Emc2
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 16,808
- 16,887
Nawasalimia wana JF wote. Huu nimwendelezo wa kujifunza Science ya kiroho na namna ya kujitambua.
Leo nitaongelea jinsi gani ilivyo vigumu kujitambua na kujua wewe asili yako ni nini. Jambo gumu kuliko mambo yote ni namna ya kujitambua. Inahitaji bidii na nia ya dhati ndipo utakapoanza kusonga mbele na kujua wewe umetoka wapi.
Nitaanza kueleza kwa ushuhuda wangu binafsi. Kwamba nilikuwa na nia sana ya kutambua hivi sisi binadamu ni kitu gani? Asili yetu ni nini? na tumetoka wapi? Na lengo letu hapa duniani ni nini?
Nilikuwa na maswali mengi sana pasipo na majibu. Nimekuwa sasa nikijifunza na kutafuta ukweli pasipokuwa na akili iliyofungwa. Nilianza kupata masomo ya kujitambua kupitia meditation. Kwa kweli inahitaji bidii ya hali ya juu ili kuweza kusonga mbele.
Siku moja nilikuwa nimejilaza kwenye kitanda (Baada ya kuanza kujifunza Out of Body Experience). Ghafla nikawa naisi mwili wangu unakufa ganzi (Nilikuwa na hofu sana, lakini nikajipa moyo ngoja nione kitu gani kitatokea). Baada ya muda, wakati nimetulia nikaanza kuhisi nwili wangu kama unabebwa. Nikawa na uwezo wa kupaa, nilitoka nje na kuangalia huku na huku. Mara nikarudi ndani. Nilipo rudi nikakuta kunamtu anafanana na mimi kajilaza kitandani. Ha niakaanza kuuliza wewe nani? Mtu huyo alikuwa kimya tu. Kwa kukata stori hiyo baada ya muda nikarudi katika hali ya kawaida. Nilikuwa nimelala hapo hapo.
Baada ya kupata somo kuwa huo mwili ilikuwa ni mwili wangu na mimi nilikuwa katika ulimwengu wa kiroho. Nilifurahi sana kuona kwamba ninaweza kufanya jambo hilo.
Siku nyingine tena nikiwa najifunza. Nilikuwa nimelala na gafla usingizi ukawa umepotea. Nikasema ngoja nifanye OBE. Nikawa nimejilaza kitandani mda kama dakika 40. Nikaanza kuhizi mwili wangu unakufa gazi. Kuanzia kwenye miguu hadi kwenye kichwa. Nilikaa katika hali hiyo kama baada ya saa moja hivi. Baadaye nikaamua nibadilishe namna ya kulala. Nili lala kifudi fudi(Yaani tumbo chini ya kitanda). Nilitulia tena baada ya muda mwili ukaanza kufa ganzi. Nikaendelea kujituliza. Baadaye nikahisi mwili wangu unatetemeka. Nikaangalia pembeni nikajiona. Kisha nikaamua kwenda ninakotaka. Hakika niliondoka nilikuwa na uwezo wa hali ya juu. Kila ninakotaka kwenda niliweza. Nilikutana na viumbe tofauti tofauti na watu wa aina tofauti.
Ninapenda kueleza kwamba jambo hili si rahisi linahitaji uthubutu na kuondoa woga maana unawasiliana na nafsi yako mwenyewe. Watu wengine wanataka kufanya siku moja na kuona matokeo. Inahitaji bidii. Ukishaanza kuendelea utaanza kugundua vitu vingi sana. Utajitambua kuwa wewe ni nani hasa. Utaelewa na utakuwa huru. Utumwa wa fikra utaanza kupotea na utaanza kuwa na maamuzi sahihi.
Ni wachachetu wala si wengi watakao elewa na kufuatilia ninachoongelea. Kukata tamaa na uvivu, umewakumba watu walio wengi. Lakini wale wenye kuthubutu hakika wataelewa. Ni faida ya mtu binafsi si kwaajili ya kikundi au ukoo. Ni jitihada ya mtu mwenyewe. Kuangaziwa nuru na kuondoka kwenye ufungwa ni hatua muhimu sana kwa kipindi hiki.
Chukua hatua ya kuanza kujitambua. Ukiwa na nia na matamanio, mwalimu atakuja kukutafuta na hakika utajifunza. Mwalimu yupo kila wakati anahitaji mwanafunzi.
By Annael.
The Spirit Science Teaching And Self Reality.