SoC03 Njia za kuzuia mawazo hasi, na mawazo yanayokuumiza na yanayokunyima Amani ya Moyo

SoC03 Njia za kuzuia mawazo hasi, na mawazo yanayokuumiza na yanayokunyima Amani ya Moyo

Stories of Change - 2023 Competition

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2023
Posts
382
Reaction score
687
Kama mawazo hasi, mawazo ya kujiua, mawazo ya kujihisi mpweke, mawazo ya kukataliwa au mawazo yoyote yanayokufanya ukose amani ya moyo basi ujumbe huu unakufaa sana, ujitahidi ufanye hivi.

Kila mtu hupatwa na mawazo hasi kwa namna moja au nyingine katika muda tofauti.

… ila kinachojalisha zaidi ni, nini unafanya baada ya kupatwa na hayo mawazo hasi.

Yani usikubali yakuendeshe na ukakosa amani ya moyo. Pengine ukajikuta unafanya vitu ambavyo hukupanga kabisa kufanya.

Mawazo hayo yanaweza kutokana na matokeo uliyopata kwenye masomo, mwenendo wa biashara yako, hali ya mahusiano yako au maisha kiujumla yanakufanya unajikuta una mawazo ya kukuumiza zaidi.

Huwezi kukwepa hivyo vitu, labda ukiwa umefariki ndo njia pekee ya kuepukana na mawazo kama hayo.

Lakini ingali upo hai, lazima utakutana na changamoto mbalimbali kwenye maisha. Na hizo changamoto zinaweza kuwa chanzo kikubwa cha mawazo.

Kwaiyo cha kujiuliza sio namna ya kuepukana na changamoto, bali ni jinsi gani unaweza ukatumia changamoto hizo kukua zaidi.

Na ni jinsi gani unaweza kutumia mawazo mabaya yanayokupata kama motisha ya kusonga mbele zaidi badala ya kukubali yakuangushe.

Yaani kuwa na mawazo chanya, mawazo ya kukuinua, mawazo ya kukupa matumaini hata kama huoni tumaini lolote maishani.


Unawezaje kufanya hivyo sasa ili ufaidi faida za mawazo yenye matumaini kama vile kuwa na afya na amani badala ya kuangamia na mawazo mabaya?

Zingatia njia hizi tano;

1.
Kuwa karibu na watu wenye mawazo yenye matumaini.
Kumbuka, tunafanana tabia na watu tunaokaa nao sana.

Ukikaa na watu wenye matumaini, na wanao ongea ushindi na wewe utakua na mawazo ya ushindi, na mawazo yenye matumaini.

Kuna watu ukikaa nao, unaona kabisa hali ni mbaya na hakuna mwanga wa mambo kuwa mazuri.

Maneno yao hayakupi tumaini wala motisha yoyote ya kusonga mbele.
Achana na hao watu, usitumie muda wako mwingi pamoja nao.
mana watakufanya na wewe uwe na mawazo ya kufeli kama wao.

Lakini ukitumia muda wako mwingi na wanaowaza ushindi, we mwenyewe utaanza kuona mwanga pasipo na mwanga.

Ndo mana tukitoka nyumba za ibada tunatoka na tumaini jipya. Sababu tunafundishwa imani na kwamba Mungu anaweza kutushindia changamoto tunazopitia.

Ila tatizo linakuja baada ya kufika nyumbani na kuanza shughuli nyingine.

Tunachangamana na watu wengine wenye mawazo yasiyo na matumaini.
Na kupelekea yote tuliyofundishwa kupeperuka na kuyasahau.

Ndo mana ni muhimu kujitengenezea ukaribu na watu wenye mawazo ya matumaini, na kujitenga au kutumia muda mchache sana na watu wenye mawazo ya kufeli na kushindwa.

2.
Kuwa mtu wa shukrani.
Jikumbushe mazuri yote uliyojaaliwa.

Jitahidi uyaongoze mawazo yako kutoka kwenye vitu vinavyokuumiza kuelekea vitu vinavyokupa raha, amani na unavyoshuru unavyo.

Mara nyingi tukiwa tunapitia changamoto, tunasahau mema yote tuliyowahi kupata/ kuyapitia.

Na unajikuta unamawazo ya kulalamika kuhusu changamoto unayopitia, au jinsi ulivyofeli, au jinsi ambavyo hustahili au jinsi unavyoonewa au jinsi unavyoshindwa.

Hayo mawazo, ukichunguza vizuri hayakusaidii lolote. Yanakuumiza tu na kukunyima amani ya moyo.

Unajikuta hata hufurahii maisha. Hata vitu vidogo ulivyokua unafurahia zamani huvifurahii sasa.

Lakini ukibadili mtazamo, na kuanza kutazama kwamba, leo umejaaliwa umeamka salama, familia yako imeshiba, mmevaa tayari utajiona ni mshindi.

Na uendelee kuhesabu vyote ulivyojaaliwa na kushukuru kadri uwezavyo badala ya kulalamika kadri uwezavyo.

Pia angalia mazuri ya mwenzio, sio kila saa unaangalia mabaya yake na kumsema vibaya.

3.
Kubali ulipokosea.
Kwa kukubali ulipokosea unajipunguzia mzigo mkubwa wa mawazo, na unakua huru kubadilika.

… Kuliko uking’ang’ania kuonekana hujakosea.

Ukishajipa huo uhuru sasa anza kufanyia kazi, anza kuchukua hatua sahihi.

Hatua unazochukua sio lazima ziwe kwa ajili ya kufuta makosa. Hapana. Bali lazima hizo hatua ziwe za kukusaidia katika kutimiza malengo yako.

Hata kama ni kitu kidogo kama kuomba msamaha. Kina msaada wa kukuweka huru katika safari yako ya kufikia malengo yako.

Kitu kikubwa cha kuepuka ni lawama.
Usilaumu wengine, sababu hata wewe umechangia kwa kiasi fulani katika hayo makosa.

Kadri unavyolaumu, ndivyo unajikuta unarudi katika mawazo hasi, mawazo ya kushindwa na kufeli.

Badala yake kubali, samehe na usonge mbele.

4.
Epuka mawazo ya kujitakia.
Epuka drama maishani mwako.

Epuka kuingilia yasiyokuhusu au kutaka kuwafanyia maamuzi watu wengine.

Utajikuta katika hali ambazo hata wewe hukupanga kuwemo.

Ndo mana ni muhimu sana, kujitenga na watu ambao hawaeleweki, wana mambo mengi yasiyo na msingi.

Jiepushe na umbea usio na maana. Jiepushe na kuzungumzia mawazo ya watu wasiokuhusu.

Jiepushe na kuwasema watu vibaya. Mana najua hata wewe hutopenda kusemwa vibaya.

Usimfanyie mtu kitu ambacho hata wewe hutopenda kufanyiwa.

Kuna muda unamfanyia mtu kitu usichopendwa kufanyiwa kwa sababu umezoea tu, ni tabia yako imekua.

Anza sasa kujirekebisha tabia.

Utasema, lakini wanaonizunguka wananifanyia hivyo na wapo hivyo.

Ukweli ni kwamba hao wanaokuzunguka unafanana nao, ukijibadilisha na ukabadili wanaokuzunguka utasahau kabisa kuhusu hayo.
Rudia kusoma ile njia ya kwanza.

5.
Kuwa mkarimu kwa wengine.
Sio kwa sababu unapitia magumu ndio ukaripie wengine. Au uone wengine wanakuumiza zaidi.

Ukiwa mkarimu hata mawazo yako yanakua yamejaa ukarimu. Na utajikuta unasahau mawazo mabaya uliyonayo.

… na endapo yatakujia, sasa unajua njia za kuyabadili hayo mawazo na kuwa na mawazo mazuri.

Nikutakie Wiki Njema Ukiwa na Mawazo ya Ushindi!

Share Na Wengine Wapate Kujifunza.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom