JE ULIKUWA UNATAMBUA KUWA ULEVI SUGU NI UGONJWA?
KWANZA KABISA ULEVI SUGU (ALCOHOLISM) NI NINI?
Shirika la Afya Duniani (W.H.O) lilithibitisha kuwa ulevi sugu kuwa ni ugonjwa sugu tangu mwaka 1949. Baada ya hapo ugonjwa huu umeendelea kusababisha vifo vya maelfu ya watu duniani. Hapa Tanzania pia watu wengi wameathirika na ugonjwa huu.
(Utafiti wa W.H.O umedhibitisha kuwa watu millioni 2 na nusu wanakufa kila mwaka kwa sababu ya unywaji wa pombe kupindukia)
MAGONJWA SUGU NI YAPI? Ni kama Ukimwi (HIV AIDS), DIABATES (KISUKALI), KANSA (CANCER), PRESSURE (MAGONJWA YA MOYO). Kumbuka magonjwa sugu ya hatua za (awali, kati na mwisho) kwa maana nyingine hauna TIBA.
HATUA YA KWANZA NI YEYE KUKUBALI KWAMBA ANA TATIZO NA YUKO TAYARI KUACHA YEYE MWENYEWE BILA SHINIKIZO LA MTU AU KITU CHOCHOTE.
Kwahiyo mi nakushauri mtafutie huyu jamaa yako umoja wa watu walioacha au wenye nia ya kuacha ULEVI SUGU uitwao:
Alcoholics Anonymous (A.A) ni ushirika wa wanaume na wanawake ambao wanashirikiana ujuzi, nguvu na matumaini kati yao ili waweze kutatua matatizo yao na kusaidia wengine kupona ulevi.
Sharti pekee la uanachama ni nia ya kuacha ulevi. Hakuna ada ya kuwa mwanachama wa A.A, tunajitegemea wenyewe kwa michango yetu wenyewe. A.A haifungamani na madhehebu yoyote ya dini, siasa, shirika au taasisi na haitaki kujiingiza katika mabishano yoyote. Kadhalika A.A haiungi mkono wala kupinga chama chochote.
Nia yetu ya msingi ni kukaa bila kulewa na kuwasaidia walevi wengine kupona kutokana na ulevi.
A.A ni kwa ajili ya mlevi ambaye ana
NIA YA KUACHA KUNYWA POMBE. Kama unadhani una tatizo la ulevi, unakaribishwa sana kuhudhuria vikao na mikutano.
Nakutakia mafanikio mema.
Usisite kuwasiliana nami ili nikupatie maelekezo zaidi:
+255 789 780 529,
E-mail: rnelsontz@yahoo.com