SoC01 Njia zinazoweza kutumiwa na Serikali kupata mapato badala ya kuwakamua Watanzania kwenye tozo

Stories of Change - 2021 Competition

chai ya moto

Member
Joined
Jul 27, 2021
Posts
25
Reaction score
72
Serikali zote Duniani ni lazima ziwe na vyanzo vya mapato vya uhakika vya kuendeshea Serikali mapato hayo ni muhimu kwa sababu ndiyo yanayojenga barabara,yanayonunua silaha,yanayonunua madawa na kulipa mishahara na posho watumishi wa umma na wanasisa.Hivi karibuni kumeibuka mjadala kuhusu makato yanayofanywa na Serikali kupitia miamala ya simu za mkononi,mapato hayo yanaumiza kwa sababu Watanzania wengi ni mafukara wa kutupwa.

Baada ya kelele mbalimbali tarehe 23 julai 2021 Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai aliibuka na kuwataka wale wote wanaopinga tozo hizo watoe njia mbadala ili serikali ipate fedha za maendeleo.

Hizi zifuatazo zinaweza kuwa njia mbadala za Serikali kupata fedha za maendeleo

Kuongeza wigo wa mapato

Katika nchi yetu watu wanaolipa kodi ni wachache sana ni watumishi wa umma na watumishi wa sekta binafsi pamoja na wafanyabiashara waliosajiliwa na mamlaka ya mapato Tanzania ndiyo wanaolipa kodi.Kuna watu wengi sana wanaopata mapato makubwa lakini hawalipi kodi.Kwenye kundi hili kuna madalali,mafundi ujenzi,mafundi seremala,wafugaji,wakulima,watangaza matangazo ya biashara kupitia mitandao ya kijamii na wafanyabiashara wanaotumia mitandao ya kijamii kufanya biashara.

Niliamua kuwahoji watu wafuatao ili nijue namna wanavyofanya biashara zao nilianza na Seif Salum mkazi wa Mabibo Dar es salaam, na mpaka rangi kucha yeye aliniambia anapata shilingi elfu 30 kila siku lakini halipi kodi ya aina yoyote,Jakob Mushi mfanyabiashara wa soko la Loliondo Kibaha ana mtaji wa zaidi ya milioni sita akiwa anauza nafaka lakini halipi kodi zaidi ya ushuru wa soko shilingi 500 kwa siku.Joseph Kasongu dalali mashuhuri wa nyumba,viwanja na mashamba mkazi wa Maili moja Kibaha ana miliki basi dogo,amejenga na anasomesha kutokana na kazi yake ya udalali lakini halipi kodi ya aina yoyote.Mifano ya aina hii ni mingi sana na ipo kila kona ya Tanzania. Kinachotakiwa Serikali isajili Watanzania wote wanaostahili kulipa kupitia mtandao wa vitambulisho vya taifa na kuwapa namba za mlipa kodi waanze kulipa kodi.Kinachotakiwa nI kuwapangia kodi inayolipika kutegemea na vipato vyao na kwa utaratibu rafiki utakaowezesha watu walipe kodi bila kukimbizana.

Utalii

Tanzania ina vivutio vya kila aina kuliko nchi nyingi Duniani lakini kwa mwaka inapokea watalii wachache sana,mwaka 2016 ilipokea Watalii milioni 1.2,mwaka 2017 ilipokea Watalii milioni 1.3 na mwaka 2019 ilipokea Watalii milioni 1.5 wakati Tunisia mwaka 2019 ilipokea Watalii milioni 9.4 na kama isingekuwa ugonjwa wa UVIKO 19 mwaka 2020 wangeweza kuvunja rekodi ya kupokea Watalii milioni 10. Sera nzuri,huduma bora,mikakati mizuri pamoja na kutangaza vivutio vyao ndiyo siri ya kupokea Watalii wengi hakuna uchawi wala miujiza.Kwenye kutangaza Utalii tunashindwa hata na Rwanda inayotumia fedha nyingi kutangaza utalii kupitia michezo hasa kupitia vilabu mashuhuri vya soka Duniani vya Arsenal ya Uingereza na na PSG ya Ufaransa,leo hii mchezaji mashuhuri Dunani wa soka Lionel Messi anavaa jezi iliyoandikwa "tembelea Rwanda" sisi tumebaki tumebung'aa.Rwanda mwaka 2019 walipokea Watalii milioni 1.6 .Nchi ndogo isiyo na vivutio vingi inapokea idadi ya Watalii inayofanana na Tanzania!

Idadi kubwa ya Watalii ndiyo wingi wa fedha wanazoleta ni wakati wa Serikali na wadau wa utalii kujipanga na kutatua kero zinazowapata Watalii wakitembelea Tanzania pamoja na kutangaza kwa nguvu utalii wetu ili tupate fedha nyingi na kuachana na kuwabinya Watanzania kwenye tozo mbalimbali.

Rasilimali zilizopo chini ya ardhi

Kwenye ardhi ya Tanzania kuna gesi za aina mbalimbali na madini ya kila aina lakini rasilimali hizo bado hazijalinufaisha taifa kwa kiwango kikubwa.Kuna madini mengi bado hayajachimbwa.Mwaka 2013 niliwahi kutembelea machimbo ya madini ya rubi ya Ngembambili na Masuguru Wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma ambayo yanachimbwa na wachimbaji wadogo wadogo ambao hawana vifaa ,ujuzi na tekinolojia inayotakiwa kwenye uchimbaji,wanachokifanya ni kuchimba juu juu na kuhamia sehemu nyingine.Pale wanapohama wanakuwa wameacha madini ambayo yanakuwa chini sana na hawawezi kuyafikia kutokana na kuwa na zana duni,kutokuwa na ujuzi na kukosa tekinolojia ya uchimbaji .Machimbo ya aina hii ni mingi sana inachotakiwa Serikali ishirikiane na wadau kufanya utafiti kwenye machimbo kama haya na kuwezesha madini yachimbwe ili fedha zipatikane za kujenga barabara,kulipa posho na mishahara Watumishi na Wanasiasa,kujenga madaraja na matumizi mengine muhimu ya Serikali.

Pia kuna sehemu nyigi za nchi ambako kuna rasilimali chini ya ardhi lakini bado hazijagundulika mfano kampuni ya Helium one mwaka 2016 iligundua gesi ya Helium mkoani Rukwa yenye ujazo wa futi za ujazo bilioni 98.9 za gesi hiyo muhimu na hadimu Duniani imeifanya Tanzania kuwa na hifadhi kubwa zaidi ya gesi hiyo Duniani.Kwa ugunduzi huo wa gesi ya Helium kuna uwezekano mkubwa wa Tanzania kuwa na gesi nyingine na madini mbalimbali ambayo hayagundulika au hayajaanza kuchimbwa kwahiyo Serikali ishirikiane na wadau kufanya utafiti na kukiwepo madini au gesi washirikiane na wawekezji kwa kumiliki hisa na uwekezaji wa aina hiyo siyo mgeni Tanzania kwani kwenye mgodi wa makaa ya mawe wa Ngaka uliopo Mbinga Ruvuma kampuni ya Intra energy inamiliki asilimia 70 na Serikali ya Tanzania kupitia kampuni ya Tancoal iliyo chini ya Shirika la maendeleo la Taifa inamiliki asilimia 30.

Rasilimali zilizopo chini ya ardhi kama zikichimbwa kwa kutumia sera nzuri,mikakati bora na kutanguliza uzalendo zinaweza kuipaisha nchi hii kiuchumi na Watanzania wakanufaika kwa rasilimali hizo kama ilivyo kwa nchi ya Botswana ambao uchumi wao wanategemea almasi ambayo inachangia asilimia 50 ya mapato ya Serikali.Botswana imefanikia sana kwenye madini kwa sababu ya ubia wa 50 kwa 50 na makiampuni yanayochimba almasi nchini humo.

Pamoja na vyanzo nilivyo orodhesha pia Watumishi wa umma walioajiriwa kwa kazi hiyo wasumbue vichwa vyao kutafuta vyanzo vya mapato na kuboresha vilivyopo badala ya kuhangaika na tozo za miamala ya simu.
 
Upvote 12
Sawa wazo lako ni zuri lakini approach yako ya kutaja watu majina sio njema, Sidhani kama kabla hujawauliza uliwaambia utawataja majina kwenye media na wakakubali kukupa ushirikiano! Kumtaja mtu jina kwenye media bila ridhaa yake kisheria ni kosa!

Kama lengo ni kuonyesha mianya mapato, un aweza kuionyesha bila kutaja mtu jina na wenye mamlaka wakalifanyia kazi wazo lako!

Pia suala utalii, tatizo ni mazingira ya miundombinu! Hebu niambie ni mtalii gani mjinga atakubali kurudi tena baada ya kumpitisha kwenye zile barabara za makorongo ya Mrisho Gambo kule Arusha, alafu watu wanafichua uoza ule wanashukiwa!

Pia suala la kilimo tatizo lake ni thamani ya mazao ya kilimo, Hebu nenda mikoa ya nyanda za juu ujionee wakulima na wafanya biashara wa mahindi yalivyowadodea, hayana soko, hayana faida na hapohapo umekopeshwa pembejeo, msimu wa marejesho umeshafika lakini bei bado ni ya kufilisi na wateja ni wa kutafta kwa tochi, Je nani atakuwa na hamu na kilimo! Hata juzi tumemsikia Katibu mkuu wa CCM akijaribu kuitaka serikali kununua mahind ya wakulima ni sababu bidhaa hiyo imedorora masokoni!

Wazo la Tanzania kuinvest kwenye viwanda lilikuwa zuri sema shida, likabakia kuwa sera ya mtu mmoja! Ni lazima tufahamu kuwa Wazungu huwa hawapendi nchi za dunia ya 3 zifanye mapinduzi kwenye eneo la viwanda, tukija kujitutumua kufanikiwa hapo tutafika mbali kiuchumi tofauti na sasa ambapo serikali kuu inategemea tozo, huku zile serikali za mitaa zikitegemea mapato ya faini wanazotoza wananchi kwa makosa mbalimbali yakiwemo uchafuzi wa mazingira badala ya kuwaelimisha kuacha vitendo hivyo!
 
Hi

Hizo changamoto za kwenye utalii ndiyo wahusika wakae wazitatue,wadau wote wa utalii ikiwemo serikali.Tuige wenzetu wanafanikiwa vipi kupokea watalii wengi mfano Tunisia na sisi tufanye kama wao au tuboreshe zaidi yao.

Kilimo pia Kama viongozi wangekuwa na nia kilimo ndicho kitu ambacho kingewatoa Watanzania wengi kwenye umasikini.Nchi hii kila zao linastawi lakini tunajiwekea vikwazo wenyewe mf.kuzuia mara kwa mara kupelekea mahindi Kenya inafika kipindi na wao wanachoka wanaagiza mahindi Brazil,bado nje ya nchi Kama DRC ,Sudan Kusini kuna soko kubwa la mahindi ni jukumu la wizara ya Viwanda na biashara kutafuta soko nje ya nchi.
 
Sawa wazo lako ni zuri lakini approach yako ya kutaja watu majina sio njema, Sidhani kama kabla hujawauliza uliwaambia utawataja majina kwenye media na wakakubali kukupa ushirikiano! Kumtaja mtu jina kwenye media bila ridhaa yake kisheria ni kosa!
Kama lengo ni kuonyesha mianya mapato, un aweza kuionyesha bila kutaja mtu jina na wenye mamlaka wakalifanyia kazi wazo lako!
Pia suala utalii, tatizo ni mazingira ya miundombinu! Hebu niambie ni mtalii gani mjinga atakubali kurudi tena baada ya kumpitisha kwenye zile barabara za makorongo ya Mrisho Gambo kule Arusha, alafu watu wanafichua uoza ule wanashukiwa!
Pia suala la kilimo tatizo lake ni thamani ya mazao ya kilimo, Hebu nenda mikoa ya nyanda za juu ujionee wakulima na wafanya biashara wa mahindi yalivyowadodea, hayana soko, hayana faida na hapohapo umekopeshwa pembejeo, msimu wa marejesho umeshafika lakini bei bado ni ya kufilisi na wateja ni wa kutafta kwa tochi, Je nani atakuwa na hamu na kilimo! Hata juzi tumemsikia Katibu mkuu wa CCM akijaribu kuitaka serikali kununua mahind ya wakulima ni sababu bidhaa hiyo imedorora masokoni!
Wazo la Tanzania kuinvest kwenye viwanda lilikuwa zuri sema shida, likabakia kuwa sera ya mtu mmoja! Ni lazima tufahamu kuwa Wazungu huwa hawapendi nchi za dunia ya 3 zifanye mapinduzi kwenye eneo la viwanda, tukija kujitutumua kufanikiwa hapo tutafika mbali kiuchumi tofauti na sasa ambapo serikali kuu inategemea tozo, huku zile serikali za mitaa zikitegemea mapato ya faini wanazotoza wananchi kwa makosa mbalimbali yakiwemo uchafuzi wa mazingira badala ya kuwaelimisha kuacha vitendo hivyo!
Wote waliohojiwa walikubali kutajwa majina na walitoa ushirikiano wa kutosha.
 
Vijana wasio na ajira ni wengi sana
Waajiriwe kama Special Task Force
Sheria kwny kipengele cha Makadirio kiboreshwe

Kila mwananchi anavyopata NIDA ID apate na TIN..iwe lazima sio ombi
Kodi ni lazima

tujifunze kwa nchi zingine
Asante kwa mchango wako mzuri.
 
Binafsi nadhani ili tujikwamue hapa tulipo tusonge mbele
NI LAZIMA TUIONDOE CCM MARAKANI
Kwanini nasema hivyo..

CCM ndio chama kilichopo madarakani tangu tupate uhuru na hawana nia ya kuondoa umasikini kwa watanzania
Wanatumia kila njia watanzania waendelee kuwa masikini na wajinga ili waendelee kuwatawala.
Tukianza na kilimo
Serikali ya CCM imevuruga na kuharibu miundombinu na masoko ya mazao kuanzia mahindi ( walifunga mipaka watu wasipeleke Kenya bila sababu ya msingi), tumbaku,mbaazi (walimkamata Manji) pamba, kahawa wakamalizia na korosho kwa kupeleka jeshi na kukamata watu kudhulumu na kuharibu soko lao
Mnadhani yote haya yanafanywa kwa bahati mbaya?

Elimu
Wamesema elimu ni bure na hakuna kuchangisha wazazi sasa nenda kwenye shule za kata uone maajabu shule moja ina walimu wawili au watatu, hakuna walimu wa sayansi, madawati,hakuna vyumba vya madarasa vya kutosha na serikali haijaajiri walimu tangu 2015 licha ya kuongezeka kwa udahili wa wanafunzi na kustaafu kwa walimu waliopo.
lengo ni kuzalisha wajinga wasioweza kuhoji na kuipinga serikali
Watoto wao hawasomi huko

Mindombinu
Katika hali ya kawaida unawezaje kununua ndege tena cash kwa matrilioni ya pesa wakati wananchi hawana maji?
Hizo pesa zingeelekezwa kwenye uchimbaji wa chuma Liganga tungeingiza fedha kiasi gani?
Hizo fedha zingewekwa kwenye miradi ya maji kila nyumba ikafungwa mita ya maji serikali ingekusanya pesa kiasi gani?
Na watu wangenufaika kwa kupata maji safi na salama hasa ukizingatia karibu 60% ya magonjwa hutokana na maji yasiyo salama.

Tunajenga reli ya mwendokasi kwa trillion 7
Hivi trillion 7 tungezielekeza kwenye kufufua viwanda vyetu vya nguo, matairi, mkonge, samaki, ngozi nk wakulima wetu wangehangaika kutafuta masoko?
Hivi trillion 7 tungeamua kupanua bandari ya Dar ikawa ya kisasa kabisa na meli zikaacha kupanga foleni pia meli kubwa zinazoishia Dubai zikaja Tanzania isingewezekana?

Nishati na Madini
Tujiulize ile gesi ya mtwara imetunufaisha kwa kiasi gani?
Kwanini tunajenga bwawa la umeme kwa gharama kubwa na gesi ipo?
Kwanini mikataba ya gesi imegubikwa na usiri mkubwa sana why?

Michezo
Kuna fursa kubwa sana ya serikali kupata fedha kupitia michezo lakini ni lazima uwekeze ndipo upate.
Mfano; fedha ambazo serikali imetumia kununua ndege na kuwalipa wabunge hewa 19 ukizichanganya unaweza kujega Uwanja mkubwa na wakisasa wa mpira wa miguu(kuliko huu wa Taifa Dsm) kila mkoa Tanzania.
Kwa kufanya hivyo kwanza tungevutia mashindano mengi kufanyikia Tanzania hivyo tungepata fedha na kutangaza nchi yetu na vivutio vyake kwa wakati mmoja
Serikali ingekusanya fedha nyingi za mashindano mbali mbali ya ndani
Pia ingetoa hamasa kwa watu wengi mijini kufanya mazoezi na kuimarisha afya zao.
Hivi ni kweli hawaoni?

Afya
Hospitali ya rufaa ya kanda inajengwa Chato yenye watu laki 4 watu wanapiga makofi wakati Mwanza yenye watu milioni 4 haina hospitali ya rufaa ya serikali.
Lakini pia Mwanza ni Centre kwa kanda ya ziwa kuliko mtu atoke Mkoa wa Mara aende Chato ingekuwa rahisi kwenda Mwanza.

Spika anaposimama na kudai tumpe njia mbadala za kupata fedha za miradi ya maji anadhalilisha bunge na Watanzania
Anatuambia kwamba ameshindwa kazi iliyompeleka bungeni
Ni vyema angeiuzulu apishe wanaoweza kuliongoza bunge na kutatua changamoto za watazania.
 
NI LAZIMA TUIONDOE CCM MARAKAKANI

Wamesema elimu ni bure na hakuna kuchangisha wazazi sasa nenda kwenye shule za kata uone maajabu shule moja ina walimu wawili au watatu, hakuna walimu wa sayansi, madawati,hakuna vyumba vya madarasa vya kutosha na serikali haijaajiri walimu tangu 2015 licha ya kuongezeka kwa udahili wa wanafunzi na kustaafu kwa walimu waliopo
lengo ni kuzalisha wajinga wasiweza kuhoji na kupinga serikali
Watoto wao hawasomi huko

Mindombinu
Katika hali ya kawaida unawezaje kununua ndege tena cash kwa matrilioni ya pesa wakati wananchi hawana maji?
Hizo pesa zingeelekezwa kwenye uchimbaji wa chuma Liganga tungeingiza fedha kiasi gani?
Hizo fedha zingewekwa kwenye miradi ya maji kila nyumba ikafungwa mita ya maji serikali ingekusanya pesa kiasi gani?
Na watu wangenufaika kwa kupata maji safi na salama hasa ukizingatia karibu 60% ya magonjwa hutokana na maji yasiyo salama.
Tunajenga reli ya mwendokasi kwa trillion 7
Hivi trillion 7 tungezielekeza kwenye kufufua viwanda vyetu vya nguo, matairi, mkonge, samaki, ngozi nk wakulima wetu wangehangaika kutafuta masoko?
Hivi trillion 7 tungeamua kupanua bandari ya Dar ikawa ya kisasa kabisa na meli zikaacha kupanga foleni pia meli kubwa zinazoishia Dubai zikaja Tanzania isingwezekana?

Nishati na Madini
Tujiulize ile gesi ya mtwara imetunufaisha kwa kiasi gani
Kwanini tunajenga bwawa la umeme kwa gharama kubwa na gesi ipo?
Kwanini mikataba ya gesi imegubikwa na usiri mkubwa sana why?

Michezo
Kuna fursa kubwa sana ya serikali kupata fedha kupitia michezo lakini ni lazima uwekeze ndipo upate
Mfano fedha ambazo serikali imetumia kununua ndege na kuwalipa wabunge hewa 19 ukizichanganya unaweza kujega Uwanja mkubwa na wakisasa wa mpira wa miguu(kuliko huu wa Taifa Dsm) kila mkoa Tanzania.
Kwa kufanya hivyo kwanza tungevutia mashindano mengi kufanyikia Tanzania hivyo tungepata fedha na kutangaza nchi yetu na vivutio vyake kwa wakati mmoja
Serikali ingekusanya fedha nyingi za mashindano mbali mbali ya ndani
Pia ingetoa hamasa kwa watu wengi mijini kufanya mazoezi na kuimarisha afya zao.
Hivi ni kweli hawaoni?

Afya
Hospitali ya rufaa ya kanda inajengwa Chato yenye watu laki 4 watu wanapiga makofi wakati Mwanza yenye watu milioni 4 haina hospitali ya rufaa ya serikali.
Lakini pia Mwanza ni Centre kwa kanda ya ziwa kuliko mtu atoke Mkoa wa Mara aende Chato ingekuwa rahisi kwenda Mwanza.

Spika anaposimama na kudai tumpe njia mbadala za kupata fedha za miradi ya maji anadhalilisha bunge na Watanzania
Anatuambia kwamba ameshindwa kazi iliyompeleka bungeni
Ni vyema angeiuzulu apishe wanaoweza kuliongoza bunge na kutatua changamoto za watazania.
Mchango mzuri
 
Mchango mzuri sana.

Back
Top Bottom