Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza


daa we noma.yaani unawapiga m23!
 
mimi niko na record ya kunywa miaka mitano daily...ukiacha ndoto za kutisha,tremor,kushituka ,nikaona enough is enough naenda mwaka wa pili sijagusa alcohol.
 
Duh kuna watu humu sijui wana zile simu za kifisadi za February maana wanamwaga pumba nyingi kama za Magulu. Kwanza kuna mtu anasema eti kichaa hakiponi (you can't generalized maana kuna vichaa vya aina nyingi).
Hakuna hasara yoyote ya kuacha ghafla ingawa inategemea ulikuwa mnywaji au mlevi. Kwangu mimi ulevi ni alcoholsm, sasa hao ndiyo unaosikia habari ya kutetemeka mikono n.k na hiyo inaweza kuwa sababu ya withdrawal..

Kama unaweza kuacha ghafla basi wewe ni mnywaji. Hii tabia zote ni psychological na ukijiambia na kuamini kuwa huwezi kulala au kubanjua bila fegi au kupata kinana baridi basi utajenga hiyo tabia na mwili utajijenga hivyo. Mimi nilianza mwaka juzi kujipangia katika kila mwaka, naacha mara mbili kwa mwezi mzima. Nimekuwa nafanya hivyo na kipindi hicho tizi nazidisha mara mbili na kubwia sana maji, na bado nakwenda baa na kunywa club soda au tonic water. Ila sababu ya uchovu wa tizi unajikuta huwezi kukaa sana mwili unakuwa hoi so ukirudi home unauchapa usingizi kwa raha zake. Kwenda baa kwa muda wakati umeacha kunasaidia kuijenga akili na kuipiganisha na vishawishi vingine taratibu ( pia kuona upumbav unaoufanya kwa kuona walevi wenzio ..) ingawa kutegemeana na hao washkaj ulionao inaweza kuwa shida pia maana kuna siku mshkaj aliziweka mpaka akawika ndani ya gari wakati wa kumpa lift...!!

Ukiacha utajikuta afya inajengeka vizuri sana, unaweza kupata ladha ya chakula vizuri na kama walivyosema wengine matunda na mboga za majani kwa wingi ni msingi mzuri wa kurejesha afya.
 
Benjamin Franklin said it best: "Beer is living proof that God loves us and wants us to be happy." So mtajijua msiokunywa, usiache utakuwa malaya balaahhh
 
Benjamin Franklin said it best: "Beer is living proof that God loves us and wants us to be happy." So mtajijua msiokunywa, usiache utakuwa malaya balaahhh

Unajuwa ni kwanini watu wengi wanaoacha pombe au wasiokunywa pombe wanakuwa malaya? ni kwa sababu unapoacha vilevi mwili unakuwa na nguvu sana tena nguvu za asili, kwahiyo kama hujaoa hii inaweza kukusumbua, lakini mhimu ni kuzidisha mazoezi hasa ya kutembea au jogging wakati huo huo kujitafutia kitu cha kukufanya kuwa bize kama vile computer, michezo nk.

Inawezekana tu kuacha pombe au kilevi chochote, la mhimu ni WEWE mwenyewe kusema sasa basi, ndiyo kuna shida za hapa na pale zitajitokeza lakini ukivumilia mwisho utafanikiwa.
 
Wadau ningependa kujua njia za kupitia ili kuacha pombe kwa mtu ambaye ni adicted
 

Chakuchambuka, miezi 4 sasa imeshatimia toka uombe ushauri wa kuacha kunywa pombe! Vipi maendeleo yako baada ya kupata ushauri na kuufanyia kazi, umefanifanikiwa kuacha au bado unakunywa pombe?
 
Kuna jamaa aligongwa kabaaang yake kutokana na kulewa sana ikawa ndo story pande za Mpiji magohe,jamaa alikuwa maarufu kila bar na totoz. Jamaa siku mbili tatu akaonekana mtaani na alikuwa hasikii aibu yoyote,baada ya mwezi 1 akagongwa tena. Watu wakaona ndo mchezo wake.
 
hahahaha kweli kilaji noma poleni walevi kikubwa munatakiwa kuacha madhara ni makubwa sana
 
Tupe historia yako kwanza katika pombe. Ulianzaje? Na jinsi gani uliendelea mpaka hapo? Ulianza kwa matatizo (stress) au kwakufuata mkumbo wa marafiki? Je, unamke au mume? Anakunywa? Anaimani gani?
 
Nifanyeje niache pombe jamani. I cant sleep bila bia moja au Mbili.

Nahitaji msaada, mpaka muda huu naandika hii nina hangover ya jana.

Natanguliza shukrani.
 
endelea kunywa tu mkuu yaani kula ujana but pale majukumu yatakapokuzidi itakuwa dawa ya bila gharama!!!
 
Mkuu panga ratiba yako upya..Muda uliyokuwa unaenda kupata moja au mbili..Fanya kitu kingine kusoma vitabu,Mazoezi..nk

Jiepushe na marafiki ambao wana Ratiba ya moja ..mbili..

Amini unaweza ku-enjoy..bila pombe..pia sio nzuri ki-Afya..

Wazo zuri sana kuacha..:thumbup:
 
Nifanyeje niache pombe jamani. I cant sleep bila bia moja au Mbili.

Nahitaji msaada, mpaka muda huu naandika hii nina hangover ya jana.

Natanguliza shukrani.
Pole sana. Hebu nikuulize:Ulipoanza kunywa pombe ulienda mahali kuomba msaada wa jinsi gani ya kunywa pombe?
Bila shaka jibu ni hapana; uliamua tu mwenyewe kuanza kunywa pombe. That's the point I am driving at. Drinking alcohol and quitting drinking is a factor of your personal will and choice. Ukitaka kuacha kunywa pombe au hata kuvuta sigara, anza na nafsi yako. Iambie nafsi yako hivi: Kuanzia leo sitaki tena pombe wala sigara. Epuka marafiki wanywa pombe na wavutaji. Binafsi mimi nilifanya hivo mwaka 1993 kuacha kuvuta sigara na mwaka 1998 kuacha kunywa pombe. Mpaka leo sivuti wala sinywi pombe. Nimejinyima vyote. Kwa uzoefu wangu kuacha kunywa pombe ni rahisi kuliko kuacha kuvuta sigara. Uraibu wa sigara ni mkali kuliko wa pombe.

Tafuta siku ujiambie: 'KUANZIA LEO SITAKI TENA POMBE' Usijidanganye kwamba kuna dawa ya kuacha kunywa pombe au
kuvuta sigara. Dawa ya kweli ni uamuzi wa nafsi yako.
 

Asanta sana Sheika
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…