Ngalikihinja
JF-Expert Member
- Sep 1, 2009
- 33,643
- 36,090
Hii ndo shida ya kunywa karibu na mochwari............Mimi niliacha pombe baada ya kusahau nyumbani nakupitiliza mochwari na mlinzi alivyo mhuni akanilaza kwenye jokofu kwa dakika 3 mpaka leo nimeokoka.
Sisi kule kwetu pombe ambayo inapatikana kwa wingi inaitwa ulanzi. Sasa tukiona mtu ni munywaji sana, kiasi cha kwamba amepitiliza, huwa tunamwekea konokono mbichi kwenye huo ulanzi halafu unamwachia lita nzima anywe peke yake. Iwapo haangalii, anaweza ama kumtafuna huyo konokono au akapitiliza tumboni. Akipitiliza tumboni ni bahati yake, lakini akimtafuna basi hatakaa anywe ulanzi tena, manake akiuona tu atakuwa anasikia kichefuchefu. Sasa kwenye mbege sijui tunaweza kuweka nini?
Kaka, kuacha pombe is a mind game. Ukitaka kuacha pombe, kama we ni mnywaji bia, hata kama huwa unakunywa kreti tatu unatakiwa uache bia moja tu! Utakua umefanikiwa.
Jizuie usinywe ile bia ya kwanza. Basi.
Wandugu natafuta dawa ya kuacha pombe jamani. Nisaidieni kila nikikumbuka ze pombe naamishia ofisi kaunta. Yaani ndugu nateseka sana. Halafu nikisha kunywa nahamasika sana na mchezo wa ule wakati watoto wamelala. Nifanyeje jamani?
Bana sinywagi mbege bana. Mi nakunywa safari ka 18, ndovu sijui ngapi maana huwa nakunywaga tuuuu, sitaki serengeti maana ina kama kaharufu fulani hv, Valuer kama 3 ama nne hivi, Konyagi zile kubwa kama 4 hv sasa nitaachaje?
Hata asipoenda bar anaweza kuagiza akawa ananywea nyumbani au hata ofisini. Kuacha pombe ni kazi ngumu sana!!!kaka kuacha pombe ni rahisi sana, wala usitumie dawa yoyote, Dawa acha kwenda bar au Grossary yoyote. Mimi mwenyewe nilikuwa nakunywa sana na nikaapa kwa mchumba wangu ambaye sasa ni mke wangu kuwa mimi sitaacha pombe, katika maisha yangu. lakini nilishaacha na dawa ni kutokwenda bar sasa huu ni mwaka wa saba. Ingawa siku zile za mwanzo mwanzo nilikuwa siku moja moja napata moja baridi.
kwa sasa nilishaacha kabisa. wala usitumie dawa yoyote we usiende bar.
wandugu natafuta dawa ya kuacha pombe jamani. Nisaidieni kila nikikumbuka ze pombe naamishia ofisi kaunta. Yaani ndugu nateseka sana. Halafu nikisha kunywa nahamasika sana na mchezo wa ule wakati watoto wamelala. Nifanyeje jamani?