Njombe: Ashikiliwa na polisi kwa kumuua mtoto wa miaka saba akidhani ni ng'ombe

Njombe: Ashikiliwa na polisi kwa kumuua mtoto wa miaka saba akidhani ni ng'ombe

Habari haijakamilika.
Kijana alilala wapi, nyumba moja na shangazi au nyumba nyingine? Je, kama ni nyumba nyingine na aliyolala shangazi mtoto aliingiaje endapo mlango ulifungwa??
Shangazi akapimwe akili kwanza!
Naongezea, shangazi wakati anampiga huyo ng'ombe (mtoto) hakutoa sauti ya vilio?

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe linamshikilia Mwanamke mmoja aitwaye Estaroda Kaduma (28) amkazi wa Kichiwa kwa tuhuma za kumuua Mtoto wa Kaka yake anayefahamika kwa jina la Brown James Kaduma (7) ambaye anasoma darasa la kwanza katika Shule ya msingi Kichiwa.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Hamis Issah amesema Kijana huyo alikuwa amelala majira ya saa nane usiku wakati Shangazi yake akiwa anafanya maombi lakini cha kushangaza alianza kupambana kwa kumpiga Mtoto akidhani ni ng’ombe mkubwa mweusi aliyefika wakati akifanya maombi.

“Huyu Dada huwa ana tabia ya kufanya maombi na katika maombi yake akaona ng’ombe mkubwa mweusi amefika katika eneo ambalo anafanya maombi, akaacha maombi akaanza kumpiga huyo ng’ombe na baadaye akatoweka baada ya muda akaonekana amefariki Kijana mdogo Mtoto wa Kaka yake baada ya kukanyagwakanyagwa kichwani na kujeruhiwa sehemu nyingine za mwili”

Kamanda Issah amesema tukio hilo linahusishwa na imani za kishirikina na kutoa wito kwa Wananchi kuachana na imani hizo ambazo zimekuwa zikileta madhara makubwa kwenye jamii.
R.I.P Brown James Kaduma
 
Kumbe ni Njombe!
Hata sishangai
[emoji84]
 
Njombe amekusuduia pana mauaji ya watoto sana huko wasitupakie rangi...
 
Amesema ameona ng'ombe mkubwa mweusi je mtoto wa miaka 7 anakuwaje na mwili mkubwa kama ng'ombe?
Na wakati kikawaida mtoto mdogo wa miaka 7 anakuwa na kamwili kadogo na kafupi?

Kuna kitu hakipo sawa either huyo mwanamke ana matatizo ya akili au ameua kwa kukusudia.
 
Wagonjwa wa akili ni wengi nchini.Hii taaluma ingaliwe kwa mapana.Wengi wanaamini wanaamini mapepo ni dalili ya magonjwa ya akili.wachunguzwe.
 
Kuna mengi ya kufanyia uchunguzi wa kina ili ukweli ujulikane badala yakujificha kwenye kivuli cha maombi.
 
Bado ni
utata ,je mtoto huyo alilala na Nani?





Usiku wa manane mtu unaomba unaomba kimwili au kiroho?
Hadi unahisi Ng'ombe binadamu inamaana hakuwa na macho yakiroho?

"Pumuzika kwa Amani mtoto wetu mpendwa"
 
Back
Top Bottom