO MOJA NA MAAMUZI CHANYA. Kwa ufafanuzi zaidi ili kuleta maana harisi niliyotazamia katika jambo nalotaka kuzungumzia tuchukulie jambo hilo labda ni kosa katika sehemu yoyote ile labda katika ndoa,siasa,dini n.k, mfano tuchukulie kosa katika ndoa.
Mfano: Bwana Jamii aliporudi nyumbani kwake baada ya miaka 2 akiwa mbali kikazi aligundua mke wake anamsaliti na alipofatilia kwa kina mke wake alikubali, ndipo akachukua maamuzi ya kumpa talaka kwasababu mke wake alikosa adabu na uaminifu katika ndoa yao. Bwana Jamii alifikiria kuhusu gharama ya harusi waliyofunya,kiasi cha pesa alichomwachia,haja alizomtimizia,aibu katika jamii n.k. hivyo akamua kumuacha mke wake.
Katika jambo hilohilo tuliangalie katika upande wa pili (2) wa kifikra. Bwana Jamii alipogundua mke wake anamsaliti licha ya mke wake kukubali lakini alimsamehe. Kwanini.!? Bwana Jamii alifikiria kuhusu umbali uliokuwepo kati yake na mke wake kwa miaka miwili ndio ulipelekea mke wake kumsaliti, alifikiria kuwa kama ambavyo yeye alikua akingia majaribuni na wanawake wengine mke wake pia alikua katika majaribu ya wanaume wengine kipindi cha miaka yote hiyo miwili wakiwa mbali mbali. Jibu la mwisho alilopata Bwana Jamii ni kumsamehe mke wake.
Sasa nataka ujiulize mwenyewe kwanini baadhi ya watu wanaweza kusamehe katika jambo fulani na watu wengine wasisamehe katika jambo hilohilo? Ukweli ni kwamba watu hao wanatofautiana kutokana na fikra mbili tofauti katika jambo moja ambapo mtu moja atachukua fikra chanya na mwingine atachukulia fikra hasi.
FIKRA CHANYA.
Ni fikra ambazo mtu anafikiria upande ambao hautamuumiza mtuhumiwa baada ya kutoa maamuzi licha ya mtuhumiwa kuwa na hatia au asiwe nayo.Maamuzi yanayopatikana hapa mara nyingi huitwa maamuzi ya busara.
FIKRA HASI.
Ni fikra ambazo mtu anafikiria upande ambao unatoa hukumu kwa mtuhumiwa baada ya shuhuda kuwa mtuhumiwa anahatia au awsiwe nayo ilhali ushahidi upo basi anawajibika.
Ili kufanya maamuzi sahihi kati ya fikra chanya au fikra hasi inatakiwa kichwa chako kiwe mahakama. Kama ambavyo mahakama inatoa nafasi kwa pande zote mbili, pande ya anaeshitaki na pande ya anaeshitakiwa ili ipate majibu yaliyosahihi. Pia kichwani kwako unatakiwa uwe na izo pande mbili kabla ya kufanya maamuzi, upande mmoja ushitaki katika jambo lako kisha baada ya kushitaki upande mwingine utetee katika jambo hilohilo. Baada ya kusikiliza pande zote katika kichwa chako fanya maamuzi yaliyo sahihi na ya haki kulingana na majibu uliyoyapata katika njia hizo mbili za kifikra.
NJIA ZA KIFIKRA KATIKA TUKIO LA KWELI
Sasa tutumie hizo njia mbili za kifikra katika kupata majibu sahihi katika tukio la kushambuliwa kwa risasi kiongozi mashuhuri wa upinzani nchini Tanzania, wa chama cha CHADEMA Mh Tundu Lissu siku ya tarehe 7 Septemba 2017.
Tukio hili lilibua hisia kubwa kwa wananchi hasa kwa upande wa chama cha upinza. Mpaka leo ni miongoni mwa matukio makubwa kuwaikutokea katika siasa za Tanzania ukiachana na utata wa kifo cha aliekuwa raisi wa Tanzania Dk John Pombe Mgufuli. Watu wengi mashuhuri na wachambuzi wa mambo ya kisiasa walilaumu serikali iliyokuwa madarakani kuwa ndio wahusika wa jaribio hilo la kumuua kiongozi huyo huku hata muhanga mwenyewe Mh Tundu Lissu aliinyoshea kidole serikali iliyokuwa madarakani.
Ili kulipatia majibu inatakiwa busara,akili na hekima ya kutosha. Nitawezaje kuvipata hivyo vyote busara,akili na hekima!? Tujaribu kutumia Njia mbili za kifikra na maamuzi sahihi.
NJIA YA KWANZA YA KIFIKRA KUHUSU TUKIO HILO
Watu wenge ukiwauliza kuhusu nani muhusika katika tukio hili jibu la haraka ni serikali iliyokuwa madarakani. Kwanini!? Kwasababu ndio mshitakiwa wa kwanza anaezaniwa kuhusika na hata ripoti ya vyombo vikubwa vya habari kama BBC na DW katika ripoti zao walihusisha tukio hilo na mvutano wa kisiasa uliokuwepo kati ya raisi aliekuwa madarakani na Mh Tundu Lissu. Hii ilijenga picha kwa wananchi wa Tanzania kuwa serikali ndio ilihusika kwasababu ya uaminifu mkubwa uliojengwa na vyombo hivyo kwa jamii, lakini pia serikali haikujiusiha sana kulizungumzia hili. Hali hii ilipelekea wanaharakati kulipigia kelele jambo hilo.
NJIA YA PILI YA KIFIKRA KUHUSU TUKIO HILO
Sasa tuangalie katika njia ya pili ya kifikra katika jambo hili. Kama nilivyo andika awali njia moja itatetea badala ya kuhukumu ili tupate jibu lililo sahihi.
1: Kwanza kabisa tunatakiwa tujiulize kulikuwa na haja ya serikali iliyokuwa madarakani kumshambulia kiongozi huyo ikiwa serikali iliyokuwepo madarakani ilikuwa na nguvu kubwa na pendwa kwa wananchi wengi kuliko waliyo ichukia. Unaweza kupata jibu haikuhitajika njia hii kwasababu raisi alikuwa na ushawishi mkubwa na nguvu kubwa kuliko mh Tundu Lissu kwa wananchi.
2: Kama kweli serikali ilituma mtu kumua Mh Tundu Lissu. Ingemtuma mwanajeshi mashuhuli ambae asingetumia risasi 38 na badala yake risasi moja tu ya kichwa lakini kinachoacha maswali muuwaji alilenga sehemu zisizokuwa na madhara (miguu). Licha ya kuwa na uwezekano wa risasi 1 tu ya kichwa au risasi chache maeneo hatari.
3: Muhanga Mh Tundu Lissu alipata majeraha mguu tofauti na upande ambao gari imeshambuliwa. Mguu ulioumia ni wa kulia ambao ukikaa kwenye siti ya abilia unakuwa upande wa dereva na mguu wa kushoto unakua upande wa mlango ambapo ndio palishambuliwa. Maana yake ni mtu alieshambulia alikua ni upande wa dereva lakini swali linabaki mbona dereva akujeruhiwa!?
4: Inawezekana upande wa gari ulioshambuliwa waliupiga risasi 38 wakiwa wamemtoa mheshimiwa ili watengeneze ushahidi wa shambulizi kuwa na mashiko.
Lakini swali linabaki kwanini sasa washambuliane wao kwa wao. Pengine ilikuwa ni mpango ili kumchafua Rais aliYekuwa madarakani ili iwape nguvu kwenye uchaguzi ujao na ndio maana jambo hilo katika kampeni za Mh Tundu lissu alilitumia kama sehemu ya sera zake.
Baada ya kutumia njia hizi mbili za kifikra inatakiwa tufanye maamuzi yaliyo sahihi. Upande wa kwanza wa kifikra unatuambia serikali iliyokuwa madarakani ndio ilihusika na shambuli hilo na upande wa pili wa kifikra unatuambia ni mpango uliosukwa na wapinzani wenyewe.
Nimetumia tukio hilo la kushambuliwa kiongozi wa upinzani kama sehemu ya kuupa nguvu mtizamo wangu wa NJIA MBILI ZA KIFIKRA NA MAAMUZI SAHIHI ili kuisaidia jamii katika kufanya maamuzi kwenye kila jambo ambalo mwanajamii anakutananalo kwenye maisha yake ya kila siku hasa maamuzi makubwa ambayo yanaweza kuwa athari kwa watu wengine. Katika jukwaa hili la story of change nataka kuleta mabadiliko chanya katika maswala ya kielimu. Asante kwa kusoma na kwaheri.

Upvote
5