Njia za kupata mtaji wa biashara

Njia za kupata mtaji wa biashara

demarine

Member
Joined
Dec 6, 2020
Posts
18
Reaction score
29
Tatizo la kukosa mtaji limekuwa kubwa mno, watu wengi wanandoto za kufanya biashara ili kujikwamua kiuchumi, kila mtu anatamani walau afanye kitu kwaajili ya kupata rizki ila wanashindwa namna ya kuanza kufanya yote kwasababu ya kukosa fedha.

Hizi apa njia kazaa ambazo unaweza tumia ili kupata mtaji;

1. Weka akiba binafsi.
nidhamu ya pesa ni kitu cha umuhimu ivo basi tujitaidi kubana matumizi hakikisha unapopata fedha angalau u save kiasi kidogo kwa maana haba na haba ujaza kibaba.punguza matumizi yasiyo na ulazima pia tuishi kuringana na uwezo wetu, watu wengi tunaishi maisha ya kuigiza jambo ambalo linapelekea kuwa na matumizi makubwa tofauti na tunachoingiza. Anza kueka akiba kijana mwenzangu ili kufikia ndoto zako.

2. Badili ulichonacho kuwa mtaji.
unaweza kuwa na kitu cha thamani ambacho uwenda hauna matumizi nacho sana ukakiuza na kikakusaidia kupata kiasi cha fedha ili kukizi maitaji yako ya biashara/ujasiriamali. Kwa mfano waweza kuwa na simu ya thamani ukaiuza na iyo pesa ukaitumia kufanya biashara zako alafu badae biashara ikichanua waweza nunua tena.

3. Ubia /ushirika.
kumbuka sio kila mwenye pesa anawazo la biashara kuna watu wanapesa ila wanakosa pakuwekeza, apa chakufanya andaa wazo lako la biashara vizuri kisha tafuta watu wenye fedha au interest na biashara wape hayo mawazo au yawezekana una pesa lakini aitoshi kufanya unachotaka apo unatafuta mtu ambae mpo na interest sawa mnafanya kazi kwa ushirika.Kikubwa mnakuwa na mkataba juu ya ugawanyaji wa faida.

4. Mikopo.
hii ni moja kati ya njia ambayo wajasiriamali wengi wanaitumia, vipo vyanzo vingi vya mikopo ikiwemo mashirika/taasisi za kifedha kama BENK ,pia waweza kopa kwa mtu binafsi au taasisi za serikari ambazo zinakopesha. Lakini kumbuka kabla ya kukopa fanya tathmini kwa umakini juu ya biashara unayotaka kufanya ili usije kujutia.

5. Ndugu na marafiki.
Ukiishi na watu vizuri kuna uwezekano mkubwa wakukusaidia ktk kufikia malengo yako.kikubwa unachotakiwa kufanya washirikishe kuhusu wazo lako na uwaambie faida ambazo wao pia wanaweza kupata kupitia kile ambacho unataka kukifanya, mwisho ukumbuke kurudisha fedha zao ama uwaahidi kuwa utarudisha baada ya muda furani ili iwe rahisi kwa wao kukupata izo fedha.

6. Kufanya kazi.
watu wengi wamekaa na mawazo ya kutaka kufanya biashara/ujasiriamali lakini awataki kufanya kazi zingine ambazo zinaweza wasaidia kupata fedha, amka kijana mwenzangu tafuta pesa mtaji auwezi kukufata ulipo ila wewe yakupasa kupambana ili kuupata.usione aibu fanya chochote cha halali ili ujikwamue apo ulipo.

7. Kushiriki kwenye mashindano.
yapo mashindano mengi ambayo uwa yanafanyika jaribu kushiriki uko uwenda ikawa ndo njia yako ya mafanikio tunaona watu wengi kupitia mashindano wanapata fedha za kutimiza ndoto zao. Kama unakipaji kitumie kuingia uko kwenye mashindano ya vipaji pia yapo mashindano ya kuibua ujasiriamali waweza shiriki pia.

Mwisho : changamoto ni nyingi mno akuna sehemu unayokwenda usipate Chang'amoto,akuna kazi utakayo fanya isiwe na changamoto kikubwa tusikate tamaa tufanye kazi kwa bidii uku tukimwomba MUNGU ipo siku tutayaona mafanikio .Rizki yako ipo mikononi mwako pambana kijana mwenzangu GOD WILL MAKE A WAY.

Screenshot_20210306-160516.jpg
 
Back
Top Bottom