payless marketplace
Member
- Aug 28, 2024
- 9
- 22
Njia za kuzuia wizi kwenye Biashara yako.
Wizi ni miongoni mwa vitu vyenye kurudisha sana nyuma Biashara zetu.
Kuweza kudhibiti wizi kwenye Biashara sio kazi nyepesi kabisa.
Lakini unatakiwa kupambana sana mpaka ukae sawa kwenye Biashara yako.
La sivyo wewe utateseka kisha wafanyakazi wako watanufaika sana.
Kuna wafanyakazi ni washenzi sana aiseee.
Kupitia hili andiko unaweza kupunguza wizi kwenye Biashara yako.
Tuanze mdogo mdogo.
1. Sifa Na Tabia Za Wezi Ambazo Unatakiwa Kuzifahamu.
Kwa mtu mwenye tabia za wizi ni rahisi sana kumtambua kama utaweza kutuliza kichwa.
Zisome hizi tabia kwa utulivu sana.
Tabia ya kwanza.
Mfanyakazi mwenye konekesheni kubwa mtaani.
Mfanyakazi anayeweza kuongea na kila mtu na kuweza kuanza mazungumzo kwa wepesi basi kuwa naye makini sana.
Wezi wana uwezo mkubwa sana wa kujichanganya na watu.
Tabia ya Pili.
Mtu mwenye tabia ya kufanya kazi sana.
Mara nyingi wafanyakazi wenye kujificha kwenye mtego wa kufanya kazi sana waangalie kwa makini.
Ufanyakazi nje ya kawaida kwa muda wa kazi na malipo pia.
Mpaka wewe mwenyewe unaogopa yaani.
Wengi hutumia mbinu ya kufanya kazi sana ili wasigundulike mapema.
Hata wakigundulika hupata msamaha kwa haraka.
Tabia ya tatu.
Kuwa karibu na viongozi.
Mfanyakazi mwenye tabia za kuwa karibu sana na Viongozi muangalie kwa jicho la pili.
Baadhi hutumia ukaribu na viongozi kufanya uhalifu wao bila kugundulika.
Tabia ya nne.
Mchunguzi wa mazingira.
Ukiona mtu anatabia ya kuchunguza udhaifu wa mazingira ya kazi kuwa naye makini.
Au mtu akiwa anaingia ofisini anakagua mazingira ya kazi na kuangalia bidhaa kuliko njia.
Kuwa naye makini.
Tabia ya tano..
Mwenye uwezo wa kupoteza ushahidi.
Ukiona una mfanyakazi mwenye tabia ya kupoteza taarifa za ofisi kuwa naye makini.
Zinawezekana zikawa ni taarifa ndogo sana.
Lakini ukichunguza kwa ukaribu utagundua kitu.
Ukiangalia kama anajitoa akili hivi.
Tabia ya sita.
Kulalamika sana.
Kuna wafanyakazi wana tabia ya kulalamika sana.
Ukiona mtu analalamika sana kuwa naye makini.
Tabia ya Saba.
Matumizi makubwa kuliko mshahara.
Ukiona una mfanyakazi matumizi yake ni makubwa kuliko kawaida basi kuwa makini sana.
Mara nyingi huwa wanafidia matumizi yao kwenye wizi.
Ila sio wote!
Tabia Ya Nane.
Hawana woga na wanajiamini kwenye harakati zao za kila siku.
Ukiona mfanyakazi anajiamini sana hana woga kuwa naye makini mno.
Tabia ya Tisa.
Kujifanya wajinga.
Kuna mfanyakazi ukiona ni kama mjinga hivi na unahisi kana kwamba hawezi kufanya matukio ya wizi.
Kuwa nao makini hawa.
Kwenye karate tunasema hivi
"Kuwa kama mlevi ili watu wakudharau"
Kisha fanya shambulio moja takatifu sana.
Hizo ni tabia za kuwa nazo makini kwenye Biashara yako.
Tuje kwenye jambo la pili.
Vitu Ambavyo Wezi Wanapenda Kuiba.
Wezi sio wajinga ni watu wenye akili zao timamu sana.
Mara nyingi wezi huiba vitu vyenya sifa hizi.
1. Vitu rahisi kuuzika.
Hapa pia inaingia pesa taslimu.
Mara nyingi wezi huwa hawaibi vitu vyenye thamani.
Bali wanaiba vitu vyenye kuweza kuuzika.
Anaweza kuacha kitu chenye thamani ya 1M na kuiba kitu chenye uwezo wa kuuza 200K.
Kuwa makini na vitu vyenye uwezo wa kuuzika kwa wepesi.
2. Vitu vyepesi kubebeka.
Mara nyingi wezi uangalia ni vitu gani rahisi kubebeka bila kuonekana.
Ambavyo anaweza kuweka kwenye mfuko au begi tu.
3. Vitu ambavyo si rahisi kushtukia.
Mara nyingi hivi vinakuwa ni vitu vidogo sana.
Au vitu vinavyokuwa ndani ya kitu..
Mfano ndani ya Box na Tv wanaweza kuiba rimoti.
Na vitu mfano wa hivyo.
So usipende kutoa vitu nusu nusu kwenye box.
4. Bidhaa adimu zenye thamani.
Kukiwa na bidhaa adimu au zenye thamani wezi pia hutolea macho.
So kuwa makini na bidhaa adimu sokoni.
Darasa litaendelea.
Nisave Pay Less.
0654208515