Njia nne unazoweza kuzitumia kutoa crypto zako kwenye app ya Binance

Njia nne unazoweza kuzitumia kutoa crypto zako kwenye app ya Binance

FestoKaguo

Senior Member
Joined
Apr 1, 2022
Posts
128
Reaction score
202
Kama umekuwa ni mtumiaji wa hizi cryptocurrency exchanges kama OKX, BYBIT au Binance kwenye kufanya transaction za cryptocurrency basi utakuwa umegundua kuwa P2P au Peer to peer trade ( Biashara baina ya mtu na mtu) kuna namna fulani imekuwa sio safe sana kuitumia kama mwanzo hasa kama unaifanya kupitia exchange ya Binance.

Huu uzi haukushauri wala kukuzuia kuendelea kutumia P2P trade kwenye kufanya transactions zako za Fiat na cryptocurrency lakini unakuongezea kitu cha ziada tu kinachoitwa Binance Pay ambacho kinaonekana kuwa na faida zaidi kwa mtumiaji wa Binance kwa sababu zifuatazo;
20250326_193412.jpg
Kabla ya kuanza na chochote huu uzi utawahusu watu wenyeuhitajiau wanaotumia Binance tayari kwahiyo kama hauna account ya Binance basi unaweza kujisajiri kupitia Crypto Exchange Referral Program | Binance Official na kisha umalize process zote za verification zilizowekwa na Binance kama vile KYC verification pamoja na kudeposit your first crypto.

Sasa ukiwa tayari na na app ya binance kwenye simu yako na ukawa umeshakamilisha tayari taratibu zote za kujisajili na kisha ukawa umepokea malipo yako au umetumiwa crypto zako kwa njia ya USDT au coin yoyote ile kwa mara ya kwanza kutoka kwa mtu yeyote yule kuja kwenye binance yako basi unaweza kutumia njia kuu nne kuzitoa hizo crypto kutoka kwenye app yako ya binance ili uweze kupata Fiat currencies au pesa za kawaida za kitanzania.

Kama unavyoona kwenye picha hapo chini njia hizo unazoweza kuzitumia ni kama vile kutuma crypto kwa kupitia wallet address ( means hapa unamtafuta mtu anayehitaji crypto anakupa address yake kisha unamtumia crypto yeye anakupa hela za kitanzania)

Pia kwenye binance kuna option ya kuuza na kununua crypto kwa kutumia mawakala ( najua sote tunajua uwepo wa mawakala wa M-pesa na tigo pesa tulio nao mtaani hivyo hata Binance pia unaweza kuitumia kwa kuuza crypto zako kupitia P2P ( Peer to peer trade), njia ya tatu unaweza kuziuza kwa kutoa directly kuja mitandao ya simu kama Halopesa, M pesa, Tigo pesa au airtel money na njia ya nne ni kupitia BINANCE PAY.
20250326_212251.jpg

Sasa katika hizo njia nne tuangalie moja moja kwa ufupi sana na kisha tuangalie ipi inaweza kuwa best zaidi na kwanini...
Tukianza na njia ya kwanza ambayo yenyewe ni ya kutumia wallet address ( Hii njia ni safe ila ina risk kubwa kinoma endapo ukikosea address au network)
Screenshot_20250326_212746_Telegram.jpg

Mfano hapo mteja alikuwa anahitaji address ya kunitumia pesa na network nitakayoitumia hivyo kama hauna uelewa unaweza kujikuta unakosea na pesa zinapotea bure na huyo mtu unauetarajia akupe Tzs anakuona kama tapeli.

Tukija njia ya pili ambayo unaweza kuitumia kutoa crypto zako ili upate Tzs ni hii ya Peer to peer trade ambayo mara nyingi inapatikana kwenye hizi exchange kama Binance, OKX, Bitget n.k ambapo huko kuna hawa mawakala wa crypto wanaojihusisha na kuuza na kununua crypto pia. Hivyo ukihitaji kuuza au kununua unaweza kutumia njia hii kwa sababu ni ya haraka
20250326_213016.jpg

Hii ni app ya binance na hiyo ni list fupi ya mawakala wanaonunua crypto kwa mtu anayehitaji kuwauzia.
Hii njia ni nzuri kutokana na rate za kuuza zinakuwa juu kidogo wakati wa kuuza lakini ina risk pia ya kuibiwa.

Nilikuwa nimesema kuna njia nne, sasa hivi tunaingia njia namba tatu ambayo ni kununua na kutoa crypto moja kwa moja kuja kwenye mitandao yetu ya simu kama M-Pesa, Mix by Yass n.k
Njia hii ni nzuri kwa sababu ni safe sana na ni ngumu kutapeliwa kwani inakuwa ni kama vile unavyotoa pesa ATM ya bank tu au Sim Banking n.k ila shida yake ni rate au gharama za kununua ni kubwa ukifananisha na gharama za kuuza
20250326_214945.jpg

Na kiwango cha chini cha kununua unapangiwa kiwe ni kiwango gani tofauti na ukitumia Address au P2P

Njia ya mwisho ambayo nitaieleza leo na ndio njia ambayo naona nzuri ni hii ya kutumia Binance Pay ( yaani unaweza kutuma crypto kwa ndugu au rafiki yako anayetumia binance kwa kutumia email yake, namba ya simu au Binance ID yake na akazipokea pasipo kukatwa hata shilingi)
20250326_215246.jpg

Hii njia ni nzuri na inafanana na ile ya kutumia address lakini tofauti yao ni kwamba hii itahitaji watumiaji wote muwe mnatumia Binance ila ile ya Address unaweza kutuma kwa mtu hata asiyetumia Binance.

Kwa leo nitaishia hapa kesho nitamalizia huu uzi kipengele cha Binance pay kwa undani zaidi vitu vinavyopatikana pale na faida zake.
Kama umependa uzi na unahitaji maelezo zaidi unaweza kunicheki kwa namba 0765772976 kwa maelekezo zaidi ya cryptocurrency
Uwe na usiku mwema msomaji wangu
🙏
 
Hivi hizi kampuni za mablocker haziwezi iba
 
Zinaweza Kuiba, ndiyo maana unatakiwa kufanya utafiti wa blocker anayeaminika kabla ya kuweka Pesa zako.
hapa labda tukutane bank uko na simu tukubaliane unanunua btu zangu shngap nahesabu cash yangu nakutumia kwenye wallet yako unacheki hapohapo bank salio lako la bitcon tukiwa wote tena tunahamisha kwa kuscan barcode sio kukutumia link.kila mtu anaondoka na chake.

Labda kama ni transaction ndogo chini ya laki 5
 
Back
Top Bottom