Tuanzie na mpango kwanza halafu tunaingia kwenye utekelezaji
Lengo kukutana na watu 1,0000 Tanzania bara yote wilaya 184 na Kila mtu akupe TSh 10,000.Jumla itakuwa ni TSh 100,000,000.
Sasa Tanzania Bara ina wilaya takribani 184. Ukigawanya watu 10,000 kwa wilaya 184 unapata wastani wa watu 50–60 tu kwa kila wilaya. Kwa hesabu hiyo naona ni kitu possible kbs yaani watu 50 tu kutoka mataasisi yote,ofisi,makanisa,masoko na manyumba yote..let's say kila wilaya ipe week moja so huu mradi period yake ni takriban miaka 3 hivi.
Sasa changamoto ndiyo inaanza.kwanza ili kumvua mtu elfu 10 inabidi ujikane kweli.kwanza funga usiwe mtu wa kula kula ovyo yaani jinyime mlo mmoja tu kwa siku inatosha pia usiwe na smartphone kuwa tu na kiswasadu. Cha kufanya msimamishe mtu omba nafasi ya kuzungumza mpe maneno deep kuhusu imani na Mungu kwa ujumla yaani mpe mtu kitu cha kujifunza kutokana na maarifa uliyonayoiwe ni maisha, kazi, biashara, mazingira, au uzoefu wako. Halafu mwisho umwambie kwa heshima kama umeona nimekuongezea kitu leo na una uwezo naomba unisaidie shilingi elfu kumi
Kwanini nimekwambia ufunge na kujitoa katika minyororo ya mazoea mabaya ni ili mtu aone una safari ya kweli si ya maigizo so inabidi ukubali maisha ya kujinyima. Hakuna anasa hakuna starehe, safari ndiyo maisha yako. Unakuwa kama monk anayetangatanga kutafuta lengo lake.kutoka wilaya mpaka wilaya unaomba lift lazima utapata binadamu wema bado wapo sana
nadharia ya huu mpango inawezekana kabisa kwa sababu hata wewe leo ukutane na stranger halafu ni mkweli mdhaifu ila mwenye matumaini na akakutia moyo lazima ungemchangia TSh 10,000 kama una hela uko vzr
NB:yaani kikubwa usiwe na mawazo ya omba omba usiende kwa mtu kama omba omba nenda kwa nguvu na imani na ujasiri na mamlaka..baada ya kazi ngumu ya miaka mitatu uliyokusanya hela sasa mshukuru Mungu na wewe rudisha kwa jamii hata million 10 halafu hizo million 90 kafungue biashara zako...nishukuru kwa hii idea wenye akili na waelewe.