Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Baada ya kumsikia Rais Samia akitangaza kuwa Jiji la Dar es Salaam ni chafu sana, tukaona Mkuu wa Mkoa Albert Chalamila akitangaza kuanza kuchukua hatua, ikiwemo kila nyumba kuwa na dustbin.
Mkuu wa Mkoa, nakuomba uzingatie pia suala la ukusanyaji wa taka katika maeneo ya Mtaa wa Njia Panda, Tegeta A. Baadhi ya maeneo hatujawahi kuliona gari la taka kwa takribani miezi mitatu sasa.
Sasa taka zinaendelea kutupwa hovyo kwa sababu hakuna huduma ya uhakika ya kuzikusanya. Ni vizuri kuweka mazingira mazuri na kuhamasisha kila nyumba kuwa na dustbin, lakini taka zinapojaa, gari la taka linapaswa kupita kwa wakati, kuzikusanya na kuzitupa katika eneo lililotengwa.
Soma Pia: RC Chalamila: Kila nyumba Dar iwe na 'dustbin' za kuwekea taka angalau mbili
Tafadhali, kabla ya kuwaagiza wananchi wanunue dustbin, hakikisheni pia huduma ya ukusanyaji taka inapatikana kwa uhakika katika mitaa yote. Hili litasaidia kuweka Jiji la Dar es Salaam katika hali ya usafi tunayohitaji.