Mndengereko One
JF-Expert Member
- Apr 26, 2015
- 340
- 243
Tengeneza banda lenye wavu, hakikisha mifugo yako inakuwa ndani ya wavu hapo utafanikiwa mkuuMm nimfugaji wa kuku na Bata ila napata changamoto ya kunguru kula vifaranga na mayai bandani wakimuona kuku katoka kutaga wao wanaingia yani ni mwendo wa kuviziana tu niwahi mm Yai au kunguru nimejaribu kuwa winda na manati nimefeli nimeweka sumu kwenye mayai niliyoyatoboa lakini bado wanadunda nilitumia sumu ya panya ya unga kwahyo naomba anaejua mbinu ya kutatua changamoto hii maana ni ndege mwenye akili sana nahitaji mwenye kujua mtego ,sumu au njia ya kuwaamisha
Kuku ni wa kienyejiTengeneza banda lenye wavu, hakikisha mifugo yako inakuwa ndani ya wavu hapo utafanikiwa mkuu
Yeas inawezekana banda lako liwe kubwa sanaKuku ni wa kienyeji
Mimi pia nafunga Kuku wa Kienyeji na Bata.Kuku ni wa kienyeji
Nyavu ipi uliyozungushiaMimi pia nafunga Kuku wa Kienyeji na Bata.
Ninachofanya nimezungushia Wavu toka Bandani, Kwa ukubwa kama wa Mita 3 × 3...!
Vifaranga vikitotolewa vitakaa Bandani ama kutoka nje ya Banda lakini kwenye Nyavu, so hawatoki nje Kabisa, walikua Kwa Bata baada ya mwezi 1 Kwa Kuku baada ya Miezi 2 ama 3, wanakua wameshakua kiasi Cha Kunguru kushindwa kuwabeba Tena, then nakua naruhusu wakatoka nje ya Nyavu kutafuta chakula Chao.
Tatizo ukifuga majogoo mengi yanaishia kupigana tuFuga majogoo wengi utanishukuru baadae
Sasa si uwe unayaamulia na kusuluhisha migogoro yao ambayo inawafanya wapigane au?😂😂😂Tatizo ukifuga majogoo mengi yanaishia kupigana tu
Migogoro yenyewe sasa🤣🤣🤣wanagombea majike kwa hiyo mkuu unataka majogoo yanipande 🤣🤣🤣🤣Sasa si uwe unayaamulia na kusuluhisha migogoro yao ambayo inawafanya wapigane au?😂😂😂
🤣🤣🤣🤣Funga kamba kuzunguka banda lako hasa mbele wanapopitia alafu ning'iniza manati hata 3. Zikiwa zinacheza cheza na upepo kunguru hasogei.
Pia ua kunguru hata mmoja tu au wawili alafu waning'inize kwenye nguzo ndefu hapo bandani, Wewe kaa tafuna korosho sebuleni.
:Mm nimfugaji wa kuku na Bata ila napata changamoto ya kunguru kula vifaranga na mayai bandani wakimuona kuku katoka kutaga wao wanaingia yani ni mwendo wa kuviziana tu niwahi mm Yai au kunguru nimejaribu kuwa winda na manati nimefeli nimeweka sumu kwenye mayai niliyoyatoboa lakini bado wanadunda nilitumia sumu ya panya ya unga kwahyo naomba anaejua mbinu ya kutatua changamoto hii maana ni ndege mwenye akili sana nahitaji mwenye kujua mtego ,sumu au njia ya kuwaamisha
Wana akili sana kuliko ndege yoyote duniani.Hao jamaa wana akili sanaa