Njombe: Aliyeshtakiwa kwa kuwabaka Wanawake kwa zamu na kuwaingizia matango sehemu za siri ahukumiwa miaka 180 jela

Njombe: Aliyeshtakiwa kwa kuwabaka Wanawake kwa zamu na kuwaingizia matango sehemu za siri ahukumiwa miaka 180 jela

Ataishi jela miaka 20.. Miaka jela unaishi 2/3 ya muda uliohukumiwa. Vifungo 6 vya miaka 30 vinaenda pamoja do ni miaka 30 na kwa kuwa unatumikia 2/3 maana yake ni atakaa jela kwa miaka 20
Ah kumbe ndiyo ipo ivyo
Nilikuwa najiuliza atawalipa vipi wakati anaweza fia huko gerezani?
 
Kwahio hapo kila kosa ni miaka 30? na anatumikia kwa pamoja, kwaufupi 6 IN 1, means atakaa ndani miaka 30? Naomba nirekebishwe kama sivyo.
Halafu huyo mganga anaachwajee?
Kwa kuwa inaenda sambamba, atatumikia miaka 30.Lakini sababu jela unatumikia 2/3 basi ataishi jela miaka 20
 
Huwa wana maana gani hawa mahakimu/majaji

Kwa maisha ya jela nani anaweza kukaa muda huo jela

USSR
20240822_185759.jpg
 
Hizi hukumu sio Bongo tu zipo nchi nyingi tu achanani na mambo ni Tanzania pekee blah blah blah.
 
Mtoa mada jaribu kujifunza haya mambo kabla ya kuonyesha ujinga wako hadharani...

Hizi hukumu zipo sana nchi nyingi hasa Jumuiya ya Madola (Commonwealth) na USA..
 
Kifungo cha juu Tanzania ni miaka 30!! Huyu alikua obviously na makosa zaidi ya moja so atatumikia 30yrs only
 
Elezea kidogo mkuu
Ukiwa na makosa zaidi ya moja wanaangalia lenye muda mrefu zaidi.

Mfano kubaka 30
Wizi 15
Kujeruhi 7
Kulawiti 30
Hapo ykijumlisha ni 72yrs lakini unatumikia adhabu zote kwa pamoja.

Ndo maana mtu aliyefungwa miaka 3621 anaweza kutoka jera lakini aliyefungwa maisha hawezi
 
Ukiwa na makosa zaidi ya moja wanaangalia lenye muda mrefu zaidi.

Mfano kubaka 30
Wizi 15
Kujeruhi 7
Kulawiti 30
Hapo ykijumlisha ni 72yrs lakini unatumikia adhabu zote kwa pamoja.

Ndo maana mtu aliyefungwa miaka 3621 anaweza kutoka jera lakini aliyefungwa maisha hawezi

Si mpaka itamkwe kama inakwenda pamoja ndugu?

Zingine huwa moja baada ya nyingine.
 
Mahakama ya Wilaya ya Njombe imemhukumu Juma Msemwa (27) na Mkazi wa Njombe, kutumikia kifungo cha miaka 180 jela kwa Makosa 6 ya ulawiti na ubakaji, ambapo kila kosa anatakiwa kwa miaka 30.

Akisoma hukumu ya kesi hiyo namba 53 ya Mwaka 2023, Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Njombe Matilda Kayombo, amesema mshtakiwa amekutwa na hatia katika makosa sita, matatu yakiwa ni ubakaji na matatu yakiwa ni makosa ya ulawiti anayodaiwa kutenda Mei 16 hadi 23, 2023 katika Mtaa wa Kihesa Kilimani Mkoani Njombe.

Hakimu Matilda ameeleza kwa mahakama imemtia hatiani baada ya kusikiliza ushahidi uliotolewa na mashahidi saba, wakiwemo waathirika wa matukio, Taarifa ya uchunguzi wa Daktari, uongozi wa Serikali ya Mtaa pamoja na Jeshi la Polisi.

Juma Msemwa anadaiwa kutenda makosa hayo kwa nyakati tofauti, baada ya kuwahadaa Wanawake watatu na kisha kuwafungia katika nyumba aliyokuwa anaishi katika Mtaa wa Kihesa, kisha kuwalawiti na kuwabaka kwa zamu usiku na mchana, zoezi lililoenda sambamba na kuwaingiza magunzi ya mahindi na matango katika sehemu za siri.


Taarifa zilizosaidia kukamatwa kwake zinaelezwa na mahakama kuwa zilitolewa na mmoja kati ya wanawake aliokuwa amewateka, ambaye alifanikiwa kutoroka na kupiga yowe kwa majirani ambao walivamia nyumbani kwa Juma na kukuta Wanawake wengine wawili wakiwa ndani.

Aidha, vilevile kulikutwa mfuko ukiwa na dawa za kienyeji, huku mahakama ikieleza kuwa sehemu ya ushahidi uliotolewa ulibainisha mtuhumiwa baada ya kuhojiwa alikiri kwamba alifanya matukio hayo akiwa anatekeleza maagizo ya mganga aliyemtaka abake Wanawake na Watoto.

Waendesha mashtaka wakiongozwa na Magdalena Whelo na Elicy James waliiomba mahakama kutoa hukumu kali kwa mtuhumiwa ili iwe funzo kwa jamii yote ikizingatiwa kwamba matukio ya ubakaji na ulawiti yamekuwa yakiongezeka Mkoani Njombe.

Mahakama imeeleza baada kujiridhisha na ushahidi uliotolewa imemhukumu Juma Msemwa kutumikia miaka 30 jela kwa kila kosa, katika makosa yote sita yaliyomtia hatiani, ambayo ni kinyume na kifungu cha sheria namba 130 kifungu kidogo cha kwanza na cha pili (e) sambamba na kifungu kidogo cha kwanza cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu Kifungu namba 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2022.

Hata hivyo pia adhabu hiyo ya kifungo imekwenda sambamba adhabu ya faini ambapo Juma Msemwa anatakiwa kulipa fidia ya fedha kiasi cha Shilingi Milioni moja, kwa kila muathirika wa makosa aliyoyafanya.
Nilijua tu, huyo hakimu lazima ni mwanamke, miaka 180 ndio nini sasa?
 
Back
Top Bottom