Feisal2020
JF-Expert Member
- Nov 15, 2018
- 1,337
- 3,436
Familia aliichukulia mbususu serious sana
Huu ni uwongo sasa, hii si ni "Headphone," huyo Erasto yu wapi?Erasto Raphaely Kabupa (50) mkazi wa kijiji cha Igelehedza kata ya Ilembula wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe amedaiwa kufariki Dunia wakati akishiriki tendo la ndoa na mke wa mtu katika nyumba ya kulala wageni. Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Njombe Mahamoud Banga amethibitisha taarifa za kifo hicho ambapo amesema mnamo June 8,2025 majira saa mbili usiku,Erasto (marehemu) alikuwa na mwanamke ambaye jina lake limehifadhiwa katika nyuma ya kulala wageni na wakati wakiendelea na tendo alizidiwa ghafla na kukimbizwa kituo cha afya Ilembula lakini alifikishwa akiwa tayari amepoteza maisha.
“Baada ya kufikishwa hospitali alitambulika amefariki dunia lakini awali alifika na mwanamke kwenye gesti inayoitwa Mwendavanu kwa lengo la kushiriki tendo la ndoa na kimsingi sisi hatuna taarifa kama alikuwa ametumia dawa hilo ni swala la kidaktari”amesema Kamanda Banga .
RPC Banga amesema kutokana na aina ya tukio Jeshi la Polisi haliwezi kumkamata mwanamke aliye kuwa pamoja na marehemu huyo kwasababu wanaume wengi pia kwenye ndoa wamekuwa wakipoteza maisha kwasababu hiyo hivyo hawawezi kumkamata mtu kwa kufanya mauaji kwa tendo hilo.
Hata hivyo Diwani wa kata ya Ilembula Hezron Myale amesema kupitia taarifa ya familia ambayo imetolewa wakati wa mazishi yaliyofanyika leo katika kijiji cha Ilembula imebainisha kuwa sababu ya kifo cha Erasto Kabupa ni tatizo la moyo ambalo limekuwa likimsumbua kwa muda mrefu.
View attachment 3363704
Source: Ayo Tv
YUpo mwingine alifia kwenye kifua cha bar maid wake,,,huko huko nyanda za juuAibu sana
MmmhKule iringa ,, kuna kitu kinaitwa litambulilo ,, hii ni aina fulani ya mtego ambayo wanaume huwawekea wanawake sehemu zao za siri ili ikitokea kachepuka tu basi huyo mwanaume lazima kifo kimpate
Mwisho ni mwisho tuuRIP to him,
Ila kwenye maombi yetu, tusisahau kuomba mwisho mwema!