Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

''When I read the effects of drinking beer, I gave up reading''
 

Sister umeongea kwa ukali,,but majukumu yanakuja automatic so hayaepukik muda ukifika,,, nimemaliza chuo na kuanza kazi 2010, kuhusu kodi nimepanga since last year mwanzon na kodi nalipa mwenyewe as kodi ni mwaka mzima so silipi kila siku,, kuhusu wazee I thank God wanajihudumia wenyew as b mkubwa ni mwajiriwa hata yeye, mzee ameshafariki,, muda ukifika nitaoa na kuwa nayote unayotaka but now nachoongelea ni wakati huu nashindwa kuacha beer naombeni mnishauri nitumie njia gani niache as najarib nashindwa
 

upo sawa kabisa,
kula pombe mpaka ujinga ukutoke,
kama haikudhuru kula kitu bwana.
 
mkuu ngoja nikusaidie mathematically
beer 4= 10,000/day
mwezi =300,0000
mwaka =3,600,000
miaka 5= 18,000,000


hapa nime assume uko peke yako, chukua hatua
 
mimi sijaacha bia,ila nimepunguza kwa kiasi kikubwa sana,tokea mtu wa bia tatu ,nne kila siku mpaka mtu wa bia tatu ,nne kwa wiki,kilichonisaidia ni kufanya "evening walk" za kutosha,yaaani lazima nitembee kama km 6 kila jioni,by the time nikirudi home nakuwa nimechoka ,ni jumamosi pekee ndio huwa nakunywa kidogo
 
Sikia mwanangu. Uwe na hekima na kuongoza moyo wako ktk njia njema.

Usiwe miongoni mwao wanywao pombe, miongoni mwao walao nyama choma na kitimoto.

Kwa maana mlevi na mlafi wa nyama, huingia umaskini. Na utepetevu humvika mtu nguo mbovu.

Mithal 23:19.

Achana na bia.
 
Weigh your options and make the effort. Reduce your circle of friends and get busy because you may be drinking out of emptiness, boredom or too much time on your hands (idleness). You may choose to quit by reducing the amount each day or by stopping all at one. Either way, good luck. It wasnt easy for me, hope it is for you.
I was there, so to speak.
 
Jaman mi nafanya kazi auditing firms tena big 4, kazi zangu ni stress tupu as daily nina report za kufanya hadi home,, so mara nyingi nikiwa naandaa report home napenda nisindikize na castle light or ndovu as kitu ndo kinatoka poa.. Sio kama nakunywa bia na friends hapana kusema kweli mara nyingi nakunywa kwangu alone, na friji yangu bora ikose vyote but bia lazima ziwepo hata mbili,, ninajitahid kuacha nashindwa.. Mshahara sio mkubwa sana ndo maana nahitaj kupunguza matumizi kwa mambo yasiyo na umuhim na ndo nimeanza na bia, then fuel expenditure as my car ipo sokoni now, then kodi napunguza pia as natoka sinza nahamia changombe NHC house ( msiulizi nimeipataje) as nahitaj nipige hatua na mimi kama wenzangu nijenge hata nje ya mji as nimeplan kuondoka auditing firms after 4 years so ningependa nitoke huku nina kamjengo as sizan kama huko nitakapopata kazi kutakuwa na vi hele hela kama tunavyovipata huku firms.. Japokuwa wanatunyonya partners na kazi zao za stress... I wish niwe na save lak 7 kila mwez ili nijenge hata vyumba viwil vya million 10 au 15 kuanzia january had december mwakan nihamie shamba kwangu then nitafute kazi kwingine as sitak nioe nikiwa bado firm as kaz ni stress tupu kila siku safari na kazi zipo under pressure...

So nifanyeje niache bia nami mwenzenu nijenge kibanda kama nyinyi wakubwa zangu
 

let your ambitions be your weapon against alcohol.
 
Embu chukua hii.....jiunge na club yoyote ya mazoezi au kama unaweza jitahidi kila jioni unakwenda gym au kukimbia atleast 40 min kilasiku....me imeniweka pouwa sana.......
 
Kama unayo nia ya kuacha pombe utaacha tu. Badala ya kujaza fridge na pombe, anza kuweka vinywaji vingine ( maji mengi, ginger ale nk). Unaweza kuanza kwa kukata bia badala ya kunywa nne ambayo ni nyingi mno kwa siku, unakunywa mbili. Baada ya hapo jaribu mbili kila baada ya siku moja, kwahiyo badala ya bia 28 (!!!) kwa wiki zinakuwa 14. Punguza hadi unakunywa labda moja kila baada ya siku kadhaa ambayo sio mbaya. Si lazima uache kabisa, lakini kumbuka kitu kikikukosesha raha , unatumia pesa mpaka unashindwa kuweka akiba au kujiendeleza ujue kwamba inabidi ubadili tabia kabla haujaingia kwenye matatizo. Mwishowe utaongeza iwe 6 kwa siku, halafu utaanza kusema huwezi kufanya kazi bila kinywaji utaanza kunywa kabla ya kuenda kazini. Be very careful. Epukana na vishawishi pia. Kumbuka kisukari hakina tiba.

Naomba kuuliza unamaliza kazi mida gani? Huna shughuli za kufanya ukimaliza kazi? Kusafisha nyumbani ? Biashara au project zako za pembeni? Unafanya mazoezi? Yote haya yanaweza kukusaidia kuepukana na vishawishi vya kunywa pombe. Ukijikeep busy utakuwa huna nguvu za kunywa tena, usingizi utakuja kirahisi zaidi, na utakuwa unajiendeleza bila kutapanya pesa zako.





 
MKATA KIU, nothing is impossible to the willing heart. Tii wito wa moyo wako. Hakuna hata mmoja wetu awezaye kukushauri vema zaidi yako mwenyewe though sisi tumeitikia wito wako. Uamuzi ni wako, jitoe ktk utumwa wa pombe. ALAMSIKI.
 
Last edited by a moderator:
Naogopa kukushauri maana nami nimo kwenye kundi la wanywaji,so jamani aliyebahatika kuacha kunywa bia anaweza kutusaidia zaidi hapa.

mimi niliacha, ni uamuzi tu! Kwani anakunywa ngapi? Unakuwa na kundi wakati wa kilaji? Unatakiwa kupunguza kwa dozi kama ni mnywaji wa kila siku. Kama ulikuwa unapiga 10 endelea kwa wiki aafu punguza ziwe 7. Baada ya wk 2 unapunguza kuwa 4 unamaintain kwa mwezi m1. Ukitoka hapo ni mbili kwa mwezi then moja mpaka utaacha. Inahitaji uvumilivu sana! Umeoa lakini? Shem anakunywa? Kama hanywi mpe kazi hiyo ataiweza kama ni mwanamke na siyo msichana mkubwa. Mimi tangu niache ni miaka mitatu sasa na huwa nakwenda na jamaa zangu bar kama kuna mtoko, wao beer mie malta kama kawa!
 
Inawezekana kuacha ni mamuzi tu tafuta vinywaji bisivyo na kilevi vyenye ladha ya bear kula na nyama ya kuchoma na ndizi choma asubuhi glass ya juice mbona unaacha tu maji ya kutosha ni muhimu.nite.

Nayanda.
 

Sio lazima kuacha kinywaji unachokipenda..kama hakikuletei athari yoyote kiafya basi tafuta kibarua cha ziada/kazi ya pili na kama mshahara utakuwa hautoshi,tafuta kazi ya tatu.

Utakuwa unatafuta pesa kushibisha kiu yako ya kinywaji.

Siku ukichoka kufanya kazi, utaacha kinywaji bila kupata ushauri. Itafikia muda,utaweza kujishauri mwenyewe.

La msingi weka mahesabu ya bia ngapi unakunywa na shilingi(dola,pauni,euro) ngapi unatumia kwa mwezi. Baada ya mwaka unaweza kujiuliza badala ya bia hizo hela ungezitumia kufanyia nini kujiinua kimaisha au kusaidia familia yako(baba,mama, ndugu na jamaa).
 

Uokoke? Kwani ukiokoka ndo unakatazwa kunywa bia? Mafundisho potofu kabisa. Huyo unayemfuata kwenye wokovu ndo mtaalam wa kutengeneza pombe. Source: Harusi ya Kana. Na isitoshe aliamua kugeuza pombe kuwa damu yake, unadhani alishindwa kugeuza maji yawe damu yake?? STUKA!!

Niitie mwalimu wangu snowhite anisahihishie huu mtihani ambao nna uhakika nimepata A+
 
Last edited by a moderator:
Unaweza kunywa bia kila siku kwa sababu huna malengo yoyote ya maendeleo. Maisha ni zaidi ya kunywa na starehe.
 

dawa si mazoezi ndugu njoo kwa Yesu ataondoa kiu yote ya pombe na zaidi ya hapo utaupata uzima wa milele
 
jaribu kuwa na control, lakini kuacha bia itakula wako kunywa kwa kiasi na panga ni muda gani wa kunywa hasa wakati wa usiku tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…