Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huna majukumu wewe, halafu unajidekeza saaaaana na kama sivyo wewe ni mtoto wa fisadi flani home kuna hela za kuchota tuuu!
Ati huwezi kuacha bia??? Ungekua unadaiwa maziwa ya watoto, kodi ya nyumba, school fees, pesa ya kutunza wazee, wife hujamvisha, matibabu ya familia yako, msosi kuanzia breakfast, lunch hadi dina,,,,,,,na kwa huo mshahara unaosema mdogo ungepaona bar kama gereza la segerea
jiangalie saaana maana maisha hayamsubiri mtu usikujutia fainali
Dawa iko mimi naivutia muda tuuuu! Aut yangu keshaacha ulevi kabisaaa, akisikia harufu tu ya biereee anatapika mpaka maini!!!!!!!!!
Dawa ni kupima kisoda kimoja cha maziwa ya kitimoto na kumix na bia aina ya Safari. Baaaaaaaaaaass Safari yako imeisha!!!!! Dawa hii watu wengi sana wamewawekew waume zao kwishaaaa habari yao!!!!!!!!! Unawakuta Hongera bar na Soda Fanta nnzi wamewazunguka!!!!!!!!!
Ukishindwa kuna muombeaji anaombea, hadi unatapika, ukitoka hapo hunywi tenaaaa! Mama Lara 1 anataka twende huku tukaokolewe, Mi nimemwambia kaona ujana wake umeisha ndo aniponze, akuuuu! Labda anifunge kamba.
mkuu ngoja nikusaidie mathematicallySister umeongea kwa ukali,,but majukumu yanakuja automatic so hayaepukik muda ukifika,,, nimemaliza chuo na kuanza kazi 2010, kuhusu kodi nimepanga since last year mwanzon na kodi nalipa mwenyewe as kodi ni mwaka mzima so silipi kila siku,, kuhusu wazee I thank God wanajihudumia wenyew as b mkubwa ni mwajiriwa hata yeye, mzee ameshafariki,, muda ukifika nitaoa na kuwa nayote unayotaka but now nachoongelea ni wakati huu nashindwa kuacha beer naombeni mnishauri nitumie njia gani niache as najarib nashindwa
Jaman mi nafanya kazi auditing firms tena big 4, kazi zangu ni stress tupu as daily nina report za kufanya hadi home,, so mara nyingi nikiwa naandaa report home napenda nisindikize na castle light or ndovu as kitu ndo kinatoka poa.. Sio kama nakunywa bia na friends hapana kusema kweli mara nyingi nakunywa kwangu alone, na friji yangu bora ikose vyote but bia lazima ziwepo hata mbili,, ninajitahid kuacha nashindwa.. Mshahara sio mkubwa sana ndo maana nahitaj kupunguza matumizi kwa mambo yasiyo na umuhim na ndo nimeanza na bia, then fuel expenditure as my car ipo sokoni now, then kodi napunguza pia as natoka sinza nahamia changombe NHC house ( msiulizi nimeipataje) as nahitaj nipige hatua na mimi kama wenzangu nijenge hata nje ya mji as nimeplan kuondoka auditing firms after 4 years so ningependa nitoke huku nina kamjengo as sizan kama huko nitakapopata kazi kutakuwa na vi hele hela kama tunavyovipata huku firms.. Japokuwa wanatunyonya partners na kazi zao za stress... I wish niwe na save lak 7 kila mwez ili nijenge hata vyumba viwil vya million 10 au 15 kuanzia january had december mwakan nihamie shamba kwangu then nitafute kazi kwingine as sitak nioe nikiwa bado firm as kaz ni stress tupu kila siku safari na kazi zipo under pressure...
So nifanyeje niache bia nami mwenzenu nijenge kibanda kama nyinyi wakubwa zangu
Heshima kwenu brothers and sisters,
Naombeni ushauri jinsi ya kuacha kunywa bia as nimejitahid nimeshindwa,,, kila nikisema leo naacha najikuta naacha kunywa ndovu nahamia castle light, nikisema tena naacha unakuta natoka kwenye castle light nahamia windhoek,, nifanye nini ili niache maana kila siku nisipopata hata bia 4 usingiz hauji najihis kama mgonjwa.. Hii inakuaje? Maana juzi b mkubwa kaja kunivisit kwangu hadi akachoka as akifungua friji hakuna cha nyanya wala bilinganya ni castle tu zimejipanga hadi nikajisikia vibaya na hapa ndo kwanza 26,,,, nimebahatika kupata ki ajira after school but daily naona mshahara hautoshi but wenzangu wanapata mshahara mdogo na hawana marupurupu yoyote lakini unawatosheleza hii inakuaje,, nifanyeje niache bia mwenzenu
Nimeamua kuwa open as hapa hatujuani lakini tunashauriana mambo muhimu na najua wengi mna njia za kuacha bia..
Naogopa kukushauri maana nami nimo kwenye kundi la wanywaji,so jamani aliyebahatika kuacha kunywa bia anaweza kutusaidia zaidi hapa.
Heshima kwenu brothers and sisters,
Naombeni ushauri jinsi ya kuacha kunywa bia as nimejitahid nimeshindwa,,,...naona mshahara hautoshi,, nifanyeje niache bia mwenzenu
Nimeamua kuwa open as hapa hatujuani lakini tunashauriana mambo muhimu na najua wengi mna njia za kuacha bia..
kuna mtu kakushauri utafute kipopo uweke ndani, ila kinaweza kukusababishia upunguze kunywa kwa muda, ila mapenzi/ ndoa za kibongo migogoro huwa haikawii unaweza ukaja kuzibugia kuliko unavyozinywa sasa ili upoteze mawazo. Na mimi nisaidieni dawa ya kuacha valeur na grant's. Sijui labda tuokoke ndio tutafanikiwa.
mimi sijaacha bia,ila nimepunguza kwa kiasi kikubwa sana,tokea mtu wa bia tatu ,nne kila siku mpaka mtu wa bia tatu ,nne kwa wiki,kilichonisaidia ni kufanya "evening walk" za kutosha,yaaani lazima nitembee kama km 6 kila jioni,by the time nikirudi home nakuwa nimechoka ,ni jumamosi pekee ndio huwa nakunywa kidogo