NJOMBE: Amuua mumewe kwa kumpiga na chuma kichwani

online GOVT applications

Senior Member
Joined
Sep 7, 2026
Posts
185
Reaction score
182
Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe linamshikilia Betrice Kalawa (45), mkazi wa Kijiji cha Malangali wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe kwa tuhuma za kumuua mume wake, Peter Mbunduzi (55) kwa kumpiga na chuma kichwani.

Hayo yameelezwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Kamishna Msaidizi wa Polisi Mahamoud Banga wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake

Amesema jeshi la polisi linamshikilia mwanamke huyo kutokana na mazingira ya tukio hilo, ikiwemo aina ya chuma kinachodaiwa kutumika katika kumpiga marehemu.

Banga amesema chuma hicho ni kile kilichokuwa kikitumika kufunga mlango kwa ndani, jambo ambalo limeibua shaka na kupelekea polisi kumshikilia mke wa marehemu wakati uchunguzi ukiendelea.

“Sasa shaka hilo ambalo tunalo tunaendelea na uchunguzi kama itathibitika kwamba amehusika na tukio hilo, basi atafikishwa mahakamani,” amesema Banga.

Ameeleza kuwa wakati wa tukio hilo, marehemu alikuwa akiishi pamoja na mke wake ambaye ni mtuhumiwa pamoja na watoto wao wawili wa kike wenye umri wa miaka 12 na 10 ambao nao wamehojiwa.
 
Attachments

  • 1788946339234.jpg
    1788946339234.jpg
    105.4 KB · Views: 17
Everytime am thinking of getting back to relationships, is like God sends me a message not to. 😂
 
Raia siku hizi mayai sana,muda wote wanatafuta mtu wa kumfia akaozee jela.
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe linamshikilia Betrice Kalawa (45), mkazi wa Kijiji cha Malangali wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe kwa tuhuma za kumuua mume wake, Peter Mbunduzi (55) kwa kumpiga na chuma kichwani.

Hayo yameelezwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Kamishna Msaidizi wa Polisi Mahamoud Banga wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake

Amesema jeshi la polisi linamshikilia mwanamke huyo kutokana na mazingira ya tukio hilo, ikiwemo aina ya chuma kinachodaiwa kutumika katika kumpiga marehemu.

Banga amesema chuma hicho ni kile kilichokuwa kikitumika kufunga mlango kwa ndani, jambo ambalo limeibua shaka na kupelekea polisi kumshikilia mke wa marehemu wakati uchunguzi ukiendelea.

“Sasa shaka hilo ambalo tunalo tunaendelea na uchunguzi kama itathibitika kwamba amehusika na tukio hilo, basi atafikishwa mahakamani,” amesema Banga.

Ameeleza kuwa wakati wa tukio hilo, marehemu alikuwa akiishi pamoja na mke wake ambaye ni mtuhumiwa pamoja na watoto wao wawili wa kike wenye umri wa miaka 12 na 10 ambao nao wamehojiwa.
Hii laana ya kuua ililetwa na polisi siku ya mauaji ya halaiki ya MO29. Inahitajika toba ya kweli kutoka kwa watawala ili nchi ipate kupona. Vingenevyo, hii laana ya mauaji itaendelea kuiandama nchi hadi kiama.
 
Sa100 kasababisha wanawake wenzake wawe na roho mbaya kwa sabavu yeye mwenyewe ni chura kiziwi
 
Back
Top Bottom