Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

Kama unataka kuacha pombe, nenda kanywe katika Bwalo la Jeshi alafu ulewe chakali alafu uanzishe fujo apo ndio utakuwa Umeacha kunywa pombe
 
Nahitaji Msaada wenu wataalamu ninachukia tabia niliyonayo ya kunywa pombe naomba kusaidiwa nini dawa ya kunywa ili niache kinywaji hiki?

Sio kwamba na kunywa kila siku huwa na kunywa Mara moja moja Ila nalewa sana kiasi cha kunivunjia heshima yangu na kila Niko jitahidi kuacha siwezi. Nimejitahidi kuikataa akili ni Ila baada ya muda nimeanza tena sasa ninachoomba kusaidiwa ni dawa kiboko ya walevi kama Mimi. Nikome kabisa kunywa pombe.

Najiuliza wengine wanaachaje mbona Mimi nashindwa
Madokta wataalamu wa tiba zote ziwe za kimila au Mbinguni au maarifa ya kawaida mnisaidie.
asanteni
 
Sanya
Pole sana kwa kipindi kigumu ulichopitia

Uraibu wa Pobe ni ugonjwa wa kimwili kiakili na kiimani ambao unaathiri maeneo yote ya maisha yetu, Mtu anapoathirika akili mara nyingi huangazia kunywaaa tuuuu au kutumia mihadarati , na anapoathirika mwilini hupata maumivu au hali ya sintofahamu kila anapoamka na kuufanya mwili uwe unahitaji Pombe muda wote ili uweze kufanya shughuli kama kawaida

ili kuweza kuondokana na tatizo hili ni vema kumuona dakatari kwa ajili ya kufanyiwa detoxfication baada ya hapo utafanyiwa Tabia Tiba (Cognitive behaviour Therapy) itakayosaidia kubadilisha fikra hisia na tabia ambazo zimazalishwa na uraibu wa pombe

baada ya hapo utakuwa na wezo mkubwa wa kukabiliana na kumili hisia zako kama vile wasiwasi(Anxiety) Hasira na depression ambazo ndio trigger kubwa zinazomrudisha mtu kunywa pombe mara kwa mara hata kama ameweza kuacha kwa muda muda flani

Mwisho utaungana na ushirika wa kujitolea wa watu waliacha kutumia mihadarati na pombe (www.na.org) au (www.aa.org) duniani ambao utakusaidia sana kuendelea kubaki safi bila ya kutumia

simply tunapokiri hatuna nguvu dhidi ya utumiaji wa pombe na kuamini Mungu ndiye anatuondolea udhaifu huo na kukata shauri kumrudia Mungu huku tukijichuguza barabara bila woha hulka kamili ya makosa yetu

tunakuwa katika wakati mzuri wa salama ya kuishi bila kunywa
 
Ukiitii dhamira yako ya kuacha utaacha tu,
Ukiwa na mawazo ya mpaka upate mbadala umekosea
Pamoja na kujiwekea UADUI na Mungu kwa kunywa pombe , pia unaua uchumi wako na afya yako
 
Dawa yake ni kuacha kutafuta hela.
Ukiwa huna pesa sio rahisi kuhudhuria sehemu za starehe.
 
Mi kuokoka tu mkuu Hamna nyingine, ukiokolewa unapewa uwezo Wa kushinda dhambi sio tuu ulevi Bali dhambi zoote. Kikubwa toba yako iwe ya kumaanisha sio mzaha hapo Yesu huingia moyoni nwako na kutake lead
 
c42bce288205d00c5bddfe9f7858674d.jpg
 
Naomba msaada kwa anaefaham dawa ya kuacha pombe
Disulfiram
Initial dose 500mg po daily in AM for two weeks
maintanance regimen 250 mg po daily may be required for month's or even longer.
WARNING
Alcohol consumption while on that medication is guaranteed to cause serious reaction.
THIS POST IS JUST FOR EDUCATION AND INFORMATION ONLY ON AVAILABILITY OF ANTI-ALCOHOL MEDICATION,NO A PRESCRIPTION TO START THAT TREATMENT REGIMEN.
 
Hutakiwi kuijua, mwambie ndugu yako akutafutie ili akutunzie hiyo siri ya hiyo dawa
 
Nenda kanisani, shika mafundisho ya Mungu, jali familia yako, jiweke mbali na walevi wenzako
 
eaea09928a4878b262cd1e79ea3e9065.jpg

je unataka kuacha pombe lakini unashindwa? basi angalia jinsi ya kupata msaada. siku hizi kuna dawa zimeingia kwenye soko la dawa ambazo zinaweza kukusaidia kuacha pombe, dawa hizi hazikuachishi pombe lakini zinaleta hali ambayo utajikuta hupendi kunywa pombe yaani ukinywa huoni raha tena.

matibabu haya yanatakiwa yaende na njia zingine za kucha pombe kama ushauri, kuamua moyoni kuacha, kuomba msaada kwa marafiki, kukaa mbali na wanywaji, kuepuka kukutana bar na rafiki zako na kadhalika.
zifuatazo ni dawa husika za kuacha pombe

[emoji117] disulfiram; hii ni dawa ya kwanza kabisa iliyogunduliwa ya kuwafanywa watu kuacha pombe, inafanya kazi kwa kuzuia mwili kuondoa pombe mwilini baada ya kunywa na matokeo yake mtu huweza kukaa na hang over kwa muda wa mpaka wiki mbili.

Mtu hujisikia kichwa kuuma, kutapika, kuishiwa nguvu, kuchanganyikiwa, kutokwa jasho sana, kupumua kwa shida, na kushindwa kuona vizuri kila anapokunywa. mtumiaji hutapaika sana kama mtu aliyekunywa sumu kila akigusa pombe. hali hii humfanya mtu aiogope pombe kabisa.
fcbdb52c1e5e08cf572a12cedca670ab.jpg

[emoji117]naltrexone; hii ni dawa ambayo inafanya kazi kwenye ubongo, kitaalamu kuna sehemu ya ubongo ambayo hupata raha mtu anavyoendelea kunywa pombe...dawa hii huzuia sehemu hiyo ya raha na kumfanya mtu asione raha yeyote kunywa pombe.

Watu wengi hunywa pombe sababu kuna raha wanaipata wakati wanakunywa pombe hivyo wakiikosa raha hii hulazimika kuacha. dawa hii haina madhara ya kutapika kama ile ya mwanzo, dawa hii huchomwa kama sindano kwa mnywaji kila baada ya muda fulani mpaka atakapoacha kabisa.
a39400b7a103a1ad20bff01828819fc6.jpg

[emoji117] acamprosate; mtu ambaye amezoea pombe hawezi kuacha ghafla kwani anakua ameshaizoea mwilini kitaalamu kama addiction hivyo akiacha ghafla hupata matatizo ambayo yanaitwa kitaalamu kama withdraw syndrome ambayo mtu huapata dalili za wasiwasi, kutetemeka,kukosa usingizi, na kutokwa na jasho, sasa dawa hii humsaidia huyu mtumiaji arudi kwenye hali yake ya kawaida baada ya kuacha pombe bila kupata hayo madhara niliyotaja.
080adf8f068e6551d90f66e7d4c3747d.jpg

mwisho; dawa hizi hupewa kwa watu tu ambao wako tayari kuacha pombe na mgonjwa asiwekewe kwenye pombe yake au kunyweshwa bila mwenyewe kujua kwani hiatamsaidia. kabla ya kuanza dozi ni vizuri daktari aliyekaribu na mgonjwa afahamu ili kama madahara ya dawa yakiwa makubwa aweze kumsaidia muhusika.
 
Back
Top Bottom