Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

I manage to quit alcohol japo sikuwahi kuwa an alcoholic....it is not an easy endeavour hasa bila an intervention from high above.
 
Hilo ni pepo ndugu yangu, maana ukisha lewa unagombana, kubali au kataa hilo ni pepo na usipo angalia lisije likakufikisha pabaya! Tafuta kanisa la walokole wa kweli na fanya urafiki nao wawe wanakuja nyumbani kwako kwa maombi! Mola akuongoze kwenye hiyo safari na akupe haja ya moyo wako ndugu yangu!
 
Kwasababu unatawaliwa na hisia zako [emoji117] rule your mind or it will rule you.
 
Hii ni pesa kidogo sana kuliko mtu anaye honga, kumbuka bar siyo kunywa tu, mtu unaweza kumpa ofa ya bia mbili kesho ukamfuata ofisini akakusaidia kuliko aliyempa rushwa ya laki 2, pia wasio kunywa wanakuwa wanzinzi balaa hivyo wanapoteza pesa nyingi sana kwenye nyumba ndogo.
 
Kama kweli anakunywa ana anzisha ugomvi ni bora aache lakini kama ana kunywa kistarabu sioni tatizo.
 
Hauwezi kwenda bar,ukapunguza pombe kidogo ukiwa na pesa,na hauwezi kuacha pombe kwa kunywa kidogo kidogo
 
Hizi cost za usafiri na kuhonga umezipataje mkuu naomba uzoefu wako japo hunywi!
 
mimi mnywaji mzuri tu. Kunywa pombe hakuna madhara, ilmradi uzingatie kunywa kwa kiasi na kwa mda maalumu. Kunywa kiasi sio unywe kidogo, kunywa hadi ulewe. pia zingatia lishe bora na aina za pombe. maisha Muuuurua kabisa

POMBE ILIUMBWA KUMFURAHISHA MWANADAMU
POMBE NI KAMA UHAI KWENYE ROHO YA BINADAMU
MAISHA YAFAA NINI BILA POMBE?
EE MUNGU ASANTE KWA KUTULETEA KIMEA
ASANTE KWA MIMEA NA VYOTE VITENGENEZAVYO POMBE
ASANTE KWA KUTUPATIA MUDA WA KUPOMBEKA TUWAPO HAPA DUNIANI
ASANTE KWA KUTUPATIA FEDHA KWA MATUMIZI YA POMBE
MLAZE PEMA PEPONI ALIYEGUNDUA POMBE, NI NABII WETU
WABARIKI WOTE WATENGENEZAO NA KUUZA POMBE
WALAANIWE WOTE WANAOPIGA VITA POMBE
WALAANIWE WOTE WANAOCHUKIA NA KUNYANYAPAA WALEVI
OLE WAO WAISEMAYO VIBAYA POMBE - HAWATAUONA MWANGA WA MILELE
OLE WAO WAPIGA VITA POMBE - HAWATAUONA UZIMA WA MILELE
EEE MWENYEZI MUMGU TUNASHUKURU KWA SIKU INGINE TENA
TUNAKUOMBA UTULINDE KATIKA UNYWAJI WETU HADI TUREJEE MAKWETU
UWALINDE WALIOBAKI MAJUMBANI - WATOTO NA WAGONJWA
UWAONGEZEE UVUMILIVU NA BARAKA TELE WAUZA POMBE
UTUPATIE POMBE MILELE NA MILELE
AAAAAAAMINAAAAAAAAAA
 
Chukua hii kutoka kwangu,pombe imenifanyia visa 18 ila kisa cha 14 na cha 18 ndio vipigo vikali zaidi, hasa cha 14,nikiifikiria naiweka tu kwenye kapu,achana na kumaliza pesa mpaka kesho kukopa nauli ya kwenda kazini,au kutafuna mshahara wote kwa usiku mmoja, ntakupa kidogo cha 18, nilipoteza kazi hivyo nilichokua nacho killikua ni kiwanja tu ambacho nilikua nimejidunduliza nikanunua wakati nikiwa kazini,nikajishauri niuze kile kiwanja ili nianzishe biashara, bahati nzuri kikapata mteja nikakiuza bila shida,pesa taslimu milioni 5,kilichotokea baada ya hapo nilisafiri kwenda arusha nikasalimie wazazi na kuwahadithia nilivyoachishwa kazi na kuhusu mipango yangu yanayofuata,nikawaachia hela kidogo nikawaaga,nilipigiwa simu na jamaangu mmoja alikua anaishi arusha,nakwambiaje tulikunywa ile pesa na kubadilisha mademu kwa wiki mbili,nilishtuka ela imebaki milioni moja na elfu semanini,nilikua natoa tu kupitia atm bila kucheki hata balance,toka hapo nikasema jamanieee nakwenda mwenyewe kanisani na naacha pombe tangu jp ile ,leo ni mwaka wa tatu,nakunywa tu juice,dawa ya pombe ni kuamua wewe mwenyewe,halafu nenda kwenye nyumba ya ibada kamwbie mungu nisaidie niache pombe basi
 


duh wewe utakuwa mwenyekiti wa chama cha walevi.

kwa ushawishi huu wajumbe wako sidhani kama wataacha
 
Watu wanaenda bar kwa ajili ya kupanga mipango ya kupata pesa, wanywa pombe ambao siyo walevi wana maendeleo balaa kuliko hata wasio kunywa ambao wanakuwa wanzinzi balaa.
daaah kwel mkuu kuna mtu nilimwambia ni Heri mwanaume awe Mlevi wa Pombe lakin sio wanawake walinishangaa sana ila hawakujua naamanisha nin
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…