NJOMBE: Amuua mumewe kwa kumpiga na chuma kichwani

NJOMBE: Amuua mumewe kwa kumpiga na chuma kichwani

Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe linamshikilia Betrice Kalawa (45), mkazi wa Kijiji cha Malangali wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe kwa tuhuma za kumuua mume wake, Peter Mbunduzi (55) kwa kumpiga na chuma kichwani.

Hayo yameelezwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Kamishna Msaidizi wa Polisi Mahamoud Banga wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake

Amesema jeshi la polisi linamshikilia mwanamke huyo kutokana na mazingira ya tukio hilo, ikiwemo aina ya chuma kinachodaiwa kutumika katika kumpiga marehemu.

Banga amesema chuma hicho ni kile kilichokuwa kikitumika kufunga mlango kwa ndani, jambo ambalo limeibua shaka na kupelekea polisi kumshikilia mke wa marehemu wakati uchunguzi ukiendelea.

“Sasa shaka hilo ambalo tunalo tunaendelea na uchunguzi kama itathibitika kwamba amehusika na tukio hilo, basi atafikishwa mahakamani,” amesema Banga.

Ameeleza kuwa wakati wa tukio hilo, marehemu alikuwa akiishi pamoja na mke wake ambaye ni mtuhumiwa pamoja na watoto wao wawili wa kike wenye umri wa miaka 12 na 10 ambao nao wamehojiwa.
"Sumu ya mapenzi ni maudhi"

Kataa Ndoa 3 - Wataka ndoa 0
 
Mzee dogo wa miaka 12 kama ni mwanae wa kwanza kampata akiwa 43
Alikua Senior bachelor kabisa alaf akasaliti chama
Tatizo linaanza hapa, Hana uzoefu wa Kuishi nao, yeye anatumia maguvu.

Wanaume wananyanyasa Sana wanawake hasa huko vijijini.
 
Back
Top Bottom