SoC04 Njia za kutatua ajira kwa vijana wa kidato cha nne na cha sita

SoC04 Njia za kutatua ajira kwa vijana wa kidato cha nne na cha sita

Tanzania Tuitakayo competition threads

MTAKASIMBA_PRINCE

New Member
Joined
May 16, 2024
Posts
1
Reaction score
1
SOKO LA AJIRA KWA VIJANA WENYE ELIMU YA KIDATO CHA NNE NA KIDATO CHA SITA.

TUJIULIZE MASWALI YAFUATAYO.

  • Je vijana wenye elimu ya kidato cha nne na sita wanasaidiwaje katika soko la ajira?
  • Je mfumo wetu wa elimu umewatengenezea ujuzi wowote hawa vijana waliohitimu kidato cha nne na cha sita na kushindwa kuendelea na chuo?
  • Miaka yote aliyotumia kusoma ni sawa na bure kama ameondoka hana ujuzi wowote zaidi ya kuchora mende?
  • Mfumo wetu wa elimu unaongoza kuua vipaji vya vijana mashuleni?
  • Je hawa vijana hawana umuhimu katika maendeleo ya nchi yao?
Siku za hivi karibuni vijana wengi wa kidato cha nne na sita wamepatwa na changamoto kubwa ya ushindani katika soko la ajira hali inayofanya kuona hakuna kitu wanaweza fanya kupambana na hali hiyo ili kujikwamua kiuchumi hata ambao wana ujuzi mbalimbali bado wanapata changamoto kutumia ujuzi walionao ili kujikwamua hii inaweza kutokana na mfumo mzima wa elimu ambao umemlemaza huyu kijana mwenye kipaji au ujuzi kushindwa kutumia uwezo wake kujikwamua kiuchumi wengi wanabaki tu mtaani.

Hata wakati mwingine hao wenye ujuzi wanakutana na changamoto ya kukosa vyeti vya ujuzi walionao waajiri wetu wengi wana angalia sana vyeti vya elimu au ujuzi ulionao bila hivo wachache sana wanachukua tahadhali ya kuajiri vijana ambao hawana vyeti.

NINI KIFANYIKE SASA ILI KUWEZA KUWASAIDIA HAWA VIJANA NA KUONGEZA MAENDELEO KATIKA TAIFA KWA MIAKA 5 IJAYO

Kuna njia kadhaa ambazo tunaweza kuwasaidia vijana waliohitimu kidato cha nne na kidato cha sita kujikwamua na ajira:

  • Mafunzo ya ufundi: Kuwapa mafunzo ya ufundi au stadi za kazi kunaweza kuwasaidia kupata ujuzi unaohitajika katika soko la ajira kwa mfano mafunzo ya ufundi umeme, ufundi uashi, ufundi na gereji nakadhalika.
  • Kuanzisha vyuo vya Sanaa sehemu mbalimbali nchini..Kuongeza vyuo vya Sanaa sehemu mbalimbali ndani ya nchi kama ambavyo serikali imejitahidi kufanya katika vyuo vya ufundi izingatie pia katika vyuo vya Sanaa viwepo sehemu tofauti mikoani hata na wilayani.chuo cha Sanaa Bagamoyo peke ake Akitoshi.itasaidia kuendeleza vipaji vya Sanaa vinavyohusiana na muziki,uigizaji,michezo ya kuigiza,uchoraji na kadhalika.pia vyuo vya Sanaa vitapaswa kutoa mafunzo kamili yanayojumuisha masomo ya nadharia na vitendo ili wanafunzi waweze kupata uelewa wa kina na pia hata kufanya vyuo hivyo viwe na tija iliyokusudiwa.
  • Mifumo ya Misaada ya Kifedha: Kutoa msaada wa kifedha au mikopo kwa vijana ili kusaidia kuanzisha biashara zao au kuendeleza mafunzo yao.Ianzishwe hata bodi ya mikopo kwa vijana ambao wameshindwa Kwenda chuo kikuu.kama ambavyo kuna bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu serikali inaweza kuangalia namna kuwezesha pia kua na bodi ya mikopo kwa vijana au wanafunzi wanaochukua Sanaa na mafunzo ya ufundi ili kuwezesha vijana wengi zaidi kupata mafunzo mbalimbali yatakayowawezesha kujiajiri na hata kusaidia kuongeza pato la taifa kwa namna moja au nyingine.
  • Ushauri na Msaada wa Kazi: Kuwapatia ushauri na mwongozo katika kutafuta kazi au kuunda biashara zao ni muhimu sana.
  • Vikundi vya Ujasiriamali: Kuwapa fursa ya kujiunga na vikundi vya ujasiriamali au kuunda vikundi vyao wenyewe kunaweza kuwasaidia kuanzisha biashara zao. Vikundi vya ujasiriamali ni muhimu sana katika kusaidia wajasiriamali kukua na kufanikiwa vikundi hivi huwakutanisha wajasiriamali Pamoja kubadilishana uzoefu maarifa na kuwasaidia kujenga mtandao wa kibiashara.
  • Kuboresha mfumo wa elimu; ni muhimu kurekebisha mfumo wa elimu ili kuhakikisha kwamba wahitimu wanapata ujuzi unaohitajika katika soko la ajira. mitaala mbalimbali inapaswa kuzingatia mahitaji ya sasa ya soko la ajira.
  • Kuongeza ushirikiano kati ya sekta ya elimu na sekta ya ajira; kuwa na ushirikiano wa karibu wa vyuo vikuu, taasisi za mafunzo ya ufundi na waajiri kunaweza kusaidia kuhakikisha kwamba mafunzo yanayotolewa yanalingana na mahitaji ya soko la ajira.
  • Kuongeza fursa za kujiajiri; kuongeza fursa za kujiajiri kwa vijana wenye elimu ya kidato cha nne na cha sita hapa Tanzania ni muhimu sana kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii hapa kuna hatua kadhaa serikali inaweza fanya ili kuhamasisha ujasiriamali katika miaka mitanoo ijayo ambazo ni ,kutoa elimu na mafunzo ya ujasiriamali,kutoa mikopo nafuu,kuwezesha upatikanaji wa masoko,kuwekeza katika miundombinu kama vile umeme na internet.kwa kuchukua hatua kama hizi na kuweka mkakati Madhubuti wa kuongeza fursa za kujiajiri kwa vijana serikali inaweza kusaidia Kuhamasisha Ujasiriamali na kukuza Uchumi wa nchi kwa ujumla .
  • Kuwekeza katika sekta inayokua haraka; Kukuza sekta kama vile, TEHAMA, nishati mbadala, kilimo cha kisasa, utalii na viwanda vya ndani kunaweza kutoa fursa nyingi za ajira hata kwa wenye elimu ya chini ya kidato cha sita na cha kidato cha nne.
  • Kuboresha Mazingira ya Biashara: Kupunguza urasimu, serikali inaweza kuchukua hatua za kupunguza urasimu na vizuizi vingne ambavyo vinaweza kuwakwamishwa hawa vijana pale wanapoanzisha biashara zao. kufanya taratibu za kuanzisha biashara ziwe rahisi na haraka. Na pia kuongeza upatikanaji wa mikopo kwa wajasiriamali.
  • Kuwekeza katika Uwezeshaji wa Teknolojia: Kukuza matumizi ya teknolojia katika sekta mbalimbali ili kuongeza ufanisi na kujenga fursa za ajira.vijana wanaweza pata mafunzo mbalimbali mtandaoni kulingana na maslahi yao na mahitaji ya soko la ajira kuna mitandao mingi inayotoa kozi za bure au za bei nafuu katika fani mbalimbali ,pia kwa upande mwingine teknolojia inawawezesha vijana kutafuta fursa za biashara mtandaoni kuanzisha tovuti au maduka ya mtandaoni na hata kukuza biashara zao kwa njia ya digital marketing.
Mikakati hii ikitekelezwa kwa ufanisi na kwa ushirikiano, inaweza kusaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana katika miaka mitano ijayo.
 
Upvote 6
Back
Top Bottom