Heart Wood.
JF-Expert Member
- Nov 16, 2014
- 982
- 1,179
Ukifuatilia Takwimu, utasikia TRA wanadai idadi ya walipa kodi nchi hii ni ndogo sana licha ya nguvu nyingi zinazotumika ikiwemo masuala ya TaskForce, kuhakikisha watu wanadai receipts na matumizi ya EFD machines.
Kwa njia hizo, ni kweli kabisa idadi ya walipakodi itaendelea kuwa ndogo. Nini kifanyike?
1) Tujipe malengo ya miaka hata 10 kuboresha na kuunda upya mifumo ya ulipaji kodi ili iwe ya kidijitali. Mifumo hii ina gharama kubwa, lakini ndio njia sahihi zaidi.
2) Hii inamana pia kuwa tutengeneze mifumo na kuhama kutoka kwenye matumizi ya cash na kuwa ya ki-electronic. Ukienda dukani unalipa kwa kadi yako badala ya kushika mipesa mkononi. Hii inamaana gani? Hii inamaana kuwa endapo kutakuwa na idadi kubwa ya watu wanaolipa kwa card za malipo au kadi za banks, VAT itakuwa inatozwa moja kwa moja na itakuwa rahisi kufahamu kipato cha mfanyabiashara kuliko ilivyo sasa ambapo kodi inakadiriwa na makadirio hayo yanaweza yasiwe sahihi.
3) Ukifuatilia kwa karibu, kundi pekee la watu wanaolipa kodi ya kipato (income tax) nchi hii kwa haki ni kundi la waajiriwa walio kwenye sekta rasmi maana vipato vyao vinajulikana na hukatwa moja kwa moja kutolka kwa waajiri wao kwa njia rahisi zaidi.
4) Kundi lingine lililoko kwenye informal sectors, mfano mafundi ujenzi, vibarua mbalimbali, madereva, wafanyakazi wakujitegemea, wasanii, bodaboda n.k hawalipi kodi popote maana kundi hili halijawekwa kwenye mfumo unaoeleweka. Kwahiyo watu wote wanaofanya kazi hata kama ni vibarua wawekwe kwenye mifumo rasmi ili ijulikane wanafanya kazi wapi na kipato chao kikoje na kodi yao iwe kiasi gani.
Nitaendelea.....