Njia rahisi ya kutotolesha vifaranga vingi bila kutumia mashine (incubators)

Njia rahisi ya kutotolesha vifaranga vingi bila kutumia mashine (incubators)

Kwa wale wafugaji wa kuku wa kienyeji na wasio na uwezo wa kupata artificial incubators, fuata njia hii kutotolesha vifaranga vingi katika kipindi kifupi.
  1. Uwe na majike kadhaa wanaotaga (mfano 40)
  2. kusanya mayai yatakayotagwa ndani ya wiki 2 (yatunze vizuri yasiharibike)
  3. Kawaida kuku wa kienyeji hutaga mayai 12-14 kabla ya kupumzika kutaga (kutaka kuatamia)
  4. Kuku atakaenyesha dalili za kutaka kuatamia katika kundi,mwekee yai moja aatamie
  5. Endelea vivyohivyo kwa kuku watakaoonyesha kuatamia hadi watakapofikia idadi kuku 10
  6. Andaa chumba kizuri chenye mwanga,kisafi na nafasi ya kutosha kukaa kuku 10 bila kubanana
  7. Katika chuma hicho,weka viota (nests) 10- unaweza kutumia boksi ndogo,tia mchanga laini,na tandaza majani laini au pamba juu ya mchanga.
  8. Chukua mayai,yapange ndani ya viota hivyo (mayai 12 kila kiota)
  9. Chukua kuku wale 10,wapange katika viota hivyo. Yai moja kila kuku waliokuwa nayo,yatupe.
  10. Kwenye chumba hicho,weka vyombo vya maji na maji,vyombo vya chakula (chenye mchangayiko mzuri),pia usisahau kuweka dawa ya kuzuia wadudu (viroboto,utitiri nk)
  11. Baada ya siku 21, mayai yataanguliwa (90%-98%). Wanyanganye kuku vifaranga vyote,na vihamishie kwenye artificial brooder (sehemu ya joto ya kukuzia vifaranga). Wakati unaondoa vifaranga,rudishia mayai mengine kwa idadi ile ile na kuku walewale.
  12. Nashauri ufanye mizunguko ya aina hiyo 3,ndo uwapumzishe kuku au kubadilisha wengine.
  13. Kwa hesabu rahisi, kuku 10 @ vifaranga 12 = vifaranga 120 (siku 21), na ukirudia ni vifaranga 240 (siku 42) sawa na vifaranga 362 (siku 63=miezi 2). Hii ina maana kama utatumia kuku 20 kuatamisha, utakuwa na vifaranga 724 ndani ya miezi 2.
  14. Kama vifaranga hivi vitatunzwa vizuri (mada itakuja wiki ijayo) baada ya miezi 2 ya kukua, kwa bei ya soko ni Tsh 3,000/= kwa kifaranga kimoja x 724 (endapo hakuna vifo) = 2,172,000/=
  15. Kwa kuku wa kienyeji ambao kwa sehemu kubwa hawahitaji gharama kubwa ya chakula na madawa 25-30% ni gharama za madawa na chakula cha ziada.
  16. Ukifanya tahmini utagundua kuna faida kubwa. Karibuni tupunguze au kuondoa kabisa umasikini wa kipato
Barikiwa
 
Sijaelewa kitu hapo.. Ina maana KUKU baada ya siku 21 anaendelea kuatamia mayai mengine bila kuchoka??? Duh mm nilijuwa akimaliza kutotoa nimpaka atage tena na ndy atamie tena .Hebu nielimishe hapo
Isitoshe kuku anakawaida ya kususa. Maneno na matendo si sawa. Kwa maneno, ghorofa litajengwa bali kwa matendo kazi kweli kweli.
 
Back
Top Bottom