Njia nzuri kutatua mgogoro DRC

Njia nzuri kutatua mgogoro DRC

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Ili kumaliza mgogoro DRC jumuiya ya kimataifa LAZIMA ifanye yafuatayo:
1. DRC iwatambue na kuwakubali raia wake wenye asili ya makabila ya nchi nyingine. Kama vile Tanzania ilivyoyatambua makabila ya wamasai, wasegeju, wajaluo, wapare, wahaya, wamakonde, wamanyema.
2. Rwanda na Uganda izungumze na raia wake waliokimbilia DRC kuomba hifadhi wakizikimbia serikali zao za Rwanda na Uganda. Wakimbizi wao warudi nyumbani kwao.
3. Rwanda na Uganda ziache kupora rasilimali za DRC.
4. DRC isaidiwe kuimarisha jeshi lake ili imudu kulinda mipaka yake kikamilifu kama zilivyo nchi nyingine jirani yake.
5. Rwanda na Uganda ziondoe majeshi yao kwenye nchi ya Congo kwa gharama yoyote Ile hata ikibidi kwa mturu wa bunduki. na
6. Majeshi ya sadc yawekwe kwenye mipaka kati ya Rwanda na DRC na DRC na Uganda (buffer zone) kwa muda wakati wakijenga uwezo wa DRC kuweza kulinda mipaka yake na nchi hizo kikamilifu
 
Back
Top Bottom