Njia ya kudhibiti kunguru wananirudisha nyuma

Njia ya kudhibiti kunguru wananirudisha nyuma

Mndengereko One

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2015
Posts
340
Reaction score
243
Mm nimfugaji wa kuku na Bata ila napata changamoto ya kunguru kula vifaranga na mayai bandani wakimuona kuku katoka kutaga wao wanaingia yani ni mwendo wa kuviziana tu niwahi mm Yai au kunguru nimejaribu kuwa winda na manati nimefeli nimeweka sumu kwenye mayai niliyoyatoboa lakini bado wanadunda nilitumia sumu ya panya ya unga kwahyo naomba anaejua mbinu ya kutatua changamoto hii maana ni ndege mwenye akili sana nahitaji mwenye kujua mtego ,sumu au njia ya kuwaamisha
 
Tengeneza banda lenye wavu, hakikisha mifugo yako inakuwa ndani ya wavu hapo utafanikiwa mkuu
 
Kuku ni wa kienyeji
Mimi pia nafunga Kuku wa Kienyeji na Bata.
Ninachofanya nimezungushia Wavu toka Bandani, Kwa ukubwa kama wa Mita 3 × 3...!
Vifaranga vikitotolewa vitakaa Bandani ama kutoka nje ya Banda lakini kwenye Nyavu, so hawatoki nje Kabisa, walikua Kwa Bata baada ya mwezi 1 Kwa Kuku baada ya Miezi 2 ama 3, wanakua wameshakua kiasi Cha Kunguru kushindwa kuwabeba Tena, then nakua naruhusu wakatoka nje ya Nyavu kutafuta chakula Chao.
 
Nyavu ipi uliyozungushia
 
Pole sana Mkuu,nilikuwa na tatizo kama hili ila Mimi changamoto ilikuwa ni kenge ,walikuwa Kila siku tunafukuzana nao,almost kenge 20 walikuwa eneo moja,nimewateketeza wote Sasa Niko huru.

Kama hao kunguru wanakula mayai basi kuwamaliza ni rahisi,je wakichukua yai wanatobolea mdomoni au wanalitoboa likiwa chini na kuanza kula kiiini?

Kama wanatobolea mdomoni na kumeza kiini basi tafuta mayai ya kuku wa kisasa ,sumu ya kuu wadudu Ile ya maji ( kimiminika) , super glue, unga wa ngano/ mhogo , sindano ya nguo ya mkono na Bomba la sindano ya kuchomea binadamu.

Hatua :-tikisa yai taratibu Hadi kiini kiwe maji na Kisha toboa katundu kadogo taratibu na umwage Yale maji ya yai,Kisha mwaga Hadi maji ya yai yaishe na utie ndani sumu Kwa kutumia mbomba la sindano na baada ya hapo ziba Kwa super glue na unga wa ngano weka mayai hayo sehemu afikapo huyo ndege.

Kaa Kwa kusubiri matokeo
 
Funga kamba kuzunguka banda lako hasa mbele wanapopitia alafu ning'iniza manati hata 3. Zikiwa zinacheza cheza na upepo kunguru hasogei.
Pia ua kunguru hata mmoja tu au wawili alafu waning'inize kwenye nguzo ndefu hapo bandani, Wewe kaa tafuna korosho sebuleni.
🤣🤣🤣🤣
 
Mm nimfugaji wa kuku na Bata ila napata changamoto ya kunguru kula vifaranga na mayai bandani wakimuona kuku katoka kutaga wao wanaingia yani ni mwendo wa kuviziana tu niwahi mm Yai au kunguru nimejaribu kuwa winda na manati nimefeli nimeweka sumu kwenye mayai niliyoyatoboa lakini bado wanadunda nilitumia sumu ya panya ya unga kwahyo naomba anaejua mbinu ya kutatua changamoto hii maana ni ndege mwenye akili sana nahitaji mwenye kujua mtego ,sumu au njia ya kuwaamisha
:
Pole sana kwa changamoto unayokutana nayo na kunguru. Hapa kuna baadhi ya mbinu ambazo zinaweza kusaidia kuwalinda vifaranga na mayai yako dhidi ya kunguru:

1. Kufunika Banda: Tumia wavu wa chuma au neti kufunika banda la kuku ili kunguru wasiweze kuingia

2. Kukusanya Mayai Mara kwa Mara: Hakikisha unakusanya mayai mara kwa mara ili kupunguza nafasi ya kunguru kuyapata

3. Kutumia Vitu Vinavyong’aa: Vitu kama CD za zamani au vipande vya kioo vinaweza kutundikwa karibu na banda la kuku. Hii itasaidia kuwatisha kunguru kutokana na mwanga unaoreflect1.
Kutumia Vifaa vya Kutoa Sauti: Vifaa vinavyotoa sauti kubwa au kelele vinaweza kusaidia kuwatisha kunguru

4. Kupanda Mimea Minene: Mimea minene inaweza kusaidia kuficha vifaranga na mayai kutoka kwa macho ya kunguru.

5. Kuweka Mitego: Unaweza kutumia mitego maalum ya kunguru, lakini hakikisha unafuata sheria na taratibu za eneo lako kuhusu matumizi ya mitego1.
 
Back
Top Bottom