Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

Changanya MAVI ya kuku ktk hiyo glass ya bia, konyagi, ama pombe yoyote unayokunywa. Kunywa na maliza kama glass mbili hivi na usisikilize ladha yake wakati unakunywa.
Baada ya nusu saa utatapika sana.

Unless this is a joke....

Kwanini ufikie hatua ya kufanya hivi kisa ati unataka kuacha pombe? Dawa pekee ni KUAMUA kuacha tu. Enzi zile ninatandika mtungi kwa sana uncle wangu alikuwa ananiambia ''Kama ni LAZIMA ukae bar na unywe kitu, kwa nini usinywe maji au maziwa''??
 
Namuunga mkono 100% I have tried This na nimeweza
 
uache pombe kwani unataka kuwa mchawi au. wasiokunywa pombe ni wachawi na wale wenye mashetani. pombe deal ila usizidishe tu.
 
uache pombe kwani unataka kuwa mchawi au. wasiokunywa pombe ni wachawi na wale wenye mashetani. pombe deal ila usizidishe tu.

Sio kweli.
Ulevi ni ulevi tu! haijalishi kuzidisha au kutozidisha.
Karibu katika ulimwengu wa Juice.
 
Kuacha kunywa Pombe nakushauri kanunue pombe kama ni Bia au pombe yoyote ile unayokunywa kisha nenda Makaburini kaiweka juu ya kaburi ikae siku moja masaa 24 kisha siku inayofuata siku ya pili nenda kaichukue kisha unywe hutakunywa tena maisha yako ndio dawa yenyewe hiyo hebu jaribu kisha utaniambia matokeo yake
 
Uncle wangu alikua mlevi wa kupindukia..baada ya kuacha kurudia mara kadhaa mwaka juzi akafanikiwa kuacha!Yani hata hakutangaza anaacha tulishangaa tu kabadilika!Mpaka leo hajagusa!Natamani angekua karibu nimuulize alitumia njia gani ila ndo kama hivyo tena!Lakini ukweli ni kwamba wala hauhitaji dawa..kama umedhamiria kuacha kweli ni kiasi tu cha kujizuia!Vuta soda yako au maji wakati wenzako wanasakata Safari!Mwanzoni watakucheka ila we puuza..siku ya siku utajikuta huoni umuhimu wa pombe tena!
 
tatizo sababu za kuacha pombe ulizoziainisha ni za kwako mwenyewe na sio lazima ziapply kwa wengine e.g kuchelewa ofisini, kuchukua barmaids na machangu, drinking daily! Haya si matatizo ya kila mtu! So struggle urself
 
Kwanini uache pombe bana?? Utaanza umbea, nak ugombana na watoto home. We punguza tu kwani huwezi kupunguza kama unalewa sana usiende bar unazofahamiana na watu kwa sana nenda bar kama vy the way tu unapita hupati ofa. Halafu jifunze kutotembea na ATM na pesa nyingi uwe na kama 20,000 Tshs tu kwa siku hutaspend sana
 
tatizo sababu za kuacha pombe ulizoziainisha ni za kwako mwenyewe na sio lazima ziapply kwa wengine e.g kuchelewa ofisini, kuchukua barmaids na machangu, drinking daily! Haya si matatizo ya kila mtu! So struggle urself

Ukweli utabaki pale pale. Hizi ndio characteristics za walevi wengi
 
Asante sana kwa ushauri huu!!
Naomba nitoe shukrani kwenu nyie wote kwani Leo nakamilisha mwezi na siku Mbili sijapata hiyo kitu.
nimeamini inawezekana, Ninaambiwa na wengi pia nimepumzika tu nitarudia ulabu, But I diont see myself back there again.
jamani acheni utani pombe inamaliza pesa!! ukitaka kujua hili acha pombe hata kwa wiki moja tu, kama wewe ni mlevi daily.
 
Is this a joke?

sijajaribu kwa kuwa sijawahi kuwa mnywaji wa pombe. Ila jamaa yangu mmoja aliwahi niambia kuwa hiyo ni tiba mbadala ya kuacha pombe (mavi ya kuku na bia-kama mr mlalache alivyoshauri)!! you can try and inform us later the outcome, no matter what??
 
This must be a joke. kwanini ule mavi ya kuku?
 
una girlfriend au mke? kama yupo anatumia vileo? kama hatumiii amewahi kushauri uache? kama amewahi kushauri ulimjibu nini? nauliza haya maswali kwasababu kama una GF unayempenda ni rahisi sana kuacha endapo tu na yeye hapendi... Ushauri.... kila unapojisikia kunywa fanya mapenzi na GF wako na muendeleee na story za mahaba mpaka jioni kisha usiku.... au movies nzuri tizama na umpendaye...

Tatizo ni kama huna demu... ushauri wagu hapo hautafanya kazi..... afu si lazima ukinywa mpaka uzime... ndo maana wajutia asubuhi unapoanza ku HANG OVER
 
Mi huwa nawaambia, kuacha pombe means kuacha kunywa bia MOJA TU! Yani we pambana ujizuie kunywa bia moja, utaacha pombe milele. Bia moja itakushinda kuacha? Ile bia MOJA ya kwanza ukishaweza kuiacha kazi kwisha! Huitaji mavi ya kuku wala nini..
 
there is a place where they provide services to help you quit alcohol drugs or cigarate. they organise rehabs and group support for alcoholics where you get a very good support and your problem will remain as history. contact them through psychologicalsupport@hotmail.com
 
Uache pombe unataka kuanza kushinda kwenye kahawa nini?we punguza tu bana uwe unakunywa kiasi,me mwenyewe hata nikiona tangazo la bia kwenye TV mate yanajaa mdomoni,aah subili kidogo naludi.
 
kama umeshajua madhaifu unayoyapata baada ya kunywa kama ulivyoorodhesha inakuwaje ushindwe kutumia mapungufu hayo kuacha pombe. inavyoonekana ni kuwa hata ukifahamu mkeo anachakachuliwa hutaweza kumwacha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…